RUVUMA....MKUU WA MKOA WA RUVUMA AKUTANA NA BARAZA LA WAZEE WA KUMBUKUMBU YA VITA YA MAJIMAJI


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  akutana na Baraza la wazee wa kumbukumbu ya vita vya majimaji ambapo pia alipata nafasi ya kutembelea maeneo ya makumbusho. Tunawashukuru na tutaendelea kuwaenzi mashujaa wetu waliopigania haki za watanzania na kukataa kutawaliwa na wakoloni. Mungu awarehemu. Amina


Jumatatu njema ndugu zanguni...ni jumatano ya mwisho ya mwezi huu wa kwanza/januari

Friday, January 26, 2018

KARINUNI TUJUMUIKE MCHANA HUU NDUGU ZANGU!

Ugali, samaki sato na mchicha bila kusahau pilipili...karibuni mchana huu tujumuike. Ijumaa njema

Wednesday, January 24, 2018

HIZI NI PICHA ZA WIKI HII ZA....AMBAZO NI ZA MBWEMBWE KIDOGO.....

 Ndani  ya suti 2012
Hapa sijui  ni ngoma  gani 2017 Peramiho

Monday, January 22, 2018

NYASA NI MAARUFU KWA KILIMO CHA MATUNDA

 
Hapa ni kijiji cha Ndengele katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma tulimkuta kijana anauza ndizi mkungu mzima shilingi 2000 tu.


Katika eneo la Liuli tulikuta mananasi matatu yanauzwa shilingi 1000.

NB; Albano Midelo

Friday, January 19, 2018

SALAMU KUTOKA RUHUWIKO/SONGEA NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA

Ni mwisho wa juma mwingine tena nami napenda kuwatakieni wote  WAKATI MZURI WENYE AMANI, FURAHA NA AMANI VITAWALE MIOYONI MWENU....TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE,,,.....KAPULYA WENU.


Thursday, January 18, 2018

LEO TUANGALIE MAZINGIRA YA KWETU RUHUWIKO NYUMBANI KWA KAPULYA WENU

 Hapa ni shamba, kwa kawaida tulitaka sehemu hii iwe sehemu ya bustani ya matunda kama muonavyo migomba ya ndizi, kuna miti ya machungwa, miti ya mipapai,  pilipili, manananasi na mahindi pia yapo ila hapo baadaye itakuwa ni matunda tu.
 Hapa ni mti wa parachichi nadhani karibuni tutaanza kula
 Hapa ndo palishinda kila kitu maana hii ni mboga  niipendayo sana  sana matembele:-).....

...unapopika vyakula vingi hususani tembele ni tamu ukiweka limao kwa mbali basi kapulya wenu anao mti wa limao ....TUKUTANE TENA PANAPO MAJALIWA....KARIBUNI RUHUWIKO KWETU:-)

Wednesday, January 17, 2018

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA HII IWE PICHA YA WIKI

Nikiangalia hii picha nakumbuka/najikumbuka mwenyewe jinsi tulivyokuwa kule kijijini KINGOLE tulikuwa na shamba la mihogo mbali kidogo mtaa wa LEGEZA...Basi nakumbuka  sana enzi zile.

Monday, January 15, 2018

LEO TUANZA JUMATATU HII KIHIVI...KARIBUNI TUFINYANGE NDUGU ZANGU

....Na  kabla ya kula yatupasa kumshukuru Mungu....haya na sasa tuanze kufinyanga kwa pamoja.

Friday, January 12, 2018

SIJUII KUZALIWA TANZANIA...TUPENDANE


NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA JUMA. TUSIKAMANE NA TUTAKIANE UPENDO NA AMANI PIA FURAHA DAIMA

Tuesday, January 9, 2018

NILIPOKUWA SAFARINI ....NYUMBANI RUVUMA 2017 NA HAPA BAADHI YA PICHA NA MATUNIO...

Hii ni barabara toka Songea kwenda Peramiho ..miaka 3 iliyopita hiki kibao hakikuwepo ...maendeleo ni kasi sana inafurahisha:-)
Kutua ardhi uliyozaliwa sio mchezo ni raha sana  kama muonavyo Mungu anavyoshukuriwa na hapa pia ni Peramiho
Na raha inaongezeka pale unapokutana na ndugu  kama hapa huyu ni binti  Lucy ni binti ya kakangu.
kwa leo tuishie hapa  panapo majaliwa na tutaendelea na picha pia matukio mengine ya huko Ruvuma kwetu.....

Friday, January 5, 2018

NACHUKUA NAFASI HII KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUNIONGEZEA MWAKA MWINGINE TENA

Namshukuru Mwenyezi Mungu,  kwa kuniongezea mwaka mwingine katika maisha yangu....kuna wengine walizaliwa siku kama hii lakini hawapo duniani kusherekea siku yao.
Hongera  kwa mimi na wengine wote waliozaliwa siku kama hii......uzee nao ndo huuoo unanivizia KARIBUNI KUSHEREHEKEA NAMI:-)

Monday, January 1, 2018

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KHERI YA MWAKA MPYA 2018

KARIBU TUANZE MWAKA MPYA KWA  MTINDO HUU UGALI NA MAHAREGE, MBOGA MAJANI NA MLENDA.
TUMALIZIA NA KUSIKILIZA KIPANDE HIKI CHA MZIKI

KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2018...