Monday, December 31, 2018

UJUMBE WA MWISHO WA MWAKA 2018 KUTOKA KWANGU KUJA KWENU

UJUMBE :-
HATA SURA NZURI ITAZEEKA, NA MWILI MZURI UTACHOKA, ILA ROHO NZURI HUBAKI  KUWA NZURI MILELE NA MILELE.
NACHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURUNI SANA KWA MWAKA HUU 2018 KWA USHIRIKIANO WENU. AHSANTE SANA SANA . NI MIMI KAPULYA WENU.

Wednesday, December 26, 2018

MWOKOZI YESU AMEZALIWA


NI MATEGEMEO YANGU KUWA SIKUKUU HII YA KUZALIWA MWOKOZI WETU IMEKUWA NJEMA KWA WENGI WETU. NAMI NACHUKUA NAFASI HII NA KUSEMA NAWATAKIENI  WOTE NOELI NJEMA

Monday, December 17, 2018

LEO NIMEKUMBUKA MITINDO YA ZAMANI JINSI WATU WALIVYOKUWA WAKIPEANA HISIA ZAO

Hapa itakuwa anaenda kisimani ndoo kaficha sehemu, hivi unafikiri kwa nini hawaangaliani?
Hapa yaonekana mdada anaenda kutafuta kuni

...na mtindo huu ni kiboko wote wanaonekana kuwa na aibu ...


....hii ni  baadhi ya mitindo ya hapo kale.  Au pia watu walikuwa wakiandika barua au kumtuma mtu. Siku hizi eti mtu anatuma sms ya kawaida au WhatsApp

Thursday, December 13, 2018

TAREHE HII HAPA LEO NI SIKUKU YA MTAKATIFU LUCIA...

Kwa hiyo mimi nimeona itapendeza zaidi kama nikiitumia mikono yangu kwa kutengeneza aina hii maalumu ya mikate(LUSSEKATTER)  ili kujumuika ndugu, marafiki pia majirani kwa kusherehea siku hii....


.....pia aina hii ya biskuti (pepparkaka) GINGERBREAD


Na hapa ni maagizo  jinsi inavyokuwa. Nakumbuka binti yetu aliwahi kuigiza duh! niliogopa sana maana hiyo mishumaa inawaka kwa ukweli ......ila walijiandaa na ndoo za maji...

Monday, December 10, 2018

HAPO KALE KARIAKOO YETU ILIVYOKUWA........

NAWATAKIENI WOTE JUMATATU NJEMA SANA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!

Wednesday, December 5, 2018

NIMEYATAMANI SANA HAYA MATUNDA...............


Hapa ni mbula au sisi wangoni twasema  mabuni ni matamu sana pia juisi yake ni tamu mno.
Na hapa ni masuku, sasa ndio msimu wake 

Tuesday, December 4, 2018

NI MWEZI MPYA TENA ...TUANZE NA MSEMO HUU KUUANZA MWEZI HUU WA KUMI NA MBILI!

Msemo/ujumbe wa leo:-
Njia bora ya kuacha kuwaza ni jinsi gani unafikiri ya kwamba unajifahamu/jijua ni kuzingatia kile unachokijua, unajua.
TUKUTANE TENA PANAPO MAJALIWA!

Wednesday, November 28, 2018

BADO TUPO SONGEA KWETU

Karika pilika za kununua ngua Songea mjini

Tuesday, November 27, 2018

NAIPENDA SONGEA YANGU PIA CHAI HASA BILA SUKARI!

Kikombe hiki nimekipenda sana  hasa kwa kunywea chai na zaidi haya maneno ya naipenda SONGEA

Thursday, November 22, 2018

USIACHE KWENDA KANISANI

 


Mshiriki wa Kanisa, ambaye hapo nyuma amekuwa akihudhuria ibada kila juma,
 aliacha kwenda Kanisani. 
Baada ya wiki kadhaa kupita, Mchungaji aliamua kumtembelea nyumbani kwake.
Ilikuwa jioni ya baridi. Mchungaji alimkuta ndugu yule nyumbani peke yake akiwa
amekaa mbele ya jiko akiota moto
dhidi ya baridi. Akiwa anajaribu kutambua sababu ya  Mchungaji kumtembelea,
alimkaribisha na kumpatia kiti ili 
waote moto pamoja na kusubiri kitakachoendelea.
Mchungaji aliketi, lakini hakusema chochote, alikuwa kimya. Katikati ya ukimya ule,
aliutazama ule moto na mkaa 
uliokuwa ukiwaka jikoni. 
Baada ya dakika kadhaa, Mchungaji akachukua kibanio cha mkaa,
kwa makini akachukua kaa moja lililokuwa 
linawaka zaidi na akaliweka chini peke yake na kisha akakaa tena kwenye kiti chake kimyakimya.

Mwenyeji alitizama chote kilichokuwa kikiendelea akijaribu kujifunza kimyakimya.
Kadri lile kaa lililowekwa pembeni 
lilivyokuwa likiishiwa muwako wake, taratibu majivu yakaanza kulishika na hatimaye likazimika kabisa. 
Likawa baridi likazima kabisa.

Hakuna hata neno lililozungumzwa tangu waliposalimiana.
Mchungaji aliutazama ule mkaa ulozimika 
na akaona kwamba huu ni wakati sasa wa kuondoka.
Alisimama taratibu akauokota ule mkaa ulozimika na
 kuurudisha katikati ya makaa mengine yaliyokuwa yakiwaka moto.
Papohapo likashika moto likaanza kuwaka 
kama makaa mengine.
Mchungaji akaanza kuondoka. Alipofika mlangoni,
mwenyeji akiwa anabubujikwa na machozi shavuni, 
akasema "Mchungaji,
 ahsante sana kwa kunitembelea na hasa kwa hubiri lako hili la mkaa. 
Nimelielewa somo na kuanzia juma lijalo, nitaanza tena kuja kanisani"
**MWISHO WA SIMULIZI*

Nini tunajifunza hapa? Katika siku hizi za mwisho,
mwovu atatumia kila mbinu kuwafanya wanadamu 
wasihudhurie makanisani kwa kuwapatia sababu mbalimbali.
Lakini ushauri wangu, usiache kwenda kwenye ibada
kwa kisingizio kisicho na mashiko.
Kuwa Kanisani na kujichanganya na waamini wenzako kuna faida kubwa na 
kunatia joto la kiroho. Ukijitenga na washiriki wenzako,
utazimika kiroho na hatimaye utakufa kabisa kiroho.

Usiache kwenda kanisani kisa eti kule hawakujali,
usiache kwenda kanisani kisa eti Mchungaji/Askofu anapenda 
sadaka sana, usiache kwenda kanisani kisa huna sadaka,
usiache kwenda kanisani kisa uko katika hisia, 
usiache kwenda kanisani kisa unahofia kurudia nguo uliyovaa juma lililopita,
 usiache kwenda kanisani kisa 
unahofia kuna mtu mmekwazana kule,
usiache kwenda kanisani kisa hujisikii, usiache kwenda kanisani kisa 
wamekuudhi.
Ukiacha kwenda kanisani utazimika kama lile kaa moja,
ni kanisani ndiko MUNGU huachilia baraka ya kutufanya 
tuwe moto mkali, tunapojitenga na kanisa,
baridi ya dunia hii itatupiga na hatimaye tutazimika kabisa. 
Tafadhali usiache kwenda kanisani na Mungu akujalie upate hamasa mpya.

_*Nimeikuta simulizi hii mahali:
Pengine yaweza kutusaidia tuhudhurie ibada ikibidi mpaka katikati ya wiki.*_

Monday, November 19, 2018

PALE UNAPOOTA NDOTO YA KUWA NA SEHEMU KAMA HII

umekaa hapa na kuangalia uumbaji wa Mungu 
Hapa ni sehemu ya kupumzikia/kula
Jiko la kuchomea piza

Sunday, November 18, 2018

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JIONI HII YA JUMAPILI YA LEO IWE TULIVU NA YENYE AMANI

Nawatakieni jioni hii ya jumapili ya leo iwe tulivu, yenye furaha na amani ya kutosha. KILA LA KHERI!...Kapulya wenu.

Monday, November 12, 2018

HII NI KAZI YA MIKONO YA KAKANGU HUKO MBINGA...MTOTO UMLEAVYO NDIYO AKUAVYOO

 Ukijishughulisha hakika njaa hutaiona......
Tujifunze kujishughulisha na hapo tutaona mafanikio yake

Tuesday, November 6, 2018

MBOGA ZA ASILI ZINA MANUFAA/FAIDA NA UTAMU WAKE

UYOGA PORI
Ni chakula nikipendacho sana na ni hodari sana kuutafuta huko mstuni. Maana ukiwa huko mstuni inakuwa kama ni kupoteza mawazo na pia unapata mazoezi na kIkubwa zaidi unapata mboga tena ya bureee. 
Mlenda bamia na mboga majani ya maboga au  mlenda wa porini na karanga. Binafsi nitachagua bamia na mboga maboga au mlenda pori usiotiwa karanga.

Wednesday, October 31, 2018

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA HII PICHA IWE YA MWISHO WA MWEZI....USALAMA BARABARANI...

Tuwe waangalifu tuwapo barabarani hii ni hatari sana kwa mwendesha pikipiki na mteja pia wapita njia.
NACHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURUNI KWA USHIRIKIANO WENU MZURI DAIMA NA HASA MWEZI HUU ULIOISHA NA PIA TUUKARIBISHE MWEZI WA KUMI NA MOJA KWA FURAHA. PIA TUSISAHAU KUKUMBUKANA:-)...Kapulya.

Monday, October 29, 2018

MAPISHI YA LEO KANDE, MAHINDI NA UGALIWA KUCHOMA/KUOKA

 Katika chungu ni kande zikipikwa na pembeni yake mahindi yakichomwa yaani raha hasa kipindi kile cha masika.
Ugali uliolala usitupe, choma/oka ni kitafuno kizuri saba kwa chai asubuhi....jaribu utaona utamu wake.... panapo majaliwa ttutaonana tena karibuni.

Thursday, October 25, 2018

PICHA YA LEO:- MARA NYINGI NIKIPITA NJIA HII YA IRINGA NI LAZIMA NISIMAME HAPA KUNUNUA SAMAKI

Ukiwa njiani utakutana na wachuuzi wa samaki, kama huyu mama ...picha kwa hisani ya Mjengwa.

Monday, October 22, 2018

WIKI ILIYOPITA TULIKUWA SONGEA MKOANI RUVUMA TUKIANGALIA MILIMA LEO TUENDELEE MBELE KIDOGO MPAKA MBINGA ILI KUANGALIA MANDHARI NZURI YA KIJIJI CHA LITEMBO

 NIMEYAPENDA HAYA MAZINGIRA
 Ebu angalia kulivyokuwa kwa kijani mpaka raha hata kama unapita tu lazima utasimama

Hapa nahisi ni Ofisi kama wasoma kibao/bango

Friday, October 19, 2018

ASILI YA KABILA LA WANGONI SEHEMU YA KWANZA


Wangoni ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, hasa upande wa Kusini wa Songea. Pia wako Msumbiji. Lugha yao ni Kingon

Wednesday, October 17, 2018

LEO TUTEMBELEE KWETU SONGEA KIJIOGRAFIA

 Huu ni mlima MATOGORO uliopo kkaribu na kijiji cha MAHILU kilichopo Songea
 Hapa ni magharibi ya kijiji cha Mhukuru twakutana na mlima kipululu
 Mlima Litimbanjuhi uliopo karibi na kijiji cha Namatuhi
 Hapa pia ni mlima Manolo uliopo kijiji cha Namatuhi pia
Kama  watoka Wino kuelekea Iringa utaona mandhari hii nzuri ya milima

Monday, October 15, 2018

JUMATATU HII TUTEMBELEE MJI WA IRINGA

Napenda kuwatakia Jumatatu njema na kila la kheri kwa chochote  mtakachofanya.  PAMOJA DAIMA

Wednesday, October 10, 2018

UTALII WILAYANI NYASA:- LEO TUFANYA UTALII KWENYE UFUKWE ULIOPOMJINI LIULI

     

Utalii ni sekta inayokua kwa kasi sana Duniani. Imechangia katika kukua kwa uchumi wa nchi nyingi sana, imeongeza ajira nyingi sana, zipo zile za moja kwa moja na zingine ambazo si za moja kwa moja.

Sehemu zinazo wavutia sana watalii si mbuga za wanyama, si milima, si mapango bali fukwe nzuri na tulivu za bahari na maziwa.
Uswisi inajulikana kama 'the playing ground of europe' kutokana na ziwa dogo la Geneva, Visiwa caribean, Zanzibar, Mombasa na kadhalika zimekuwa zikiwavutia sana watalii kutokana kuwa na fukwe zinazovutia.
Ziwa Nyasa ni moja ya maziwa safi bado halijaharibiwa na shughuli za kibinadamu.Lina fukwe nzuri,safi na salama,maji meupe kwa ajili ya michezo mbalimbali...kama mashindano ya kuogelea, mbio za madau au maboti.
Watu wa Nyasa, ili nionekane mkweli kuhusu fukwe zetu mimi naonesha mfano-Ufukwe wa LIULI.
Na John Joseph, Liuli
 

Wednesday, October 3, 2018

TANGU WAKIWA WADOGO HUPENDA KUJITUMA, LAKINI JAMII HAIWAAMINI

Wiki hii tuanze na picha hii..yaani kama ujumbe usemavyo hapo juu....NAPENDA KUWATAKIENI WIKI NJEMA NA PIA JUMATANO NJEMA....KAPULYA WENU!!

Thursday, September 27, 2018

LIJUI TUNDA LA PAPAI NA FAIDA ZAKE KWA AFYA......

Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha. 

Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.

Wiki mbili zilizopita tumeona vyakula kama karanga, korosho vinavyoweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, wiki hii pia tunaona papai nalo limo kwenye orodha ya vyakula vinavyotoa kinga ya ugonjwa huo.

Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.

HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonyesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.

KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.

KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya ‘beta-carotene’ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k

NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.



TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.

CHANZO JAMIIFORUMS:- AHSANTE SANA KWA ELIMU NAMI NIMEONA NISIELIMIKE PEKE YANGU NIKAONA NIWEKE HAPA KINARAZANI.

Friday, September 21, 2018

NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA...HAYA TUFURAHI PAMOJA NA KIPANDE HIKI CHA NGOMA...



Tuwukeee tuwukeee kamwimbo katamu sana. Natamani kuungana  nao na kucheza ila nabaki kucheza peke yaangu....NAWATAKIENI MWISHO WA WIKI HII UWE WENYE FURAHA NA AMANI! KAPULYA WENU

Thursday, September 20, 2018

PALE UNAPOLIMA UNATUMAINA KUVUNA NA SASA MATOKEO TUNAYAONA

Hapo mwaona baadhi ya mazao niliyovuna nyanya, tikiti maji ambalo ndani ni njano tamu sana, zabibu  na pia mwaona kwa pembeni ni pilipili  ni raha sana  kula vyakula ulivyolima mwenyewe kwa mikono yako. KARIBUNI TULE NDUGU ZANGU.

Monday, September 17, 2018

Thursday, September 13, 2018

FAHARI YA MKULIMA NI KULIMA NA KULA ALICHOVUNA....KAZI YA MIKONO YAMGU...

kula vyakula unavyopanda mwenyewe ni kwamba ule utamu unazidi...nilipanda hili tunda aina ya tikiti maji lakini lenyewe ni la njano ndani  ha picha hapo chini yaonyesha vizuri zaidi. Nilianza kulifuatilia hili tunda  kwa ukuaji wake kama uonavyo ua
Na sasa lishakuwa kubwa yaani ni kama boga ila bado kukomaa ni kwamba ukomaaji wake ni mpaka hili ganda liwe njano njano....
Na leo siku rasmi ya kuvuna na kula. Utakula ulichopanda, hakika najisikia fahari sana ....

Tuesday, September 11, 2018

UJUMBE WA JUMANNE YA LEO KUTOKA KWANGU KUJA KWENU...

UJUMBE:- Kuna muda inabidi uanguke chini zaidi ya hapo ulipo ili uweze kusimama na kukaa juu zaidi ya hapo ulipo...
Hata siku moja usijaribu kukata TAMAA. Dharau, matusi na kebehi: havimzuii mtu kungára.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPA HAPA...KAPULYA WENU.

Monday, September 3, 2018

TUANZE MWEZI HUU WA TISA NA WIKI YAKE YA KWANZA KIHIVI .....

Nikiangalia hawa watoto warukapo kamba natamani siku, miaka irudi nyumba ili nami niweze kuruka tena ...UJUMBE:- WAACHENI WATOTO WAWE WATOTO.

Wednesday, August 29, 2018

PENDEZA KWA UBUNIFU WA KITANZANIA

Umuhimu wa kupendeza uko wazi kwa kila mtu,mara nyingi mavazi yamekuwa kama kipimo cha utanashati,basi ili kuongeza mvuto yafaa kuongezea vitu vya pekee vilivyotengenezwa kwa ujuzi wa kimasai ili tu kuonyesha utofauti kimitindo na utanashati..

Kazi za mikono ya wapendwa wetu ambao wanadumisha utamaduni  inapendeza sana

Monday, August 27, 2018

MIMI NDIO NILIMUA BATA MZINGA KWA BAHATI MBAYA


KATIKA PITAPITA ZANGU NIMEKUTANA NA HILI FUNZO NIKAONA NIWEKA HAPA ILI NA WENZANGU MUWEZE KUSOMA NA KUJIFUNZA KARIBUNI:-

Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lakini ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama. Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama msafiri amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya.

Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama. Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena msafiri amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama.

Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia..
"Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mimi ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe.
Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena.

FUNZO,
Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe.
*MUNGU ATUSAMEHE DHAMBI ZETU NA ATUWEKE HURU...*

Sunday, August 26, 2018

JUMAPILI YA LEO TUWE PAMOJA KWA MAOMBI NA HII NI SALA YANGU

Ee Mungu wajua sababu ya mimi kuendelea kuwepo kwenye uwepo wako, naomba uendelee kunijalia hekima na busara katika kukabiliana  na majaribu mbalimbali maana wewe ndiye wajua leo yangu na kesho yangu itakavyokuwa.
AMINA