Monday, November 22, 2010

MAONI YA MTAKATIFU SIMON KITURURU KUTOKA KWENYE MADA/PICHA YENYE KICHWA CHA HABARI:- NIMEUPENDA UBUNIFU HUU!!

Ya nini kupoteza pesa kuwanunulia watoto vifaa vya kuchezea wakati inawezekana kutengeneza. Yaani hapo vitu vunavyohitajika ni dungu baada ya mafita ya kula kwisha, mwanzi, ndala zilichoka kwa ajili ya matairi bila kusahau ufundi. Haya basi kimbia gari halimgoji mtu Erik ndiye dereva ...tena bei nafuu kabisssssaaaaaaaaaaaaaaa-
natafuta kitoweo kwa manati:-)
Nimeyapenda maoni haya ambayo yanasemaukweki wa sasa na ule wa zamani. nakumbuka wakati nilipokuwa mdodo/kabinti nilikuwa nabeba kigunzi au kile kilixhokuwa kwenye mkungu wa ndizi kama mtoto. Zamani tulikuwa hatununuliwo vitu kama sasa. Ukitaka kujikumbusha ni picha gani basi bonyeza ubunifu. Ahsante sana Mt. Simon Kituiruru- Na hivi ndivyo alivyoanza mt. Simon:-

Si utani! Ubunifu ni muhimu!

Tatizo kiitwacho maendeleo kinafunda watu wengi tu kuwa ujanja ni kununua na ununuacho ghali zaidi ndio ushahidi wewe mjanja zaidi au tu Bab KUBWA kuliko ukiwa unatatua mambo mwenyewe kiubunifu wako mwenyewe.

Kwa mfano siku hizi BONGO(mijini) unakuta hata manati watoto wanataka wanunuliwe.

Ukilinganisha na enzi zetu ukipenda kuchezea magari unajitengenezea kwa waya au hata makopo na ikibidi unaiba ndala nyumbani ukachonge matairi ikiwa ni kutatua tu tatizo la kutaka kucheza gari kibunifu ambalo unajua Mzazi anaweza asikununulie.

Tunako kwenda sijui nini kitatokea kama ubunifu ni jinsi ya kununua na wapi pa kununua wakati mengi tu unaweza kubunia na kutatua mwenyewe.

Fikiria hata chakula kwenye menu za bongo ubunifu ni hafifu sana. Ni yale yale CHIPSI mayai, ugali kwa maharage na kadhalika... wakati kibano kilitakiwa kitengeneze ubunifu kama kibano cha uhaba wa chakula kilivyowaletea ubunifu wa PIZZA kwa Waitaliano masikini.


Nawaza tu kwa sauti!

3 comments:

  1. hii inapendeza sana kwani wanabuni kwa kutumia mawazo yao zaidi na wanapata watakacho kwa jasho lao!.

    ReplyDelete
  2. nimekubali huu ubunifu ni kwelki tuwaongezee taluma

    ReplyDelete