Thursday, January 18, 2018

LEO TUANGALIE MAZINGIRA YA KWETU RUHUWIKO NYUMBANI KWA KAPULYA WENU

 Hapa ni shamba, kwa kawaida tulitaka sehemu hii iwe sehemu ya bustani ya matunda kama muonavyo migomba ya ndizi, kuna miti ya machungwa, miti ya mipapai,  pilipili, manananasi na mahindi pia yapo ila hapo baadaye itakuwa ni matunda tu.
 Hapa ni mti wa parachichi nadhani karibuni tutaanza kula
 Hapa ndo palishinda kila kitu maana hii ni mboga  niipendayo sana  sana matembele:-).....

...unapopika vyakula vingi hususani tembele ni tamu ukiweka limao kwa mbali basi kapulya wenu anao mti wa limao ....TUKUTANE TENA PANAPO MAJALIWA....KARIBUNI RUHUWIKO KWETU:-)

No comments:

Post a Comment