Nimeiangalia picha hii na kujikuta :-) ebu angalia hayo matembele na naona hapo kwenye hilo kapu kuna zaidi ila nikakaza moyo na kuendelea kuwaza.....
Jioni inaingia nimekaa hapa nawaza nini cha kupika mwanamke mimi...Ghafla natoka nje naangalia bustani . Uwiiiii..bado bado kabisa. Naingia tena mtandaoni ili kupata mawazo nakutana na picha hii. Kamoyo kanadunda na hamu ya kupa huo mchicha, matembele,chaina ...halafu naangalia akina mama walivyojipanga hapa nami naanza kupata wazo nitawauzia majirani mboga zangu...ujanja eeeh:-) Picha kutoka kwa Mjengwa.
Ngoja nikuelezeni jambo moja picha hiyo inanikumbusha kila jumapili Songea/manzense huwa ni siku maalumu kwa wakulima kwa hiyo kila kitu kinakuwa kimetoka tu shambani. EEeehh bwana wewe yaani mpaka raha kwa hiyo zimenifikisha mpaka huko na ndo hamu inazidi kwelikweli...
ReplyDeleteHuku nyumbani hatuchagua cha kupika bali tunapika kilichopo.
ReplyDeleteNyumbani ni nyumbani kwa kweli....
ReplyDeletenimeipenda hiyo NYUMBANI HATUCHAGUI CHA KUPIKA WALA HATUNA RATIBA KILICHPO NDO TWAPIKA HATA KA MWEZI MZIMA TWALA UGALI MBOGAMBOG AWALAAAAAAAAAAAAAAA HAITUSUMBUI
ReplyDelete@Yasinta;
ReplyDeleteUkisema bora mapishi na siyo mapishi bora kwa laazizi wako na familia yako,wenzako wanasema...........!!
tena mboga zote hapo shurti kwa ugali
ReplyDeleteWaboreshe mazingira.Kuweka chini namna hiyo si vizuri kiafya na hata kumvutia mteja.Watengeneze meza na juu take waweke hizo mboga na matunda.
ReplyDeleteNdugu zangu Ahsanteni sana kwa michango yenu...Maana bila uwepo wenu nisingepata nguvu...
ReplyDelete@Yasinta;
ReplyDeleteUwepo wako ndiyo furaha yetu na raha yetu ndiyo uwepo wako na bila uwepo wako hakuna raha wala furaha yetu.