Tuesday, November 23, 2010

Ni muhimu kufanya mazoezi !!!!

Ni muhimu kufanya mazoezi, ni kwamba unauweka mwili wako safi na pia unaepuka ma magonjwa madogo madogo.Bibi anasema, usidhani wewe tu unaweza , hata mimi naweza usidhani umri ni kitu ha ha ha ha:-)!!!! Mmmmmhhh!! nawaza kwa sauti hivi huyu bibi ana mifupa kweli?




15 comments:

  1. Nikienda Kijini kwetu huko upareni, naona maisha ya kawaida tu watu waishiyo ni mazoezi tosha. Kwanza ni milimani, ukienda tu hata dukani na kurudi nyumbani ni sawasawa na mtu mwingine kafanya HIKING.

    Tatizo ni kwamba watu wanafikiri mazoezi ni mpaka yafanane na kinachoitwa mazoezi kwa mfano picha zilizowekwa hapa.


    Naamini mazoei yanaweza kuwa tu mpaka ingawa una gari,....

    TEMBEA.

    Ingawa unawakukubebea mizigo,....
    ...beba mwenyewe.

    Kwa misuli ya mwili,...
    piga deki nyumba yako,...
    ...ingia mpaka chini ya uvungu.


    Usitumie Lifti au ngazi zikupandishazo zenyewe (Escalators)

    ...panda ngazi.


    Kimbilia BASI. Kimbia kama umechelewa Kanisani , Kwa mpenzi au Nyumbani.


    Jinyoshe kusugua ukuta.

    Jaribu staili tofauti hata zile ngumu za kufikia utamu wakati unafanya uasherati na sio za kimishenari tu kila siku.


    Shughuli nyingi za nyumbani usipozilainisha ni zoezi tosha na kikubwa unakuwa unaua ndege wawili kwa jiwe moja.

    Kwa Wabongo si lazima tuige mazoezi kama yaletwayo na wamagharibi. Mtu unaweza ukapanga siku yako na shughuli zako zikageuka mazoezi.


    Nachojaribu kusema ni:
    ..
    nakubali mazoezi ni muhimu lakini sio lazima yafanyike kama yale yaliyozoeleka kuitwa mazoezi.

    Kumbuka kuruka kichurachura ni mazoezi ,...
    ....lakini kuruka kichura kwa weza kuitwa adhabu kama akilini hukuchukulii kama mazoezi.

    Samahani kwa kuwaza kwa sauti!

    ReplyDelete
  2. We bibi kwenye picha ya chini hapo usituyeyushe hapo, utawezea wapi zoezi kama hilo?.

    ReplyDelete
  3. Du..huyo bibi lazima anapumua kupitia kila uwazi kwa kufanya hayo mazoezi....

    ReplyDelete
  4. Naungana nawe dada. Mazoezi ni muhimu sana katika miili yetu.

    ReplyDelete
  5. Kitururu naona umetupa neno la leo.

    Yasinta nasikia na wewe kwa mbio huwezekaniki....

    ReplyDelete
  6. Kaka M. huyo bibi kwa kweli amevunja rekodi.

    Mt. umeneno kwa kweli.

    Kaka Baraka! kuna akina bibi wana nguvu za mazoezi sio mchezo.

    Israel! kaazi kwelikweli.

    Ahsante Naxy!

    Da´Mija ! we ulijuaje? Basi siku ya kukutana na wewe tutafanya mashindano au unasemaje..LOL

    ReplyDelete
  7. Hakuna tatizo Yasinta ngoja nianze kujifua kabisaa..

    ReplyDelete
  8. Mija! HA HA HA HAAAAAA!! Umenivunja mbavu eti uanza mbona sasa utakuwa mwa mwisho...

    ReplyDelete
  9. @ Mtakatifu: umenisemea na mimi. Sina la kuongezea.

    ReplyDelete
  10. ...Jaribu staili tofauti hata zile ngumu za kufikia utamu wakati unafanya uasherati na sio za kimishenari tu kila siku...

    duhu! tatizo nini sijui

    ReplyDelete
  11. "Majege avi nagu" (Mifupa anayo), tofauti yetu na yeye ni kwamba bibi huyu alianza mazoezi tangu akiwa mdogo, na huenda alikuwa mwana mazoezi na sarakasi tangu utoto wake ndio maana kwanza ameweza kuishi umri mrefu na pia anaweza mazoezi makali hivyo.

    ReplyDelete
  12. Bibi!!!
    Jamani Israel Saria!!!! Hiyo comment yako heeeee!

    ReplyDelete
  13. Duh yasinta hayo mazoezi ya bibi mbona magumu sana akimaliza si itabidi anywe diclopa? of course mazoezi ni kitu kizuri sana kwa binadamu kwani yanatufanya tuwe fit i hata katika utendaji wetu wa kazi hususani sisi wanawake kwani kazi zetu ziko very complicated.
    NIce day sis

    ReplyDelete