Wednesday, June 27, 2012

KWELI ZILIPENDWA HASWA!!!!

NI KILE KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO YA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUWA HAPA HAPA YAANI NDANI YA BLOG HII KWA KURUDIA NA PICHA HII NILISHAWAHI KUIWEKA  KWA KUKUMBUSHA ANGALIA HAPA KAPULYA. KARIBUNI SANA.....
Kitu kimoja nasikitika sina picha ambayo nilikuwa kabinti kadogo sana. Najiuliza sijui nilionekana vipi lakini sipati jibu. Panapo majaliwa tuonane tena JUMATANO IJAYO....Kaaaazi kweli naipenda zamani/zilipendwa kwa kweli..inaonekana niliupenda huo mpapai au sijui ndo ulikuwa mtindo kusimama kwenye miti..LOL

32 comments:

  1. u mrembo sana my dada, enzi zako hizoooooo, matunda kwa afya si lazima dokta aseme, jumatano njema pia

    ReplyDelete
  2. Katika picha hiyo ya mwaka 1993 namwona Camila!!!! Ama kweliiii

    ReplyDelete
  3. Daaah ulikuwa bomba sana mtani wangu.

    ReplyDelete
  4. Zilipendwa na zinaendelea kupendwa,hahahahaaaa hapo upo bombi kweli,kweli mtani wangu...lol!

    ReplyDelete
  5. Kichagga wanasema:Nokuo na ucha wopfo[Unazeeka na uzuri wako].

    ReplyDelete
  6. Ray una misemo weweeeee, ila msemo wako una ukweli ndani yake

    ReplyDelete
  7. Hongera sana dada kwa nguo zako za heshima tangia enzi hizoooooo lakini yee sketi yavii ya mpyela yeniyo mbomi rahaa mbaka mmoyo - bambu mbawala

    ReplyDelete
  8. @Ester;
    Asante sana kwa pongezi zilizohanikizwa na shukrani ndani ya asante kutoka katika papachi za moyo wako.Kama vile chumvi na nazi huongeza ladha katika maharage na mboga za maji bila kusahau mlo wote kwa ujumla wake na misemo huongeza ladha ya mazungumzo na utamu wa hadithi unazidi kukolea.
    Picha ya Yasinta inatukumbusha kuwa mavi ya hayanuki na daima ya kale ni dhahabu.Mwanamke anayedumisha maadili na staha ya kike anapaswa kuiga kielelezo za picha hii kwa kuchagua mavazi yanayoweza kuhifadhi vema maumbile yake ya kike kwa kuwa hiyo ndiyo fahari ya mwanamke.Wanawake wanaweza au ni lazima wawezeshwe kwanza???Nashindwa kuwaza kwa sauti!!!

    ReplyDelete
  9. Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa uwepo,pongezina upendo wenu. Ni ruksa kuendelea na mada/picha hii ya leo.

    ReplyDelete
  10. @Yasinta;
    Kwa upendo wako tumekupokea na jehazi moja bado tunasafiria.Omo na tezi marejeo ngamani.

    ReplyDelete
  11. Yaani mwali wewe ulikuwa mrembo tangu zamani!!!!!!

    ReplyDelete
  12. @Rachael;
    Umeamua tucheke au????

    ReplyDelete
  13. Yaani hapa umefanana na rafiki yangu mmoja anaitwa Twendilwe...yaani duh!

    Yasinta wewe fashionista, ni basi tu!!
    Kumbe makorokoro ya kiafrika shingoni umeyaanza siku nyingi?

    Hongera sana Da'Mkuu..

    ReplyDelete
  14. Huu mpapai umenikumbusha nika post kilimo cha mipapai leo

    ReplyDelete
  15. Heri mimi sijasema, ...lakini ngoja niseme,hii picha ndiyo ile uliyompa shemeji kipindi kile...!

    ReplyDelete
  16. @emu-three;
    Makofi kwako tafadhaliiiiiiiiiiii!!!
    Umesema na wote wamesikia na huenda huo ndiyo ukweli wenyewe au yeye mwenyewe anasemaje?

    ReplyDelete
  17. Jamni kaka Ray kwanini mcheke?au kwa furaha!!!!!pamoja sana.

    ReplyDelete
  18. Mtoto mzuri kweli weye! Ungekuwa hauna Mmme...........yani sijui!:-(@Kadala

    ReplyDelete
  19. We Kapulya we Kapyula. Acha nijiachie unyayo. Maana mengi yameishasema.

    ReplyDelete
  20. Ray..Ahsante!!
    Rachel! unajua kuchekesha wewe!! si unaona hadi kaka Ray kacheka:-)
    Mija! duniani wawili wawili.. fasheni..tumetoka mbali..
    Kaka Benet! nafurahi kama umepata kumbukumbu.
    Emu3!wewe kumbe muchukozi..ngoja nimuulize kama ni hii..LOL
    Ray! ha ha haaa unajuaje kama kapatia?
    Rachel!ni kweli umenifanya hata mie nicheke..kwa furaha:-)
    Simon/Kadoda! mbona hujamalizia hapo kwenye deshi?
    Mwl.Mhango Ahsante kwa kupita hapa nina hakika hata nawe ulikuwa na la kusema ambalo tayari umesema...

    ReplyDelete
  21. Wow! you have not changed much. You have really taken good care of yourself and still look young.

    ReplyDelete
  22. @Samuel;
    That is good,very goooooood!!!!!

    ReplyDelete
  23. Brother Samuel! I am trying thank you so much...

    ReplyDelete
  24. Kitururu Kitururu,..mbona wako wengi tu wasokuwa na waume? mi naona kakangu labda una masharti magumu mno hadi wadada wanaona isiwe taabu, kweli si kweli??

    Stay blessed u all..

    ReplyDelete
  25. @Simon;
    Hoja ndiyo hiyo na wadau tunasubiri mchango wako kibarazani kwa kadala!!!

    ReplyDelete
  26. umenikumbusha mbali sana nafikiri hapo ni wilima on those days

    ReplyDelete
  27. Mie Msumbufu sitaki kusumbua Mtu!:-)@Mwanamke wa Shoka Mija

    @Kapulya/Kadala: Mambo mengine siri!:-)

    ReplyDelete
  28. @Simon;
    Uhuru wako uanaishia pale wa mwenzako unapoanzia.Mkuu umesomeka vema na hoja binafsi imekamilika.

    ReplyDelete
  29. Hahahaha@Mtani wangu Mchungaji Ray

    ReplyDelete
  30. @Simon;
    Asante sana kwa maneno mazuri na kumbuka kuwa mimi ni mtenda kazi asiye na faida na hapa natimiza tu kile ambacho huenda kikawa ndiyo matarajio ya jamii yangu.

    ReplyDelete