Monday, June 11, 2012

TUANZE JUMATATU HII NA SWALI HILI:-JE NI KWELI?

Nakumbuka nilipokuwa mdogo wakati naishi kule Lundo kulikuwa na sehemu tulikuwa hatupiti. Kisa kulikuwa kunasemekana kuna JOKA kubwa ambali lilikuwa lina vichwa vitatu na pia lilikuwa linauma kichwani tu. Sijui kama ilikuwa kweli au ilikuwa ni njia ya kuwazuia watoto wasiende kule? je Nyoka kama huyu yupo kweli? na anatumia midomo yote kuuma? Katika wadudu/wanyama niwaogopao nyoka ni namba moja , ingawa sijawahi kuumwa na nyoka. Huwa nashangaa nionapo watu wana nyoka ndani ya nyumba  kwa ajili ya kufuga ......sipati jibu kwa nini....

1 comment:

  1. Habari hii imenikumbusha zamani hizo huko mjengoni.Waziri wa elimu zama hizo aliwahi kutoa kauli ya kuchekesha wakati aliposema:
    Nilipofika katika mkoa mmoja huko kanda ya ziwa niliuzwa kwa nini watendaji wengi wa serikali wanatoka katika mkoa mmoja huko kanda ya kaskazini?Waziri alijibu:"Wakati huko kanda ya kaskazini waliamua kuwekeza kwenye elimu huku kanda ya ziwa mliamua kuwekeza kwenye dawa ya nyoka".

    ReplyDelete