Majira ya saa nne leo binti yetu Philomena Ngonyani katuacha baada ya kuumwa kwa kipindi kirefu. Tunamwomba eeehh Mwenyezi Mungu atutie nguvu katika kipindi hiki chote kigumu.
Nitakukumbuka daima Shangazi yangu,
Friday, December 30, 2016
HII IWE PICHA YA MWISHO YA WIKI HII NA LABDA MWAKA HUU 2016
Mara nyingi inasemekana ni wanawake tu huweza kufanya vitu zaidi ya viwili lakini hapa katika picha twaona kinyume....
UJUMBE WA LEO:- Nachukua fursa hii kuwashukuruni wasomaji wote wa MAISHA NA MAFANIKIO kwa kuungana nami kila siku. Maana bila ninyi nisingeweza kuendelea kublog maana hizi zote ni juhudi zenu. AHSANTENI SANA NA TUZIDI KUPEANA MOYO. KAPULYA
UJUMBE WA LEO:- Nachukua fursa hii kuwashukuruni wasomaji wote wa MAISHA NA MAFANIKIO kwa kuungana nami kila siku. Maana bila ninyi nisingeweza kuendelea kublog maana hizi zote ni juhudi zenu. AHSANTENI SANA NA TUZIDI KUPEANA MOYO. KAPULYA
Wednesday, December 28, 2016
MANISPAA YA SONGEA:- MAZINGIRA NA WATU WAKE
Sehemu ya eneo la Msitu wa Matogoro ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea
Wananchi wa Kijiji cha Chikunja Kata ya Matimila Tarafa ya Muhukulu
Wananchi wa Kata ya Kilagano waliokuwa wanafanya shughuli za Kilimo katika eneo la Hifadhi ya misituCHANZO CHA PICHA:- HAPA
Tuesday, December 27, 2016
BARABARANI SEHEMU FULANI MKOANI RUVUMA ...JE? UNAJUA WAPI?
Mazingira ...barabarani sehemu fulani mkoani Ruvuma ...unajua ni wapi?....zawadi nono imeandaliwa kwa wa watano wa kwanza kujibu:-)
Monday, December 26, 2016
UJUMBE KUTOKA KWANGU KUJA KWENU KWA KUFUNGA MWAKA HUU 2016.
kinaitwa furaha hapa duniani.....
Yote ni mzunguko wa maisha tunapita milima na mabonde, kwenye miiba na kwenye asali kitu cha muhimu ni kumuomba Mungu na kumshukuru kwa chochote kinachokuja mbele yako
Sunday, December 25, 2016
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KRISMASI NJEMA..PICHA MKESHA WA KRISMAS
mtoto Yesu kalazwa holoni
Baraka na amani zitawale katika nyumba zet pia upendo . Leo ni sikukuu ya kuzaliwa/kumbukumbu ya Mkombozi wetu Yesu Kristo. UJUMBE TUPENDANE, NA MUHIMU ZAIDI TUKUMBUKANE. KRISMAS NJEMA KWA WOTE MTAOPITA HAPA....
Wednesday, December 21, 2016
MAPISHI YA LEO:- PAI YA SPINACHI NA SALADI YA NYANYA
Ni pai spinachi:- unahitaji unga wa ngano vikombe 3 vya chai/3dl tatu, samli 125g, maji vijiko 3 vya mezani. Kisha maziwa vikombe 2/dl 2, na mayai mawili koroga pamoja na chumvi pia pilipili manga. Baada ya hapo katakata kitunguu maji kimoja na kipande kimoja cha kitunguu saumu kaanga ila usiunguze kisha changanya spinachi geuza geuza kidogo. weka kinyunga kwenye chombo na weka kwa oven dakika kumi. Halafu weka spinachi na vitunguu halafu chizi/jibini vikombe viwili na mwisho yale maziwa na mayai uliyokoroga pamoja. weka kwa oven uliyoiandaa kwa joto la 225 kwa dakika 30...Tayari kwa mlo:-)
Usisahau na kasaladi kidogo...mimi nilichagua nyanya tu ila saladi yoyote ni safi tu ....TUKUTANE TENA SIKU NYINGINE.....KAPULYA
Usisahau na kasaladi kidogo...mimi nilichagua nyanya tu ila saladi yoyote ni safi tu ....TUKUTANE TENA SIKU NYINGINE.....KAPULYA
Tuesday, December 20, 2016
SALAMU KUTOKA KWETU RUHUWIKO...KAZI YA MIKONO YANGU...
Nakumbuka siku niliyopanda hili nanasi na mengine nilichekwa sana nikaambiwa nadhani watu wanapanda kama mihogo. Ila sikukata tamaa leo matunda ni haya:-) KAZI YA MIKONO YANGU
Na hapa ni ndizi... kwa hiyo ndugu zanguni karibuni sana Ruhuwiko ...
Monday, December 19, 2016
Sunday, December 18, 2016
NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA-VAZI LA LEO CHUI CHUI:-)
Leo ni shati la chui chui na sketi nyeusi
Friday, December 16, 2016
Wednesday, December 14, 2016
HILI NENO, "MWANAUME NI KICHWA CHA NYUMBA," HUWAPA KIBRI SANA HAWA VIUMBE
Kuna jambo moja ambalo hufundishwa na viongozi wa dini mbalimbali, ambalo pia waumini hulihubiri vizuri kila mahali wapatapo nafasi ya kufanya hivyo. Nalo si jingine ni lile la ‘mwanaume ni kichwa cha nyumba,’ ikiwa na maana kuwa mwanaume ndiye mkuu wa nyumba au familia. Suala hili linazungumzwa kama kwamba, mwanaume kuwa mkuu wa familia ni jambo la kimaumbile, lakini pia huzungumzwa kama vile, ukuu huo ni tiketi ya mwanaume kuikandamiza familia au mke.
Nijuavyo mimi, wanaume wengi kuwa wakuu wa nyumba au familia ni suala la mazoea zaidi kuliko maumbile. Kwa miaka milioni kadhaa, mwanaume amejikuta akiwa ndiye mkuu wa familia. Kutokana na mazoea haya, jambo hili limekuwa kama vile ni la kimaumbile, yaani haliwezi kubadilika au kubadilishwa.
Lakini mbona kuna wanawake ambao ndiyo wakuu wa familia na familia hizo zinakwenda vizuri tu. Lakini vilevile kuna wanawake ambao hawana waume na wanaongoza vyema familia zao. Kwa bahati mbaya kwenye jambo hili, ni kwamba, kumekuwa na msisitizo kuwataka wanawake wawaheshimu waume na siyo wanandoa kuheshimiana. ‘mwanaume ni kichwa cha nyumba, ndiye msemaji wa mwisho. Inabidi aheshimiwe.’ Kuna watu ambao bila aibu huzungumza lugha hii.
Ni kweli wanaume wanahitaji au wanapaswa kuheshimiwa. Lakini siyo wanaume peke yao, bali binadamu wote wanapaswa kuheshimiwa bila kujali wanafanya nini au wakoje. Kwa hiyo siyo kwa sababu ni wasemaji wa mwisho, basi wao ndiyo wanaopaswa kuheshimiwa. Kwa kuamini hivyo wanaume wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kuwakandamiza wake zao na hata watoto. ‘Mimi ndiyo msemaji humu ndani, nimesema sitaki, basi.’ Mara nyingi matumizi ya mabavu kwa namna hiyo hutumika.
Kuna haja kwa wanaume kujua kwamba, kuwa kwao viongozi wa familia hakuwapi ubora wa ziada. Wanawake nao wanapaswa kujua kwamba, kutokuwa kwao wasemaji wa mwisho wa familia, hakupunguzi hata chembe ya thamani ya ubinadamu wao, kwani binadamu na wanandoa wanapaswa kuheshimiana.
HABARI HII NIMEITOA KWA MDOGO WANGU KOERO HAPA
Tuesday, December 13, 2016
Monday, December 12, 2016
SIKU NA WIKI NYINGINE TENA ....AMBAYO TUNAANZIA KATIKA ZIWA NYASA KWETU
Wavuvi wa dagaa wanatua nanga ufukweni tayari kusubiri wateja. Na mimi niliuwa mteja wa kwanza......wahi nawe upate kitoweo:-)
Sunday, December 11, 2016
NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA TATU YA KIPINDI HIKI CHA MAJILIO IWE NJEMA...!
NUKUU "Mpendwa mwana wa Mungu, tukiendelea kwa furaha katika Majilio, leo tunaendelea kulitazama Neno la Mungu kwa furaha ili tujifunze na kuonja upendo wa Mungu kwa njia ya Neno wake. Ni Dominika ya III ya Kipindi cha Majilio, Mwaka C wa Kanisa, tukialikwa kufurahi kwa uchangamfu kwa maana Bwana yu karibu. Kama kawaida Dominika ya III ni Dominika ya furaha, kumbe, furahini katika Bwana. Katika Dominika hii tunatafakari Neno la Mungu pia tukimtazama Mtakatifu Yosefu, Baba mlishi wa Bwana."
JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGU. UJUMBE TUPENDANE!
Thursday, December 8, 2016
LEO JIKONI:- MAPISHI YA MAANDAZI
Wednesday, December 7, 2016
PICHA YA WIKI: VAZI LA KITENGE..SARESARE MAUA
Tuesday, December 6, 2016
MANGATUNGU (VELVET BEANS AU COWITCH BEANS) NI CHAKULA KWETU UNGONINI
KWETU UNGONINI TUNAITA MANGATUNGU. Chakula hiki inabidi upike kwa makini sana. Kwanza unachemsha kisha unamenya. Na hapo kazi inaanza unachemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi. Sababu ni kwamba inasemekana kuna sumu ndio maana maji ya mwanzo huwa meusi sana . Kwa lugha ya kiingereza huitwa "velvet beans au cowitch beans"...pia inasemekana:- Mangatungu ni dawa kama viagra, ni kahawa, na ni dawa ya kutibu magonjwa ya nerves kama vile Parkinson disease. Kwa habari zaidi soma http://en.wikipedia.org/wiki/Mucuna_pruriens#Uses
N a baada ya kuchemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi na mwisho wake matokeo yake huwa hivi tayari kwa kula...ni chakula kizuri cha asili...
N a baada ya kuchemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi na mwisho wake matokeo yake huwa hivi tayari kwa kula...ni chakula kizuri cha asili...
Monday, December 5, 2016
KARIBUNI SONGEA: FAHAMU BAADHI YA MAMBO HALISI YA MJI WA SONGEA
Karibuni Songea Mji wa kitalii:
1. Kuna matuta makubwa ya barabarani Tanzania nzima (bumps) yapo Bombambili ambapo kabla ya
kufika Songea mjini lazima ukutane nayo.
2. Kuna pikipiki nyingi kuliko watu.
3. Kuna matunda mengi ya kipekee kama madonga, masuku, mfudu, mbula, mamvubula na mengine mengi.
4. Kuna mboga nyingi za kipekee kama Mangaukau, linamfusulela, chikandi, likungu, kipele,pitiku(mboga ya maboga),
mangatungu n.k.
5. Majina mengi ya watu wake ni ya wanyama mfano Komba, Mapunda, Mbawala, Tembo,
simba (Kahimba), Nungu, Nyoka, Matembo, Ngonyani, Nyati, Kobe n.k.
6. Pia kuna ngoma nyingi mf. lizombe/kitoto, madogoli, beta, zilanga, ligambusa, kihoda, mganda, lindeku,
Mandilo, Chomanga, Tumba, Puyanga.
7. Bila kusahau Dagaa watamu sana (Nyasa) na viazi vitamu kuliko vyote vinavyojulikana kwa jina
la makaba.
Hiyo ndiyo SONGEA yetu, Mji uliobarikiwa, Chezea Songea yetu weye. KARIBUNI SANA HAPA NI BAADHI TU YA UHALISIA WA MJI HUU.
Friday, December 2, 2016
KANGAZIII:- IJUMAA NJEMA NDUGU ZANGU!
Haya jamani niseme kama mwalimu wa hesabu wa shule ya msingi alivyoitwa MWALIMU MWEZI MPYA ...nilikuwa namaanisha ni mwezi mpya na ni Ijumaa ya kwanza ya mwezi huu mpya na ni mwisho wa juma...nami nawatakieni IJUMAA NJEMA SANA!
Thursday, December 1, 2016
TUANZE MWEZI WA KUMI NA MBILI HUU KIHIVI..PALE UPATAPO UGENI......
Ilikuwa siku ya furaha sana hii siku ...kama picha inavyojionyesha. Huwa napenda sana kufikiwa na wageni ni raha ilioje...Hawa wageni walitoka Bukoba.