Monday, June 25, 2012

Tuanze jumatatu hii kwa kuangalia jinsi watu walivyo:- Malezi ya watoto/Ukatili Kwa Watoto


Watu /binadamu tumeumbwa tofauti , labda pia ni jambo la kumshukuru Mungu. Maana fikiria kama wote tungekuwa wakatitili sijui ingekuwaje? Na kama wote tungekuwa wema sijui ingekuwaje??

4 comments:

  1. Ndio maana wanasema kuwa ukatili upo ndio maana kuna msamiati `ukatili' vinginevyo tusingejua kabisa kuwa kuna `wakatili'
    Hata hivyo sio hiyo sio tiketi ya kufanya ukatili....

    ReplyDelete
  2. @emu-three;
    Umelonga kiukweli!
    ==========================
    Mwanzo 4:1-26

    1 Basi Adamu akalala na Hawa mke wake naye akapata mimba. Baada ya muda akamzaa Kaini na kusema: “Nimezaa mwanamume kwa msaada wa Yehova.” 2 Baadaye akazaa tena, Abeli ndugu yake.

    Naye Abeli akawa mchungaji wa kondoo, bali Kaini akawa mkulima wa udongo. 3 Ikawa kwamba baada ya wakati fulani kwisha Kaini akaleta mazao ya udongo yawe toleo kwa Yehova. 4 Abeli naye akaleta baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa kundi lake, pia vipande vyao vyenye mafuta. Ingawa Yehova alikuwa akimtazama Abeli na toleo lake kwa kibali, 5 hakumtazama Kaini na toleo lake kwa kibali chochote. Ndipo Kaini akawaka hasira, na uso wake ukaanza kukunjamana. 6 Basi Yehova akamwambia Kaini: “Kwa nini umewaka hasira na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Ukigeuka utende mema, je, hutainuliwa? Lakini usipogeuka utende mema, kuna dhambi inayovizia katika mwingilio, nayo inakutamani wewe. Je, wewe utaishinda?”

    8 Baada ya hayo Kaini akamwambia Abeli ndugu yake: “Twende shambani.” Basi ikawa kwamba walipokuwa shambani Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua. 9 Baadaye Yehova akamuuliza Kaini: “Yuko wapi Abeli ndugu yako?” naye akasema: “Sijui. Kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” 10 Kwa hiyo akasema: “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika udongo. 11 Na sasa umelaaniwa kwa kufukuzwa kutoka katika udongo, ambao umefungua kinywa chake ili kupokea damu ya ndugu yako kwa mkono wako. 12 Utakapoulima udongo, hautakurudishia nguvu zake. Utakuwa mwenye kutanga-tanga na mkimbizi duniani.” 13 Kwa hiyo Kaini akamwambia Yehova: “Adhabu yangu ya kosa ni kubwa mno, haichukuliki. 14 Tazama unanifukuza leo kutoka usoni pa udongo, nami nitafichwa kutoka usoni pako; nami nitakuwa mwenye kutanga-tanga na mkimbizi duniani, na itakuwa kwamba yeyote atakayenikuta ataniua.” 15 Ndipo Yehova akamwambia: “Kwa sababu hiyo yeyote anayemuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba.”

    Hivyo Yehova akaweka ishara kwa ajili ya Kaini ili kwamba yeyote anayemkuta asimpige. 16 Ndipo Kaini akaenda zake kutoka usoni pa Yehova na kukaa katika nchi ya Ukimbizi upande wa mashariki wa Edeni.

    17 Baadaye Kaini akalala na mke wake naye akapata mimba, akamzaa Enoko. Kisha akajishughulisha na ujenzi wa jiji, akaliita hilo jiji kwa jina la mwana wake Enoko. 18 Baadaye Enoko akazaa mwana anayeitwa Iradi. Na Iradi akamzaa Mehuyaeli, na Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki.

    19 Na Lameki akajichukulia wake wawili. Jina la wa kwanza lilikuwa Ada na jina la wa pili lilikuwa Zila. 20 Baada ya muda Ada akamzaa Yabali. Akawa mwanzilishi wa wale wanaokaa katika mahema na walio na mifugo. 21 Na jina la ndugu yake lilikuwa Yubali. Akawa mwanzilishi wa wote wanaotumia kinubi na zumari. 22 Zila naye pia akamzaa Tubal-kaini, mfuaji wa kila namna ya vifaa vya shaba na chuma. Na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. 23 Basi Lameki akatunga maneno haya kwa ajili ya wake zake Ada na Zila:

    “Sikieni sauti yangu, enyi wake za Lameki;
    Tegeni sikio kwa maneno yangu:
    Nimemuua mtu kwa kunitia jeraha,
    Naam, kijana kwa kunipiga.

    24 Ikiwa Kaini atalipizwa kisasi mara 7,
    Basi Lameki ni mara 77.”

    25 Naye Adamu akalala na mke wake tena naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sethi, kwa sababu, kama alivyosema: “Mungu amenichagulia uzao mwingine badala ya Abeli, kwa sababu Kaini alimuua.” 26 Na Sethi akazaa mwana pia naye akamwita jina lake Enoshi. Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Yehova.

    ReplyDelete
  3. Dunia inamabo sijui watu wana mambo!!yaani inasikitisha mno.


    Asante da'Kadala.

    ReplyDelete
  4. Ndugu zanguni mliotangulia em3, Ray na Kachiki/Rachel hakika kweli duniani kuna mambo. Na ni mambo hasa na yanatia huruma na kusikitisha. Nimewahi kusikia pia watu wa hivyo/wanaokuwa wakatili hivyo inasemekana katika malezi yao walifanyiwa hivyo. Ila duh! ako katoto ka miaka 6-7 kalivyofanyaiwa nimeshindwa kuvumilia na kuishia kulia tu.

    ReplyDelete