Wednesday, August 31, 2011

Mtoto huyu ametelekezwa na wazazi wake baada ya kuzaliwa na ulemavu njia ya haja kubwa!!!!

Haya ndugu zanguni ile siku ya kipengele cha marudio ya makala/mada mbalimbali ndio leo yaani ile JUMATANO. Na leo katika pita pita zangu nimekutana na makala hii ebu soma mwenyewe...Mimi nimeipata hapa.
----------------------------------------------------------------------------------------------
Na Albano Midelo.
MTOTO Anna Mapunda mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Mkako wilayani Mbinga mkoani Ruvuma anahitaji msaada wa matibabu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam baada ya kuzaliwa na ulemavu sehemu ya haja kubwa.
Mtoto huyo anasumbuliwa na tatizo la kutokwa na sehemu ya haja kubwa nje kila anapokwenda kujisaidia na kwamba sehemu hiyo hukaa nje kwa hadi saa tatu kisha huanza kurudi yenyewe taratibu ambapo mtoto huyo hupata maumivu makali.
Kutokana na mtoto Anna kuzaliwa na tatizo hilo,baba yake mzazi anadaiwa alikuwa anampiga mtoto huyo kila sehemu ya haja kubwa inapotoka nje wakati anajisaidia hatimaye aliamua kumpa talaka mke wake na kwenda kuoa mwanamke mwingine ambapo mama mzazi wa Anna naye aliamua kwenda kuolewa na mume mwingine katika mji wa Mbambabay mwambao mwa ziwa Nyasa.
Mtoto Anna akiwa na mama yake mzazi tatizo hilo liliendelea kumsumbua mtoto huyo ingawa alimpeleka katika zahanati ya kijiji pamoja na kwenda kwa waganga wa jadi kwa ajili ya kutafuta tiba za jadi ,hata hivyo tatizo liliendelea hali iliyosababisha mama huyo kumtelekeza mtoto wake baada ya kukata tamaa.
Mtoto Anna mapema mwaka huu alichukuliwa na shangazi yake ambaye anaishi mjini Songea na kwamba baba mzazi wa mtoto huyo alimwambia dada yake ambaye ni shangazi ya mtoto huyo kuwa amchukue ampeleke hata kwa wachuna ngozi yeye hamtaki kwa madai kuwa ameleta laana katika familia yake.
Shangazi ya mtoto huyo alimchukua mtoto huyo na kuanza kuhangaika ili kutatua tatizo hilo ndipo alimpeleka kwa rafiki yake katibu ya Tanzania Assemblies Of God TAG kanisa la Ruhuwiko Songea Veronika Milanzi pichani kulia akiwa na mtoto Anna ambaye alikuwa akimpeleka katika kanisa hilo kwa ajili ya kumfanyia maombi kila siku.



“Nilimpompeleka siku ya kwanza kanisani kwa ajili ya kufanyiwa maombi mtoto huyu alikataa kurudi tena kwa shangazi yake tangu wakati huo hadi sasa ni karibu mwezi wanne mtoto huyu anaishi na mimi ,shangazi yake amekubali niendelea kuishi naye hadi sasa lakini tatizo lake la kutoka haja kubwa bado linaendelea’’,alisema
Katibu huyo wa TAG licha ya kumfanyia mtoto maombi kila siku lakini pia alichangishana fedha na baadhi ya waumini ili kumpeleka mtoto katika hospitali ya misheni ya Peramiho ambako walimchunguza na kudai kuwa angekuwa na tatizo la kutoka utumbo wa haja kubwa bila kurudi ndani wangemfanyia upasuaji na kumaliza tatizo hilo na kwamba kwa kuwa utumbo wa haja kubwa wa mtoto huyo unatoka nje anapokwenda haja na kisha unajirudi ndani pole pole hawana uwezo wa kumfanyia upasuaji.
Akizungumzia kitaalamu kuhusu tatizo hilo Dk Henry Mayala anasema magonjwa katika njia ya haja kubwa kitalaamu yanaitwa bawasiri ambayo ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi.
Dk.Mayala anabainisha kuwa bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa na kwamba kuna aina mbili za bawasili ambazo ni bawasili ya nje na ndani“Bawasili ya nje hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid na bawasili ya ndani hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili’’,alisisitiza.
Kulingana na mtaalamu huyo bawasili ya ndani imegawanyika katika madaraja manne ambayo ni daraja la kwanza la ni kutotoka katika mahali pake pa kawaida,daraja la pili bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo,daraja la tatua bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo na daraja la nnebawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Amezitaja sababu zinazosababisha magonjwa ya haja kubwa kuwa ni pamoja na Tatizo sugu la kuharisha,Kupata kinyesi kigumu Ujauzito,Uzito kupita kiasi (obesity), Ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex),Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.• Umri mkubwa.
Milanzi ambaye anataka kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam au hospitali nyingine ambazo zinaweza kutoa matibabu anatoa rai kwa watu wenye mapenzi mema kumsaidia mtoto huyo gharama za matibabu,usafiri na kujikimu kwa kuwa yeye haina uwezo.
Iwapo umeguswa na ungependa kutoa ushauri au msaada wa wowote wa kufanikisha matibabu ya mtoto Anna Mapunda andika albano.midelo@gmail.com,simu+255 766463129

8 comments:

  1. Katika habari hii kilichonishangazi na kunihuzunisha zaidi ni kitendo walichokifanya wazazi kumtekeleza mtoto Anna...inakuaje mzazi afanye hivi hasa mama...najiuliza KWA SAUTI...

    ReplyDelete
  2. Yasinta. kila nikiingia humu kwenye blog yako, nataka kusema kitu kuhusu huyu mtoto,najikuta nasita.Naomba sasa nijaribu kusema kidogo.natafuta nijinsi gani mtoto huyu kwatatizo lake asaidiwe.wazazi washa haribu kabisa,jamii ndo inayo msaidia huyu mtoto.sijuwi utaratibu wa hospitali,zetu ukoje.mfano katika hospitali ya wilaya,mtoto anaweza kupelekwa hosipitali ya lufaa muhimbili,kutokana na tatizo lake.ila sina hakika na jinsi linavyo shughulikiwa(samahani) kama swala lenyewe, ni mtoto katupwa,au kunakitu hapo,sijuwi,akili yangu ina kataa,yaani naona kama ,kutupwa,na matibabu nivitu vinavyo kwenda sambamba,badalaya ugonjwa wake.mtoto huyu ni mdogo sana kaokotwa,moja kwa moja serikali ina jukumu,nisawa nawatoto wachanga wakiokotwa inakuwaje,hupelekwa hpsipitali,na baadaye utaratibu hufuata,hivyo sioni tofauti ya huyu mtoto, na hao wengine vichanga .natamani nifuatilie,ila nashindwa.Kaka S.

    ReplyDelete
  3. Kaka S. Hata mimi kwanza nilikuwa nasitasita lakini nikaona niweke hapa kutoka kule nilikoikuta ili kupata mawazo zaidi na pia kama ulivyoona kuna add. ya mail pia namba ya simu. Nadhani kwa kuweza kumsaidia au kujua zaidi twaweza kufanya utafiti...ni wazo langu

    ReplyDelete
  4. Yasinta,kufanya utafiti ni muhimu,ilikujuwa namna ya kumsaidia huyu mtoto.unajuwa kwa kijijini mtoto huyu nina hakika ndugu zake wapo,na vijijini watu wanajuwana kwa urahisi kabisa.pia kwa umri wa mtoto kama huyo narudia tena,ukiokota mtoto,nimoja kwamoja anapelekwa serikali za mtaa,nakama tatizo lilikuwa kaokotwa taratibu za kiserikali zingechukua mkondo wake,hivyo ndivyo mimi navyo juwa.na kwa kuwa nimdogo/mtoto kaokotwa swala la hosipitali ya taifa muhimbili wala halina shida,ilmradi tu awebado katika mzingira ya kuokotwa.sasa huyu msamalia mwema kwanini asimpeleke kunako husika.anyway mengine siyo vizuri kuyajadili hapa kibarazani, ila kweli ninania ya kujua huyu mtoto atasaidiwa vipi.kaka S

    ReplyDelete
  5. Nimewasiliana na albano.midelo@gmail.com na ameniahidi kunijibu.

    ReplyDelete
  6. Duh!! hatuna lugha ya kusema hapo, ni mungu tu awe tabibu mkuu.

    ReplyDelete
  7. Watoto walio chini ya miaka 5 wanatibiwa bure kwenye hospitali za serikali inchuding Muhimbili. Kinachonishangaza kwenye hii story ni hao wahusika badala ya kumpeleka mtoto hospitali ya wilaya, ya mkoa ili akatibiwe na serikali na kupewa referral kwenda Muhimbili wamekaa nae eti wanamfanyia maombi huko kanisani kwao. Basi jumapili moja sadaka zote ziwe ni kwa ajili ya huyu mtoto, na jumapili inayofuata sadaka zote ziwe nauli ya mpeleka mgonjwa lakini aanziwe kwanza hospitali ya mkoa apewe referral letter ili akifika Muhimbili apokelewe kirahisi.

    ReplyDelete