Tuesday, August 30, 2011

NILIPOKUTANA NA MWANABLOG MARKUS MPANGALA

Baada ya kukutana na kaka S hapa Ruaha safari ikaendelea kufika Dar es Salaamau, ikawa bahati tena nika/tukakutana na mwanablog mwingine pia ni mjomba na rafiki wa karibu sana. Si mwingine tena ni Mzee wa Lundu Nyasa.


Alijitahidi na akaja hapa Silver Sands kutusalimia hapa ni yeye Mzee Lundu Nyasa/Markus Mpangala, Yasinta na Kijana Erik.
Na hapa ni Markus na wajomba zake Erik na Dada Camilla.... Ilikuwa ni furaha kukutana na yeye. Kwani kama kawaida huwa furaha sana kuonana tulibadilisha maneno mawili matatu na muda ukawa ni mdogo ....

8 comments:

  1. Safi sana, alituwakilisha ambao hatukupata bahatii ya kukuona

    ReplyDelete
  2. Najua ile siku,
    furaha ilidumu,
    vicheko vitamu,
    soga adimu,

    mioyo iloja hamu,
    hamu kufahamu,
    muda gani utadumu,
    lakini siku tamu,

    Camilla ulicheka,
    utani nlokulazimisha,
    ukacheka kwa nukta
    Erik mwana wa Yasinta,
    Soka analipenda.

    naweza kuandika mengiiiiiiiii lakini ni raha sana kuona ana marafiki na wale tupendanao. Erik mjomba kazana hadi umpiku Zlatan nawe Camilla Lol...... kama Naomi Campbell. Hakika binti Yasinta anafaa kuwa mwanamitindo. Nitafurahi siku nikimwona anafanya kazi hiyo. ila chaguo lako...... utunze.

    ReplyDelete
  3. ayaaaaah! atakuwa alijidai kweli..we mtani shemeji hii sikukuu mie mgeni wako sasa ole wako uzime simu kisa kulewa ulanzi

    ReplyDelete
  4. Hii safi sana! Ni fursa adimu na adhimu pia!

    ReplyDelete
  5. Haya ndiyo maisha na mafanikio bi mkubwa wetu!

    ReplyDelete
  6. TOUCHING BASE!

    Tunashukuru sana mumekuja kututembelea. Mbona lakini mumekimbia haraka na kurejea ng'ambo? Muliogopa joto nini...?

    Haya, karibuni tena, Watoto Wazuri!

    ReplyDelete