Friday, December 30, 2016

FAMILIA YA AKINA NGONYANI IMEPATWA NA MSIBA ....BINTI PHILOMENA HATUNAYE TENA

Majira ya saa nne leo binti yetu Philomena Ngonyani katuacha baada ya kuumwa kwa  kipindi kirefu. Tunamwomba eeehh Mwenyezi Mungu atutie nguvu katika kipindi hiki chote kigumu.
Nitakukumbuka daima Shangazi yangu,

13 comments:

  1. Poleni sana kwa msiba. Philomena ametutangulia tu, sie sote tupo njia moja. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana kwa msiba. Philomena ametutangulia tu, sie sote tupo njia moja. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  3. Kaka Evarist! Ahsante sana kwa pole na pia kwa kutupa matumaini kwa kipindi hiki kigumu. Amina.

    ReplyDelete
  4. Daah! polen sana wapendwa kiukweli hakuna anaejua dakika inayofuata atakua ktk hali gani, sote tuu wake na kwake tutarejea...tuzidi kujiweka tayari kwa saa hiyo maana kila nafsi itaionja mauti...dada yetu katangulia nasi tunafatia ee mwenyez mungu mpokee mja wako

    ReplyDelete
  5. Prince Emac...Amina. Twasukuru kwa kuwa nasi katika msiba wa binti Philomena.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana wanafamilia ya Ngonyani. Mungu azidi kuwatia nguvu katika hali mnayopitia sasa.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana Dada na Familia yote ya Ngoyani. Mungu awape wepesi kipindi hiki kigumu. Naungana nanyi kumwombea Da Philomena apumzike kwa Mungu palipo pema daima.

    ReplyDelete
  8. Mungu awatie nguvu na kuwafariji. Hii ni safari ya kila mmoja. Kinachogomba ni kwamba hatujui saa wala siku.

    ReplyDelete
  9. Poleni Sana Kwa msiba wa binti yenu Philomena, Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Amin na awape wepesi Inshaallah. By Salumu.

    ReplyDelete
  10. AHSANTE WOTE KWA KUWA NASI WANAFAMILIA ...KWA TAARIFA NI KWAMBA MAZISHI NI KESHO JUMATATU.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana. Mungu awape ustahumilivu na amweke ndugu yenu katika raha ya milele. Amina.

    ReplyDelete
  12. Goodbye friend.... RIP philomena

    ReplyDelete
  13. Ndugu yangu Mbele... Ahsante sana kwa kuwa nasi kwa kipindi hiki kigumu...

    Ayubu Ahsante!

    ReplyDelete