Saturday, January 2, 2016

MWAKA MPYA!

Nimekumbuka leo nilipokuwa  mtoto nilikuwa nikipata taabu sana kuhusu mwaka mpya ufikapo. 

Katija akili yangu nilifikiri  MWAKA MPYA  ni kila kitu hubadilika na kuwa kipya hususan rangi ya Mbingu. Kumbe hapana, nilipoendelea kupata akili mambo hayakubadilika. Hapo sasa udadisi ukazidi nikawa namuuliza kila mtu aliye nizidi umri  MWAKA MPYA  ina maana gani? 

Nikawa napata majibu tofauti tofauti:- kama vile...

1. Mwaka  ni jumla ya miezi  kumi na mbili.

2. Mwaka ni siku  nyingi. 

3. Mwaka ni siku inayoadhimishwa baada ya kibunzi. 

Na kibunzi  ikiwa na maana siku  kuaga mwaka,  mkesha wa kuaga mwaka mwisho  wa mwaka au pia ni aina ya ubao unaotiwa mchanga utumiwao na waganga wa asili kupigia ramli.

Mh!...nikawa najiuliza kwanini isiitwe tu NAMBA MPYA maana ni namba tu 2016?

Upya wake  ni nini kwa wale walioishi miaka 80, 50 au 30?  Na je kwa nini tunapotimiza miaka isiitwe KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KUZALIWA? Badala yake tunasema BIRTHDAY.

Bado natafakari.

No comments:

Post a Comment