MNADHIMU MKUU WA JWTZ LUTEN JERALI ABDULRAHMAN SHIMBO
Shimbo na wizi wa Trilioni 3: Apata mshtuko na kuzirai!
Hali ilivyokuwa:
JK alienda AFRICA YA KUSINI majuzi na alikuwa anajaribu kuomba msaadakuisaidia TZ, wakamwambia hatutaweza kukusaidia maana una watu wanahela ambazo ni zaidi ya ambazo tungekusaidia. Ndipo wakamfahamisha juuya Mnadhimu wetu kuwa na account huko yenye zaidi ya TZS zaidi yatrilioni 3. Habari hii ilimshtua JK naye akataka ufanyike uchunguziambao uliibuka na usahihi wa taarifa toka SA kwani ilikutwa kwelijamaa ana hela hizo.
Inasemekana Interpol wamempatia Afande Shimbo ukweli wa Account zakenje ya nchi zenye pesa nyingi sana na amechukuliwa chini ya Ulinzi waInterpol kwenda Africa ya kusini kwa matibabu.
Amekuwa akiwakata posho wanajeshi wanaoenda kujitolea kusaidia mataifaya nje na wa ndani.
Hela nyingi zaidi ni pale alipokata fungu kubwa sana toka fedha zashukrani toka Comoro baada ya Tanzania kuisaidia nchi hiyo. Fedha hizozilitakiwa kugawiwa kwa wanajeshi kwa kuisaidia nchi hiyo lakini mkuuhuyu alizipiga panga na hawakujua kuwa alikuwa kafungua akaunti nje yanchi na kuzihamishia kule.
Ameshindwa kueleza kwa undani alizipataje pesa hizi kwenye akaunti naaliishiwa nguvu na kudondoka!
Si Shimbo pekee...
Kuna kijana mdogo sana anaitwa PTE Gwilla, huyu yupo Kurugenzi ya DPAana-deal na salaries za wanajeshi... Kinachoshtua ni askari mdogo sanalakini alikuwa ana maghorofa mawili makubwa, magari aina ya Coastermawili na benki alikutwa na zaidi ya 73mil TZS (kwa mshahara wakeasingeweza kuwa na vitu hivi)
Uchunguzi umeonyesha Gwilla alikuwa anacheza na mishahara ya wanajeshikwa muda mrefu (4yrs) kwa aidha mishahara hewa, kukata 500 kwa kilamwanajeshi (4yrs) na zaidi akawa anakula hela za likizo za wanajeshikwa zaidi ya miaka 3 (2009-2011).
Huyu naye kakamatwa na anashikiliwa Mgulani.
Kuna mwingine...
Ni Mkurugenzi wa malipo jeshini, Brigedia (CC) Zakayo, naye kalambamabilioni ya hela (kiasi sijakinasa vema bado lakini ni zaidi ya EPA)naye anashughulikiwa kwa karibu.
So far, niseme kazi nzuri Interpol, walau watu wataanza kuelewa kuwawatakuja kugundulika wakifanya uhuni wa namna hii.
HABARI HII KWA HISANI YA JAMII FORUM
kazi kweli kweli eti ndio wanasema bongo tambarare!!!
ReplyDeleteMmmhhh sina la kusema,ahsante da'Yasinta!!!Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteKaka Kilasi! si utani ni kazi haswa!
ReplyDeleteRachel Hakika inabidi tuomba sana ili Tanzania yetu ibarikiwe!!
Dada Yasinta yaani nimeshindwa kushangaa ikabidi nipayuke kama hivi http://rijaki.blogspot.com/2011/08/maana-halisi-ya-vijisenti-hii-hapa.html
ReplyDeleteMi nasubiri mwisho wake ndio niseme
ReplyDeleteda Yasinta hii habari nilishawahi kuisoma Jamii Forums yapata mwezi sasa, na kisha ikaonekana kule Wanabidii. baadaye mleta habari kule Wanabidii akalazimishwa kuomba radhi kwa kuleta habari isiyokuwa na ukweli. kisha nikaiona kwenye blog ya Iringa na matukio.
ReplyDeletekuiona tena kwako kunanipa kitendawili kigumu sana. ni kweli habari hii ama ndo yale yale ya kule Jamii forums na wanabidii?
da yasinta hii habari ilitoka siku nyiiingi,ila kama ujuavyo tena ikatokea kitu inaitwaz funika kikombe mwanaharamu apite ilizimwa na wenye nchi,sasa hivi imebaki tetesi,lakini ndio hivyo wananchi tumepigwa konzi lingine kisha tukapoozwa kabla hatujatoa kilio,kaaaz kwel bongo hii
ReplyDeleteyasinta alikuwa likizo ruhuwiko anakunywa togwa kwa viazi vitamu (mbatata)
ReplyDelete@John Mwaipopo
ReplyDeleteTogwa imezidi labda nami ningependa kukubaliana nawe! (LOL!)
Lakini kama ni ukweli (na namwamini Kapulya Mdadisi ameifanya homuweki yake kabla ya kuchapisha), yapo makosa mawili hapo.
1. Kwanza: Ni vibaya tena aibu kubwa kwa jemedali kuwaibia "watoto" wake (yaani askari wa dogo) vilevile na kuibia Nchi! (Kisheria ya kijeshi, jemedali hakubaliki hata kugusa ugali wake kama askari wadogo hawajala na kushiba!)
2. Ni kosa na aibu kwa benki ya huyo Jamaa Jemedali Jizi huko (au niseme "hapa") Afrika Kusini kufichua siri yake. Kila benki DUNIANI KOTE ina wajibu wakuwa msiri juu ya mapesa ya wateja wake... vilevile hao Waafrika Kusini waliemwambia JK kuhusu Jemedali Jizi walijifanya kama wao ni wasafi na watakatifu wasoibia umma, Wanafiki Wakubwa Bondeni Hapa!
Nitembelee tafadhali kwangu ili uone jinsi inavyosemekana wakubwa katika uongozi wetu Bondeni hapa wanavyotumia vyeo vyao ili kuwanufaisha familia zao pamoja na mabepari wa nje ya Bara letu!
http://ninaewapenda.blogspot.com/2011/08/molotov-cocktail-called-obama-zuma.html
Ndio,hii habari ilianzia Jamii Forum (JF) na kusambaa kwenye mitandao mingi. Ilikuwa vigumu sana kwa watu kuiamini kwa kuwa hela zilizotajuwa zilikuwa ni nyingi na mahesabu yalikuwa yanagoma na pia kwa kuwa 'mtuhimiwa' alionekana kwenye runinga Tanzania. Lakini pia ilikuwa ni vigumu kutoiamini kwa kuwa ilitolewa kwa kutumia jina la kinara wa kulipua mabomu anayeaminika sana JF na kusapotiwa na kinara mwingine. Lakini baadae wakaitoa na kupotezea. Hivyo mpaka sasa kuna utata kuhusu hili, wapo wanaosema ni jungu tu ila wapo wanaoamini walau kuna ukweli fulani humo.
ReplyDeleteHaya mwenye macho ayaone, na mwenye sikio asikie,...ukweli ulivyo ni kuwa nchii hii sio masikini kiasi hicho, ila umasikini unatokana na watu wachache kuhujumu na kujilimbikizia mali kinyume na haki na sheria...
ReplyDeleteThis is not breaknews:
ReplyDeleteIt is shocking news.
Hapo ndipo unapogundua ni jinsi gani binaadamu tulivyowabinafsi na kutowajali wengine
Hali kama ndo hii tunakazi nzito.
mmh! hii kali,kama kuna ukweli juu ya hiyo issue,basi wabongo ni noma.ila yasinta check isije ikawa ni majungu ya wanafki juu ya jamaa(shimbo) maana issue ya udini imeshika kasi ile mbaya hapa bongo sasa hivi.WABONGO TWENDAKO SIKO.
ReplyDeletehakuna majungu wala nini hapa. hiyo habari ni ya kweli kabisa. hivi mnafikiri kiburi cha ccm kinatoka wapi?
ReplyDeleteni kwa kuwawanakula pamoja na hao wanaotakiwa kulinda taifa. hata ukiangalia muundo wa uongozi, tanzania inatawaliwa kijeshi, wala hakuna uongozi wa kiraia. uchaguzi unaofanywa siku zote ni geresha tu.
kinana - mjeshijeshi, makamba - mjeshijeshi, kikwete - mjeshijeshi, na wengine kibao. pinda - usalama wa taifa. kuna wengine kibao ambao ni viongozi ambao aidha ni kutoka vyombo vya ulinzi na usalama (wa plain clothes), au walikuwa huko kabla - ambao wananchi hawajui historia zao za kazi.
wako hata wafanyabiashara geresha ambao wamekuja kuwa wabunge au viongozi, lakini ambao ni mashushushu.
hivyo basi, ukombozi wa kweli Tanganyika utakuja siku ile ambapo wananchi wataamua kujitolea maisha yao kwa faida ya vizazi vijavyo.
ukombozi utakuja pale ambapo wanajeshi watapewa elimu stahiki badala ya hali ilivyo sasa ambapo sifa kuu ya kujiunga ni kuwa na miguu na mikono yenye vidole vya kuchezea 'trigger'. matokeo yake ni dhuluma kama tuzionazo huku wao hawajui namna ya kudai na kupata haki zao. maskini askari wetu wanakandamizwa wasijue la kufanya.
askari wanahitaji mwamko kama wa wale askari wa nchi za kiarabu waliochoshwa kutumiwa na ccm zao.
Amekata shea yake mwacheni tu. Nchi hii uonevu mwingi sana. Kwa nini maisha mazuri yawe kwa wanasiasa tu? Hata mie nikipata nafasi kama hiyo nitakata shea yangu niwaache wadanganyika muendelee kudanganywa.
ReplyDeleteHapana c wez kusema
ReplyDeletehuyu huyu jemedari,
makubwa lakini kwa nchi yetu ni kawaida kabisa vitu kama ivyo kutokea .......
ReplyDelete