ANAWEZA KUWA ANALIA KWA SIRI OFISINI
Tunaishi kwenye dunia ambapo ajira imekuwa ni eneo kubwa ambapo watu mbalimbali hukutana na kujenga ukaribu. Kuna wakati, wanawake wenzetu sehemu za ajira wanaweza kuwa kwenye mateso yatokanayo na kufunjwa kwenye uhusiano wao, Kama tukijua dalili za mwanamke ambaye yupo kwenye uhusiano wa kufujwa, inaweza kuwa rahisi kwetu kumsaidia.
Kuna dalili ambazo, kama tutaziona kwa watumishi wenzetu wa kike, tunaweza kuanza kutafuta namna ya kuwazoea na hatimaye kujaribu kuona kama wako kwenye ufujaji ili kuwasaidia, hata kwa mawazo tu.
Kama tukiona mtumishi mwenzetu ana michubuko au uvimbe ambao anasingizia kwamba, alianguka au amepata ajali fulani ni vema kuanza kujiuliza kama hafujwi kwenye uhusiano wake. Inawezekana ikiwa ni kweli, amepata ajali ya aina fulani, lakini uwezekanao kwamba, amepigwa ni mkubwa pia. hasa kama matukio haya ya "ajali" hutokea mara kwa mara.
Kama mwenzetu kazini anaonyesha dalili za kusongeka sana, yaani huzuni na mawazo muda wote, ni dalili kuwa huenda anafujwa. Lakini kuna wakati anaweza kuwa anakilia kwa siri ofisini, hasa kwa kujifungia chooni au popote. Tunaweza kugundua kulia kwa kukagua macho.
Dalili nyingine zinazoweza kutuonyesha kwamba, mwenzetu anafujwa ni kuchelewachelewa kazini. Kama mwanamke anachelewa mara nyingi kufika kazini, wakati mazingira hayaonyeshi kwamba, analazika kuchelewa, huenda anafujwa.
Kama mwenzetu anapokea na kujibu simu za mtu ambaye anaonekana ama anamtisha au kumsumbua kwa njia moja au nyingine, ni dalili nyingine. Simu ambazo zinaonyesha kumkera mwenzetu kila akisikiliza, siyo dalili nzuri. Wapenzi wafujaji hupenda sana kutumia simu kushutumu au kutumia simu kuhakikisha kwamba, mpenzi yupo kazini kweli.
Kama mwenzetu anajitenga sana au hata utendaji wake unazidi kushuka, inaweza kuwa ni dalili ya kuwa anafujwa na mume wake au mpenzi
Kwa kuhisi kwamba, mwenzetu huenda anafujwa, tubaweza kumsaidia kwa kuzungumza naye au kumtuma mtu ambaye anamwamini azungumze naye ili kujua tatizo. Kumbuka kwamba wakati mwingine anayefunjwa anahitaji msaada ili aweze kutoka.
CHANZO:- KITABU CHA ...MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA NA Munga Tahenan.
'Kufujwa' ...nilijua ni kama kuharibiwa au kama vile unasema `unafuja mali ya umma...tunashukuru kwa maelezo hayo Tupo pamoja
ReplyDeleteSioni utafiti wala ushahidi wowote zaidi ya hisia ambazo nyingi si za kweli.
ReplyDelete