Wednesday, January 13, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA


SERIKALI inakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV (Intravenous Fluids) katika hospitali zake zote kubwa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mtambo wa kutengenezea drip hizo za majimaji katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, Mkoani Ruvuma.

Amesema haoni kwa nini hospitali hizo ziendelee kuagiza wakati uwezo na watalamu wa kufanya hivyo upo hapa hapa nchini.

Drip hizo zina manufaa makubwa kwa wagonjwa ikiwemo kuongeza maji kwa wagonjwa waliopungukiwa na maji mwilini na vilevile inatumika kwa ajili ya kutolea baadhi ya dawa ambapo huchanganywa.
Vilevile hutumika wakati wa huduma za upasuaji.

No comments:

Post a Comment