Karibuni Songea Mji wa kitalii:
1. Kuna matuta makubwa ya barabarani Tanzania nzima (bumps) yapo Bombambili ambapo kabla ya
kufika Songea mjini lazima ukutane nayo.
2. Kuna pikipiki nyingi kuliko watu.
3. Kuna matunda mengi ya kipekee kama madonga, masuku, mfudu, mbula, mamvubula na mengine mengi.
4. Kuna mboga nyingi za kipekee kama Mangaukau, linamfusulela, chikandi, likungu, kipele,pitiku(mboga ya maboga),
mangatungu n.k.
5. Majina mengi ya watu wake ni ya wanyama mfano Komba, Mapunda, Mbawala, Tembo,
simba (Kahimba), Nungu, Nyoka, Matembo, Ngonyani, Nyati, Kobe n.k.
6. Pia kuna ngoma nyingi mf. lizombe/kitoto, madogoli, beta, zilanga, ligambusa, kihoda, mganda, lindeku,
Mandilo, Chomanga, Tumba, Puyanga.
7. Bila kusahau Dagaa watamu sana (Nyasa) na viazi vitamu kuliko vyote vinavyojulikana kwa jina
la makaba.
Hiyo ndiyo SONGEA yetu, Mji uliobarikiwa, Chezea Songea yetu weye. KARIBUNI SANA HAPA NI BAADHI TU YA UHALISIA WA MJI HUU.
Sasa kama ni pikipiki nyingi kuliko watu, nani anaziendesha?
ReplyDeleteJust a joke!
Ahsante sana Mtani kwa ukaribisho wako wa Songea.
Haaaa :-) Mtani bwana umenichekeshaje na huo utani wako-:) Karibu sana Songea maana wewe unapenda sana Pitiku :-)
ReplyDeletedah kweli "HOME SWEET HOME"
ReplyDelete