Sunday, January 31, 2016

JANA JUMAMOSI YA TAREHE 30 /1/2016 ILIKUWA KUMBUKUMBU YA MT.YASINTA MTAWA...

Mt Yasinta Mtawa

Leo tunamkumbuka Mt Yasinta mtawa.Alizaliwa Viterbo,Italia mwaka 1585.Alisoma katika shule ya masista hapo Viterbo.Yeye alilazimika kuingia utawa katika shirika la  Wafranciscan,baada ya kuugua na kuitiwa Padri kwa ajiri ya kumkomunisha.Padri alipoingia chumbani kwake,aliona kuwa  Mt Yasinta aliishi maisha mabaya.Padri alimshauri kubadili mfumo wa maisha yake.Aliingia utawa,akafuata ushauri wa Padri.Miaka 24 baadaye,akiwa mtawa,aligeuka kuwa mfano wa kila kitu chema.Tabia njema,UchaMungu,na kusaidia watu wote.Alikufa mwaka 1640 Januari 30.Alitangazwa mwenyeheri  Septemba 1,1726.Alitangazwa mtakatifu mwaka 1807 Mei 24 na Papa Pius wa Vll

Watakatifu wengine wa Leo ni

Mt. Aldegunais
Mt. Aleaunie
Mt. Alexander
Mt. Armentarius
Mt. Armentarius
Mt. Barsimaeus
Mt. Bathildis
Mt. Felician
Mt. Hippolytus
Mt. Martina of Rome
Mt. Matthias wa Jerusalem
Mt. Mutien-Marie Wiaux
Mt. Savina wa Milan
Mt. Tudy
NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI  NJEMA! NA TUMWOMBE MT. YASINTA  ATUOMBEE WOTE!

Friday, January 29, 2016

BADO NIPO KIJIJINI KWETU LUNDO NA NDOTO ZANGU ZA VYAKULA....LEO NIMEKUMBUKA MBAAZI...

 Usifikiri ni maua yoyote yale ..hapana ni maua ya mti/mmea wa kunde aina ya MBAAZI au wengine husema kunde miti.  Ninazipenda sana....
...hapa zimeanza kukomaa tayari kwa kula kama muonavyo. Ni tamu sana kwa wali pia Ugali. Ila binafsi napenda zaidi kwa wali

Thursday, January 28, 2016

AMA KWELI...LEO NIMEYAKUMBUKA SANA HAYA MATUNDA ....

Nilipokuwa msichana mdogo wakati tukiishi kijiji cha LUNDO huko nyasa, nyumbani kwetu tulikuwa na miti miwili ya matunda haya. Nasi tulikuwa tukiyaita "farafaraji" (Red mulberry).....ni matamu sana. Pia kitu kimoja nilikuwa najivuna ni kwamba nilikuwa sikosi marafiki  tulikuwa tukila pamoja...Nimeyakumbuka sanaaa:-)

Wednesday, January 27, 2016

MWANAMAMA MFANYABIASHARA KATIKA SOKO KUU LA SONGEA....


Inasemekana kuwa, akina mama wa Tanzania wamechangamka katika ujasiriamali. Katika picha mwanamama huyu akiwa katika soko kuu la mjini Songea akifanya biashara ya mazao mbalimbali.

Tuesday, January 26, 2016

SIRI 8 ZA KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO NA USHINDI


ENDELEZA MAMBO CHANYA SIKU ZOTE.
Mafanikio ni safari. Tena ni safari ambayo wakati mwingine inahitaji uvumilivu mkubwa wa kutosha ili kufika mwisho. Kutokana na umuhimu wa safari hii ni lazima kwako uwe na nguvu, dira, mwelekeo pamoja na hamasa kubwa siku zote bila kuchoka. Kama utakosa hamasa hii ya kufikia mafanikio yako basi elewa hutafika mbali ni lazima utakwama.
Hivyo, ili kufanikiwa ni lazima kujifunza kila siku na kujua mbinu mbalimbali za kuhamasika na ambazo zitakufanya usonge mbele bila kusimama. Kwa kufanya hivyo utajikuta ukiishi maisha ya mafanikio na ushindi siku zote. Je, hivi unajua siri ya maisha ya ushindi ipo wapi? Bila kupoteza muda, leo nakukumbusha siri chache za kuishi maisha ya ushindi katika maisha yako.
1. Acha kujilisha na kuendeleza vitu dhaifu katika maisha yako.
Kama ni ubora endeleza ubora siku zote, acha kubeba udhaifu mwingi katika maisha yako usio na maana. Kwa mfano unaweza ukawa ni mvivu, acha kuendeleza uvivu huo. Unaweza ukawa una matumizi mabovu ya pesa acha kuendeleza tabia hiyo. Hayo ni mambo dhaifu unayotakiwa kuyaacha mara moja ili kujihakikishia mafanikio yako.
2. Kuwa makini na maisha yako.
Siku zote kuwa makini na maisha yako. Jitahidi kila siku asubuhi kuandika kile ulichojifunza kwa siku ya jana kupitia dunia, kiwe kizuri au kibaya kisha kifanyie kazi. Hakikisha siku isipite bila kujifunza kitu cha kubadili maisha yako. Hiyo haitoshi usiruhusu mtu achezee maisha yako kwa namna yoyote ile. Kuwa makini siku zote, itakusaidia kuishi maisha ya ushindi.
3. Acha kusubiri kitu, kuwa mtendaji.
Ni bora kuanza na kitu kidogo kuliko ukakaa na kuendelea kusubiri. Kama ni malengo anza kuyatekeza kidogo kidogo mpaka yatatimia. Kama ni kuandika andika kidogo mwisho wa siku utaandika kitabu kizima. Je, bado unaendelea kusubiri? Usisubiri huo si wakati wake kwa sasa.
4. Shauku na hamasa ni msingi mkubwa wa mafanikio yako.
Watu wanaofanikiwa sio kwamba wana akili nyingi sana kuzidi wengine, hapana. Kinachowafanya wafanikiwe ni kwa sababu ya SHAUKU ya kutaka kufanikiwa kwao na MAARIFA wanayowekeza kila siku. Ukijijengea shauku na hamasa kubwa hakuna kitu cha kukuzuia lazima ufanikiwe.
5. Jijengee mtazamo chanya ili kufanikiwa kwa viwango vikubwa.
Kama unafikiri huwezi kufanikisha ama kufikia kiwango fulani cha mafanikio katika maisha yako, basi hakuna njia nyingine ya kukutoa hapo, ndivyo itakavyokuwa.  Kwa sababu kila hatua utakayochukua itaendana sawa sawa na kile unachoamini katika maisha yako siku zote.
6. Kila siku tafuta kubadilika kwanza wewe.
Ikiwa unataka maisha yako yabadilike. Anza kwanza kubadilika wewe. Hiyo ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yoyote unayoyahitaji. Lakini ikiwa utakazana sana kubadili mambo ya nje na kujisahau wewe, itakuwa ni ngumu sana kwa wewe kuweza kubadilisha maisha yako zaidi utaendelea kubaki hivyo ulivyo.
7. Hakuna kukata tamaa kwenye mafanikio.
Kitu cha kutambua hapa huwezi kupata mafanikio kwa mara moja. Mafanikio yanakuja hatua kwa hatua kama tulivyosema mwanzoni. Kuna wakati tunakuwa tunashindwa sana lakini tunanyanyuka na kusonga mbele. Hivyo kwa namna yoyote ile hutakiwi kukata tamaa pale unaposhindwa.
8. Tafuta wazo moja na lifanyie kazi.
Najua unaweza ukawa unaweza mawazo mengi ambayo unataka kuyatendea kazi. Acha kuhagaika sana mara huku mara kule. Chagua wazo moja na kisha ulifanyie kazi. Ishi na wazo hilo na liwe kama sehemu ya maisha yako.
Hizo ni sehemu ya sheria ambazo unaweza ukazitumia zikakupa mafanikio makubwa katika maisha yako.
Katika pitapita zangu nimekutana na hii hapa nikaona niiweke hapa ili nisifaidike peke yangu.
PAMOJA DAIMA....KAPULYA!

Monday, January 25, 2016

SIKU MPYA NA JUMA MPYA NA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA IANZE SIKU NA JUMA HILA NA KATUNI HII.....

Nawatakieni wote mwanzo mwema wa juma na kila mlilopanga kufanya lifanikiwe. Tupo pamoja!

Friday, January 22, 2016

MWISHO WA JUMA HILI: BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA UJUMBE HUU....!!

"Katika maisha, haijalishi wapi unakwenda, ispokuwa na nani yupo nawe huko uendako"
NAWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA  NA WOTE MNAPENDWA...KAPULYA WENU!!

Thursday, January 21, 2016

SONGEA JUMANNE 19/1/2016 :- MGOMO WA WAFANYABIASHARA SONGEA WADUMU KWA SAA 5



Wafanyabiashara wa maduka wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika kufunga maduka yao kwa zaidi ya masaa matano kwa ajili ya kuzungumza na uongozi wa manispaa na mkuu wa wilaya ya Songea kuhusiana na omgezeko la tozo ya leseni kwa wafanyabiashara.

Hatua hiyo ya wafanyabiashara kufunga maduka ilifikiwa leo baada yakutokuwepo na makubaliano baina yao na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Songea ambao ulidaiwa kukiuka makubaliano ya awali ya pamoja yaliyofikiwa baina ya uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara,uongozi wa manispaa ya Songea na mkuu wa wilaya.

Makubaliano hayo yalikuwa ni kuangaliwa upya kwa viwango vya tozo za leseni vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria ya kodi iliyotungwa na bunge la jamhuri ya muungano ambayo haikuangalia uwezo wa kiuchumi uliopo kwa halmashauri za wilaya,miji na majiji nchini na kwa mzunguko wa fedha uliopo katika mji wa Songea wafanyabiashara waliomba pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo wao kutazamwa kulingsana na mzunguko wa kiuchumi uliopo.

Wakati mazungmzo hayo yakiendelea baina ya viongozi na jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa wa Ruvuma uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Songea uliamua kuendesha msako kwenye maduka kwa ajili ya ukaguzi wa leseni msako ambao ulitumia nguvu zaidi za jeshila polisi kwa kushirikianana askari mgambo kitendo ambacho kiliwafanya wafanyabiashara waamue kufunga maduka yao kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na suala hilo.

Akizungumza katika mkutano huo wa wafanyabiashara mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya pamoja na kutumia muda mwingi kuwaomba radhi wafanyabiashara kwa mkanganyiko huo uliojitokeza miongoni mwao na uongozi wa halmashauri wa Manispaa huku akiwaonyeshea kidole wataalamu wa halmashauri ya ya Manispaa kwa kutoa ushauri usio sahihi kwa viongozi wao na kusababisha mkanganyiko huo.

Amesema lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa mfumo ulio sahihi na rafiki kwa kila mmoja na siyo matumizi ya mabavu kwa wafanyabiashara na ili serikali iweze kutoa huduma muhimu kwa wananchi kunapaswa kuwepo kwa mfumo sahihi wa ukusanyaji wa mapato hayo huku akilaani matumizi ya askari wa jeshi la polisi katika ukaguzi huo wa leseni.

 Aidha amewashauri viongozi wa jumuiya ya wafayabiashara na uongozi wa manispaa ya Songea kuimarisha mahusiano chanya miongoni mwao ili kuweza kuijenga manispaa hiyo kiuchumi na pamoja na kushirikiana na mbunge wa jimbo la Songea mjini Leunidas Gama aweze kufikisha kilio hicho cha wafanyabiashara wa manispaa ya Songea cha ongezeko kubwa la tozo la leseni bungeni ili mapitio yaweze kufanyika.

Naye mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiasharawa mkoa wa Ruvuma Titus Mbilinyi aliwahakikishia viongozi wa halmashauri ya manispaa hiyo na mkuu wa wilaya kuwa kuwa wafanyabiashara hawapendi kufunga biashara zao kila wakati na wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa bali kinachogomba kwao ni mfumo wa ukusanyaji kodi na kauli za baadhiya watendaji wa mamlaka zilizopo.

Na Nathan Mtega, Songea


Wednesday, January 20, 2016

SIFA KUU AMBAZO WANAUME WENGI WANAZIPENDA KUTOKA KWA MWANAMKE

Hizi ni sifa kuu ambazo wanaume wengi wanazipenda kutoka kwa mwanamke:- 
 1. mwanamke mtii.
Kila mwanaume ana vitu vyake ambavyo hupenda mwanamke wake avifanye au aviache so mara nyingi mwanaume hufurahia utii kwa mwanamke wake (lakini tii kwa mambo ya msingi ambayo hayamchukizi MUNGU ).

2. Mwanamke msafi.
Kila mwanaume anapenda kuwa na mwanamke msafi anaejipenda yeye mwenyewe na anaependa mazingira yake na mumewe na mtoto watoto Wake.

3. Mwanamke mwenye hofu ya MUNGU.
Mwanamke mwenye hofu ya MUNGU huwa sambamba na mwanaume wake kwa kila jambo, lakini asiyekuwa na hofu na MUNGU hawezi kuwa mtii wala msikivu kwa mwanadamu mwenzie.

4. Mwanamke anaejipenda na kujua thamani ya utu wake.
Mwanamke anaejipenda nafsi yake na kutambua thamani yake hawezi kusahau thamani ya mwanaume wake maana kaishajijua yeye thamani yake na utu wake hivyo ni rahisi kutambua thamani na utu wa mwanaume wake. 

5. Mwanamke mkweli.
Mwanamke mkweli na muwazi hupendwa na jamii yote inayomzunguka.

 (6) Mwanamke mpenda maendeleo. Mwanamke mpenda maendeleo ni fahari ya mwanaume yeyote maana mwanamke anaweza kuleta mafanikio makubwa sana kwa mwanaume kupitia akili yake ya kupenda maendeleo.

 7. Mvumilivu.
Mwanamke mvumilivu ni faraja kwa mwanaume wake maana hata mwanaume akiyumba kiuchumi hatamkimbia na wala hatachepuka Bali atampa moyo na faraja ambayo itamfanya mwanaume huyo aendelee kukaza buti. 

 8. Mwaminifu kwenye mahusiano.
Kila mwanaume anapenda awe na mwanamke wa kwake yeye mwenyewe , yaani mwanaume hata awe kicheche vp anapenda kuwa na mwanamke mtulivu.

 9. Mwanamke mchapakazi.
Wanaume wengi wanapenda mwanamke mwenye adress yaani awe na sehemu ya kumuingizia hata hela ya wanja siyo aombe kila kitu.

 10. Mwanamke anaejituma kumfurahisha mwanaume wake kwenye 6×7 .
Kila mwanaume anapenda kupata kitu kizuri na cha tofauti kutoka kwa mwanamke wake so kila mwanamke anapaswa kutumia akili yake yote na nguvu zake zote kwenye huo upande,
acheni uvivu wadungu HAPO KAZI TU. nawatakia siku njema nawapenda sana. Imeandikwa na Esther Charles  kupitia ukurasa wake wa instargram.

Tuesday, January 19, 2016

"MJADALA ULIOVUNJA REKODI KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO MWAKA 2015"

Ndugu wasomaji wa blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO, katika kupitia mada mbalimbali nilizowahi kuweka humu ili kupata ile ambayo ilivuta hisia za wasomaji wengi na kuleta changamoto, nimevutiwa na mada hii ambayo ilileta vuta nikuvute miongoni mwa wadau wa blog hii.
Kwa hiyo basi nimeichagua mada hii kuwa ndio mada iliyovunja rekodi kwa mwaka 2015.
Natoa shukrani kwa wadau wote mlioshiriki katika kuichangia mada hii.
Naomba muungane nami katika kujikumbusha kile kilichotokea katika mjadala huu.


NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MWISHO WA JUMA UWE MWEMA..
Hili ni vazi langu la leo au mwenekano wangu wa leo na napenda kuwatakia wote JUMAMOSI NJEMA AU MWISHO WA JUMA MWEMA. KAPULYA.
Manka said...
Dada yangu habari za siku nyingi?umependeza sana na vazi lako.Bustani yako inaendeleaje?
Anonymous said...
Fantastiki! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...
Kaka Mhango....ahsante sana.
Manka ndugu wa mimi ni kweli siku nyingi ni njema....ahsante. Bustani mwaka huu si nzuri sana hali ya hewa inazingua.
Kaka ahsante.

Nicky Mwangoka said...
Umependeza sana Dada kama weekend yenyewe ilivyokuwa nzuri
Penina Simon said...
Thanks , umetokelezea bomba

Yasinta Ngonyani said...
Kaka Nicky, Dada P! Ahsanteni sana kwa kutochoka kupita hapa na kuacha yenu ya moyoni.

ray njau said...
Hapa ni kisima kama siyo kufua na maji ya kunywa je?

Yasinta Ngonyani said...
Kaka Ray Ahsante!

Ester Ulaya said...
dada yangu mwenyewe umenogaaa

Yasinta Ngonyani said...
Mama Alvin! Ahsante sana









Monday, January 18, 2016

NI SIKU NA WIKI MPYA NA TUANZE NA MLO HUU...CHAGUO LAKO TU HAPA....

 Mahindi ya kupikwa/kuchemshwa na uji au....
.....ya kuchoma. Binafsi hupenfda sana mahindi ya kupika/kuchemshwa hasa yakiwa yamechemshwa na maboga. Haya tufurahie mlo huu pamoja....Kapulya wenu

Sunday, January 17, 2016

NI JUMAPILI YA TATU TANGU MWAKA HUU 2016 UANZE:- NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA!!

Jumapili iwe njemasana kwa wote kwa ujumbe huu....:- MUNGU UFANYA  NJIA PASIPOKUWA NA NJIA....

Friday, January 15, 2016

Wednesday, January 13, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA


SERIKALI inakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV (Intravenous Fluids) katika hospitali zake zote kubwa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mtambo wa kutengenezea drip hizo za majimaji katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, Mkoani Ruvuma.

Amesema haoni kwa nini hospitali hizo ziendelee kuagiza wakati uwezo na watalamu wa kufanya hivyo upo hapa hapa nchini.

Drip hizo zina manufaa makubwa kwa wagonjwa ikiwemo kuongeza maji kwa wagonjwa waliopungukiwa na maji mwilini na vilevile inatumika kwa ajili ya kutolea baadhi ya dawa ambapo huchanganywa.
Vilevile hutumika wakati wa huduma za upasuaji.

Monday, January 11, 2016

KWA VILE TAYARI TUPO MKOANI RUVUMA BASI TUBAKI NA KUANGALIA BAADHI YA PICHA ZA PERAMIHO ILIVYOKUWA HAPO ZAMANI/KALE

VIBANDA VYA HOSPITAL YA PERAMIHO MWAKA 1930

 HAPA NI KAMA VILE SHULE YA MSINGI SIKU HIZI. iNASEMEKENA WALIKUWA WAKIFUNDISHWA KWA KIINGEREZA TU....(FORMER MIDDLE SCHOOL)
WANAFUNZI WA  WAKATI HUO WALIONEKANA HIVI KATIKA SHULE YA MSINGI HAPA WAPO NA MWALIMU WAO HUYO MWENYE NGUO NYEUPE.
NA HAPA PICHA YA MWISHO NI MASKANI YA NDUNA SONGEA MBANO...

Saturday, January 9, 2016

UJENZI HAPA MBINGA UNAENDELEA NA SI MUDA MREFU TUTAWEZA KUHAMIA...

Ukipita Mbinga basi  huna haja ya kulala hotel KARIBU SANA KWETU maana sisi  ni ndugu  na ndugu husaidiana


Friday, January 8, 2016

IRENTE VIEW POINT LUSHOTO TANGA- NI MOJA YA KIVUTIO AMBACHO WATU WENGI TULIKUWA HATUJALITAMMBUA...KARIBU


TANZANIA NI NCHI YENYE VIVUTIO VINGI SANA NA VIZURI KAMA TULIVYOONA ..NAWEZA NIKASEMA NAJIVUNIA NCHI YANGU....

Thursday, January 7, 2016

USEMI WA LEO KUTOKA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO....!

Elimu sio maandalizi ya maisha- Isipokuwa ELIMU ndiyo  MAISHA.
TUPO PAMOJA!

Tuesday, January 5, 2016

LEO NI TAREHE ALIYOZALIWA KAPULYA .. :-) AMETIMIZA MIAKA KADHAAA

Aama kweli miaka inakwenda ...kuna wakati natamani kuwa mdogo tena ....Hapa ni Njombe 2014/15
HAPA NI MSOSI TU...KARIBUNI

Leo ni tarehe/siku kama ile  familia ya Mzee Ngonyani ilikuwa na furaha kumpata binti yao ambaye alizaliwa kama tarehe hii ya leo 5/1. Na leo ameongeza mwaka tena na kuzidi kuzeeka:-). Lakini hata hivyo anapenda kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki kwa siku hii ili tumsaidie kusherekea. Na wote manakaribishwa..sana. NAWATAKIENI SIKU NA WAKATI MWEMA. WOTE MNAPENDWA SANA ...Pia salamu na HONGERA nyingi kwa wale wote wanaotimiza miaka mwezi huu wa kwanza/Januari pia.   Nachukua nafasi hii  kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama  na namwomba azidi kunilinda/kutulinda salama. 
Naona tumalizia na mwimba huu ni kwa Neema na Rehema...na Edson Mwasabwite...

Sunday, January 3, 2016

NI JUMAPILI YA KWANZA YA MWAKA HUU MPYA WA 2016...TUNAENDELEA KUUSHEHEREKE KWA KUTOSAHAU KULA MBOGA...

Hii ni mboga ya kwetu Lundusi /Peramiho.  Karibuni. TUKUMBUKE MBOGA NI MUHIMU KATIKA MIILI YETU...

Saturday, January 2, 2016

MWAKA MPYA!

Nimekumbuka leo nilipokuwa  mtoto nilikuwa nikipata taabu sana kuhusu mwaka mpya ufikapo. 

Katija akili yangu nilifikiri  MWAKA MPYA  ni kila kitu hubadilika na kuwa kipya hususan rangi ya Mbingu. Kumbe hapana, nilipoendelea kupata akili mambo hayakubadilika. Hapo sasa udadisi ukazidi nikawa namuuliza kila mtu aliye nizidi umri  MWAKA MPYA  ina maana gani? 

Nikawa napata majibu tofauti tofauti:- kama vile...

1. Mwaka  ni jumla ya miezi  kumi na mbili.

2. Mwaka ni siku  nyingi. 

3. Mwaka ni siku inayoadhimishwa baada ya kibunzi. 

Na kibunzi  ikiwa na maana siku  kuaga mwaka,  mkesha wa kuaga mwaka mwisho  wa mwaka au pia ni aina ya ubao unaotiwa mchanga utumiwao na waganga wa asili kupigia ramli.

Mh!...nikawa najiuliza kwanini isiitwe tu NAMBA MPYA maana ni namba tu 2016?

Upya wake  ni nini kwa wale walioishi miaka 80, 50 au 30?  Na je kwa nini tunapotimiza miaka isiitwe KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KUZALIWA? Badala yake tunasema BIRTHDAY.

Bado natafakari.