Thursday, April 30, 2015

TUUMALIZE HUU MWEZI WA NNE NA KIPANDE HIKI CHA MZIKI WA DUNIA NI MSONGAMANO- NDALA KASHEBA


Napenda kuchukua fursa hii na kumshukuru Mungu mwezi umeisha vizuri bila misukosuko mingi sana. Natumaini na ninyi ndugu zangu  ilikuwa hivyo. Natumaini tutauanza mwezi wa tano vema.
UJUMBE:- HONGERA KWA WALE WOTETIMIZA MIAKA MWEZI HUU NA PIA POLE SANA KWA WALE WOTE WALIONDOKEWA NA WATU WAO/WETU WA KARIBU. Kapulya wenu.

Wednesday, April 29, 2015

ZILIPENDWA:- MWANAUME HUMWOMBA MWANAMKE KUCHEZA NAYE!

Ni vijana wa enzi hizo walipokuwa wakisakata. Unaona raha ya mziki ilivyo, mwanamke mpaka kavua viatu na kuweka kando. Ama kweli ...Haya tuungane nao basi:-) Kapulya

Tuesday, April 28, 2015

VAZI LA LEO...KAPULYA HUYOOO!!

Hili ndilo vazi langu la leo ...mwanamtindo Kapulya huyo:-)

Monday, April 27, 2015

JUMATATU HII TUANZA NA KUMPONGEZA MWANAMKE WA SHOKA DADA MIJA KWA KUTIMIZA MIAKA

Rafiki, dada mkuu msaidizi...napenda kukutakia kheri kwa siku yako ya kuzaliwa. Uwe na siku njema sana na hiyo miaka uliyotimizahahahahahahhaa

Saturday, April 25, 2015

KARIBU:- KUNA USHIBE!!

Naanza bila mpango, Kwa tenzi pia na tungo,
Niyafumbue mafumbo, Ugali na mbogamboga.
Wanadharau mapishi, Wanayabeza mapishi,
Mapishi ya Waswahili, Ugali na mbogamboga.
Umeyasifu matango, Mazuri sana kwa macho,
Huleta ngozi nyororo, Ugali na mbogamboga.
Na uyoga asilia, Kushiba bila ya kula,
Nashiba na kutazama, Ugali na mbogamboga.
Ugali huo wa sembe, Sembe nyeupe pepepe,
Na dona usiutupe,Ugali na mbogamboga.
CHANZO : KWA MJENGWABLOG

Friday, April 24, 2015

IUJUMAA YA LEO TUWATEMBELE NDUGU ZETU HUKO BOTSWANA.......


Mwenzenu imetokea kupenda sana hii miziki ya asili hata kama sielewi nini wanasema nikifungua tu basi kaaazi kwelikweli...Haya ijumaa pia mwisho wa juma iwe salama kwa wote...Kapulya

Thursday, April 23, 2015

DUH KAAAZI KWELIKWELI HAPA SIJUI MWALIMU ATAJIBU NINI???

Nimeipenda hii  angalia mwal. jinsi jasho linavyomtoka kwa kutafuta jibu. Watoto huwa wakweli sana na hawaoni aibu kuuliza swali....KILA LA KHERI.

Wednesday, April 22, 2015

UJUMBE!

KAZI YA MOYO NI KUSUKUMA DAMU, KUPENDA NI KIHEREHERE CHAKO!  HIVI NI KWELI JAMANI??...Kapulya wenu.

Tuesday, April 21, 2015

SWALI LA LEO:- UNAJUA NI KABILA GANI HUTUMIA MBINU/UBUNIFU HUU NCHINI TANZANIA?

Hakika watu ni wabunifu ...ila binafsi ningependa kuwabeba mgongoni..au wewe mwenzangu unasemaje?

Monday, April 20, 2015

ASILI HAICHAGUI


Mwili wa mwanadam umeumbwa mfano wa kompyuta, kompyuta unapoinunua kuna programu ambazo unazikuta humo humo kwenye kompyuta na kuna programe zingine wewe mwenyewe unaweka, kompyuta yako itafanya kazi kutokana na idadi ya programe utakazoweka, ukiweka programu zenye faida kompyuta yako itakuwa yenye faida, ukiweka programu zisizokuwa na faisa ndio hivyo kompyuta yako itakuwa haina faida, lakini pia utendaji kazi wa kompyuta moja na kompyuta nyingine vinatofautiana kulingana na idadi ya programu zilizomo kwa mfano kompyuta ambayo ina micro soft word, ina adobe,power point, itaweza kuandika barua, kuedit picha, na kuandaa presentation.
Lakini kopyuta ambayo itakuwa na pungufu ya hizo program haitaweza kufanya kazi sawa na yenye hizo program, ndivyo na maisha ya yalivyo, unapozaliwa kuna program unazaliwa nayo (KIPAJI), na kila mtu anakipaji chake,lakini unapokuja huku duniani sasa program zingine unaweka mwenyewe.
Hapa ndipo utofauti wa maisha ya mtu mmoja na mtu mwingine unaanza kuonekana, ASILI HAICHAGUI hii inamaana kwamba chochote utakoweka kwenye akili yako lazima kitaonyesha maisha yako halisi, ukiweka mambo mabaya tu kwenye akili yako hayo ndio yatatokea kwenye maisha yako maana hiyo ndio program umeweka kwenye kompyuta yako, ukiweka uoga, uvivu, kushindwa wewe kila kitu huwezi, ndio hivyo utakuwa.
Watu wengi sana tunahangaika kuwa maisha magumu, maisha magumu lakini kiuhalisia sio kweli kuwa maisha ni magumu bali tunatumikia program tulizoweka kwenye kompyuta zetu, mfano kazi yako wewe ni kuangalia muvi masaa 12, kupiga story masaa mengi, kuchat facebook na watsap asubuhi hadi jioni, magazeti ya udaku,unafikiri ubongo wako utakuwa na uwezo gani,na utazalisha nini?
Uwezo wako utakuwa finyu kwasababu kwa asilimia kubwa unapokea mambo yasiyo na maana, lakini hebu angalia uwe unasoma vitabu, unahudhuria semina, unaangalia video za watu waliofanikiwa kiuhalisia hata kama ulikuwa hujawaza kufanikiwa utaona unaanza kupata mbinu za kufanikiwa,kwanini umeweka program ambayo sasa inaleta matunda.
Tatizo kubwa kwenye akili zetu kwa asilimia kubwa tumeweka program za kushindwa, uvivu, kutaka mafanikio ya haraka, uoga, kupoteza muda, na kufanya mambo yasio na maana matokeo yake ndio maisha tulio nayo.Nakumbuka wakati nimeamua kuanza kufanya biashara na Neptunus nilikuwa sijui chochote kuhusu biashara,kwasababu nilikuwa muajiriwa tu, nilikuwa sijui chochote kuhusu kusoma vitabu na nilikuwa nikisoma ukurasa mmoja tu nalala, lakini nilichogundua kuwa ASILI HAICHAGUI chochote nitakachoweka ndani yangu kitatumika, nikaanza kujifunza alhamdulillah nilipo sasa sipo nilipokuwa mwaka mmoja uliopita.kumbe vyoyote unavyotaka kuwa kwenye haya maisha unaweza kuwa kama ukiamua kubadilisha program ulizoweka au ulizowekewa kuwa wewe huwezi,
 
CHANZO :- IMETOLEWA NA BASSANGA MWALIMU WA UJASIRIAMALI.
 

Friday, April 17, 2015

UJUMBE WA WIKI HII KUTOKA KWA KAPULYA

Huu ujumbe nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio:-
CHOCHOTE UTAKACHOWEKA KWENYE AKILI YAKO KITATOKEA, UKIWEKA KUCHINDWA UTASHINDWA, UKIWEKA UOGA NDIO UTAKAOTOKEA CHAGUA UNACHOWEKA KWENYE AKILI YAKO. IJUMAA IWE NJEMA KWA WOTE MPITAO HAPA......Kapulya.

Thursday, April 16, 2015

MWANAMKE KANGA....NIMEPENDA MTINDO HUU WA KUFUNGA KANGA!!

Kanga zina matumizi mengi sana. Ni utamaduni mzuri sana ..ila naona kama unaanza kupotea. Nikisema hivi nina maana wanawake wengi wameanza kuacha kutumia kanga na kuiga mavazi mengine kabisa inasikitisha kwa kweli maana kiazazi kijacho hakitajua utamaduni huu. Tafadhali wanawake wenzangu tudumishe utamaduni huu. Kapulya.

Wednesday, April 15, 2015

DALILI ZA MFUJWAJI MAENEO YA KAZI

 ANAWEZA KUWA ANALIA KWA SIRI OFISINI

Tunaishi kwenye dunia ambapo ajira imekuwa ni eneo kubwa ambapo watu mbalimbali hukutana na kujenga ukaribu. Kuna wakati, wanawake wenzetu  sehemu za ajira wanaweza kuwa kwenye mateso yatokanayo na kufunjwa kwenye uhusiano wao, Kama tukijua  dalili za mwanamke ambaye yupo kwenye uhusiano wa kufujwa, inaweza kuwa rahisi kwetu kumsaidia.

Kuna dalili ambazo, kama tutaziona kwa watumishi wenzetu wa kike, tunaweza kuanza kutafuta namna ya kuwazoea na hatimaye kujaribu kuona kama wako kwenye ufujaji ili kuwasaidia, hata kwa mawazo tu.
Kama tukiona mtumishi mwenzetu ana michubuko au uvimbe ambao anasingizia kwamba, alianguka au amepata ajali fulani ni vema kuanza kujiuliza kama hafujwi kwenye uhusiano wake. Inawezekana ikiwa ni kweli, amepata ajali ya aina fulani, lakini uwezekanao kwamba, amepigwa ni mkubwa pia. hasa kama matukio haya ya "ajali" hutokea mara kwa mara.
Kama mwenzetu kazini anaonyesha dalili za kusongeka sana, yaani huzuni na mawazo muda wote, ni dalili  kuwa huenda anafujwa. Lakini kuna wakati anaweza kuwa anakilia kwa siri ofisini, hasa kwa kujifungia chooni au popote. Tunaweza kugundua kulia kwa kukagua macho.

Dalili nyingine zinazoweza kutuonyesha kwamba, mwenzetu anafujwa ni kuchelewachelewa kazini. Kama mwanamke anachelewa mara nyingi kufika kazini, wakati mazingira hayaonyeshi kwamba, analazika kuchelewa, huenda anafujwa.

Kama mwenzetu anapokea na kujibu simu za mtu ambaye anaonekana ama anamtisha au kumsumbua kwa njia moja au nyingine, ni dalili  nyingine. Simu ambazo zinaonyesha kumkera mwenzetu kila akisikiliza, siyo dalili nzuri. Wapenzi wafujaji hupenda sana kutumia simu kushutumu au kutumia simu kuhakikisha kwamba, mpenzi yupo kazini kweli.

Kama mwenzetu anajitenga sana au hata utendaji wake unazidi kushuka, inaweza kuwa ni dalili ya kuwa anafujwa na mume wake au mpenzi

Kwa kuhisi kwamba, mwenzetu huenda anafujwa, tubaweza kumsaidia kwa kuzungumza naye au kumtuma mtu ambaye anamwamini azungumze naye ili kujua tatizo. Kumbuka kwamba wakati mwingine anayefunjwa anahitaji msaada ili aweze kutoka.
CHANZO:- KITABU CHA ...MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA NA Munga Tahenan.

Tuesday, April 14, 2015

VYAKULA TUNAVYOPASWA KULA ILI TUWE NA AFYA BORA!!

Tusipuuzie vyakula vya aina hii ili kulinda afya zetu... Mie hapo nimeutamani hasa  muwa huo:-) Tuzingatie ndugu zanguni. Basi mie niwatakieni siku njma sana.  NENO LA LEO:- Usiache kufanya kitu kwa sababu umechoka, acha kwa sababu umekimaliza,

Sunday, April 12, 2015

HII NI KAZI YA MIKONO YANGU...NAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA NA MIKONO!!!!

 Nimeamka asubuhi hii na kujisikia hamu ya kuoka mikate na hapa mbaona matokeo yake
Napenda kuoka tu lakini sio kula usiniulize kwa nini kwa vile unajua jibu:-)  Nimezoea kula mihogo ya kuchemsha:-)

Friday, April 10, 2015

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA WIKI HII!!

Nimeipenda hii picha taswira yake na  kila kitu ...halafu natamani haya magimbi na mahindi:-) IJUMAA NJEMA KWA WOTE .......NAONA HATA WEWE UNATAMANI:-)

Thursday, April 9, 2015

WANAUME NA SIFA

Mwanaume siku zote anauawa na sifa, anauawa na kutaka kwake mwanamke  amuone kwamba yenye ndiye mwanaume bora kabisa na asiyeshindwa na jambo. Kwa hali hiyo, adui yake namba moja ni kukosolewa. Siyo kwamba mwanamke anapokosolewa hafurahi, hapana, lakini haimpi shida na haichukulii kama jambo kubwa kama inavyotokea kwa mwanamume. Mwanamke anapokosoa mwanamume anakuwa hajui kwamba mwenzake siyo kama yeye, kwamba kwa mwenzake kukossolewa ni kama kudungwa sindano ya sumu- anauawa kisaikolojia.
Ukweli ni kwamba,  ukienda kwenye ndoa ambazo  mume hukosolewa sana, tatizo la mume kama huyo kukosa nguvu za kushiriki tendo la ndoa ni la kawaida. Mwanamume anapokosolewa na mkewe huumia sana. Kuumia huku ambako hutokea kwenye mawazo ya kawaida na yale ya kina, humfanya mwanamume kuona kama vile amenyangánywa uanaume wake. Ndiyo maana  maumivu haya huendelea kuwepo hadi kitandani kwa sabababu mwanamumu huyu hufikia kuamini kwamba haba uanaume.
Kwa mwanamke, kwa sababu amekuwa akikosolewa tangu miaka miliono iliyopita na kutupiwa lawama hata pale ambapo kosa ni la mwanamume, kukosolewa na kukosoa kwa upande wake siyo jambo lenya kuweza kumpa mtu jazba. Lakini hivi sivyo ilivyo kwa mwanamume. Kwa bahati mbaya mwanamke hajui, anadhani anatarajia mwanamume kuwa kama yeye. Anapokosoa anadhani na kuamini kwamba atambadili mwanamume, wakati anaielekeza ndoa yake shimoni.
CHANZO:  Maisha na mafanikio na  MUNGA TEHENAN.

Monday, April 6, 2015

TUANZE WIKI HII YA PASAKA NA PICHA HII AMA KWELI....

Sijawahi kuona jogoo wakicheza mpira wala kusikia. Kaaaazi kwelikweliii  JUMATATU YA PASAKA IWE NJEMA KWA WOTE! KAPULYA

Sunday, April 5, 2015

NAPENDA KUWATAKIENI PASAKA NJEMA NA YENYE AMANI NA BARAKA TELE....!!!!

Ni PASAKA LEO..Je unajua pasaka ni nini? angalia hapa chini:-
P-Pokea
A-Amani
S- Sasa
A- Ambayo
K- Kristo
A- Ametupa-
Mungu awatangulie katika PASAKA HII. AMANI IWE NANYI. AMINA- PASAKA NJEMA KWA WOTE.

Friday, April 3, 2015

Thursday, April 2, 2015

NA TUANZE MWEZI HUU WA NNE KIHIVI:- KAPULYA AMEANZA KUTAMANI KUANZA KULIMA BUSTANI

Jinsi siku zinavyosogea kwa msimu wa bustani mikono yangu inazidi  kuwasha sana, na hivi nisemavyo nimekwisha anza atika  baadhi ya mbegu ..:-) Nasubiri kwa hamu sanaaaaa. ALHAMIS KUU IWE NJEMA KWA WOTE