Thursday, June 21, 2012

Kisa Cha Mmasai Na Mchungaji Wa Kanisa...

Kuna kisa cha Mchungaji wa Kanisa la Kibabtisti aliyefika kijiji cha Wamasai Jumapili moja kuhibiri dini.
·        Mchungaji akawa na nia pia ya kuanzisha kanisa kijijini hapo.
·        Wamasai wakakusanyika kanisani. Baada ya kuhubiri Neno la Mungu kwa saa mbili, Mchungaji akaomba arudi tena kijijini hapo Jumapili inayofuata. 
·        ... Ndipo hapo akasimama Mzee wa Kimasai na kutamka;
Mzee wa Kimasai;
 ·        " E bwana Chungaji sisi iko furahia sana neno yako ya Mungu. Lakini, usije juma la kesho, ni kwa vile kuna ile padri ya Roman imesema inakuja kusema neno ya mungu pia."
Mchungaji: 
·        " Je, inawezekana nikaja Jumapili ya keshokutwa ?"
Mzee wa Kimasai: 
·        " Hapana, Chungaji, Jumapili ya keshokutwa kuna ile Imam ya Msikiti imesema inakuja kutupa mawaidha ya Kiislamu"
Mchungaji: 
 ·        " Sasa nyinyi hamuwezi kuchanganya dini na madhehebu, itabidi mchague!"
Mzee wa Kimasai: 
·        " Aisee Baba Chungaji, wewe iko chungaji na mimi pia ni chungaji. Zile ng'ombe nachunga zinakula majani pamoja. Wake zetu wanashinda na kufanya kasi pamoja. Watoto zetu wanacheza pamoja. Sasa sisi hatutaki hiyo dini inakuja kutagawa hapa"
HABARI HII NIMETUMIWA NA MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO NAMI NIKAONA NI VIZURI KUJUZANA.

3 comments:

  1. mmasai katisha...akili mingi sana huyo

    ReplyDelete
  2. Yaaani nakwambia amewaza chapuchapu Kwali miakili mingi...ha ha ha haaa nimecheka kweli yaaani...

    ReplyDelete
  3. Hapa kwa Masai ni masimamo tu na hakuna ile macheso.Kama wewe hamna masimamo na mambo yako sauri yako!

    ReplyDelete