Wednesday, December 21, 2016

MAPISHI YA LEO:- PAI YA SPINACHI NA SALADI YA NYANYA

Ni pai spinachi:- unahitaji unga wa ngano vikombe 3 vya chai/3dl tatu, samli 125g, maji vijiko 3 vya mezani. Kisha maziwa vikombe 2/dl 2, na mayai mawili  koroga pamoja  na chumvi pia pilipili manga. Baada ya hapo katakata kitunguu  maji kimoja na kipande kimoja cha kitunguu saumu kaanga ila usiunguze kisha changanya spinachi geuza geuza kidogo.  weka kinyunga kwenye chombo na weka kwa oven dakika kumi. Halafu  weka spinachi na vitunguu halafu chizi/jibini vikombe viwili na mwisho yale maziwa na mayai uliyokoroga pamoja. weka kwa oven uliyoiandaa  kwa joto la 225 kwa dakika 30...Tayari kwa mlo:-)
Usisahau na kasaladi kidogo...mimi nilichagua nyanya tu ila saladi yoyote ni safi tu ....TUKUTANE TENA SIKU NYINGINE.....KAPULYA

2 comments:

  1. Rafiki wa mimi habari za siku, kwanza nianze na kukiri nilikua nimepotea humu ndani siku nyingi sasa leo naingia tu nakutana na mapishi ya kuvutia nataka nikajaribishe jioni ya leo si unajua kaka M yupo likizo.

    Sasa n ina swali, ukisema samli unamaanisha nini? Au ni sawa na margarine?

    ReplyDelete
  2. Rafiki yangu upo sawa kabisa...halafu unaweza kutengeneza kachumbali huwa nafanya hivyo ni tamu ila niliamia kufanya tofauti kila la kheri. ..

    ReplyDelete