Makala yangu niliyoiweka hivi karibuni niliyoipa kichwa cha habari kisemacho Sitarajii kuwa mwanaharakati, imeleta changamoto kubwa sana kiasi kwamba nimeshindwa kuiacha ipite hivihivi. Kwa yule ambaye hakupata fursa ya kuisoma anaweza ku bofya hapa na kujikumbusha.
Nimesoma maoni ya wadau wote kwa umakini kabisa na pia nimefurahishwa sana na barua ya mdogo wangu Koero aliyoiweka hapo kibarazani kwake na kuipa kichwa cha habari kisemacho Dada Yasinta nimeishitukia janja yako, unaweza kubofya hapa kumsoma. Katika barua hiyo, pamoja na utani mwingi lakini kuna mambo ya msingi kabisa yaliyojitokeza ya kujadili kwa kina.
Nakumbuka nilipokuwa likizo nyumbani Songea mwaka juzi nilikutana na utitiri wa taasasi nyingi zisizo za kiserikali maarufu kama NGOs. Kila taasasi ilikuwa imelenga jamii fulani. Nilikuta NGOs, za Ukimwi, unyanyasaji wa wanawake na watoto, za wajane, za kidini, za kilimo, za afya, za walemavu, ilimradi kila eneo linaloonekana kama litavutia wafadhili limeguswa na hizi NGOS.
Binafsi sikushughulika sana kutaka kujua manufaa yanayopatikana kupitia hizi NGOs, kwa sababu ya labda ya majukumu niliyo nayo wakati nilipokuwa likizo.
Baada ya mtundiko wangu wa hiyo makala ya kukanusha kuwa na nia ya kuazisha NGOs, Mdogo wangu Koero na kaka Bwaya wakaja na hoja kuwa sio NGOs zote zilizo na malengo yaliyokusudiwa.
Kwamba NGOs nyingi zimeanzishwa kinafiki na wamiliki wake ni wasanii tu kwa ajili ya kutaka kutafuna fedha za wafadhili kwa mgongo wa kusaidia jamii fulani.
Hata hivyo kaka yangu Chacha Wambura na yeye akaja na hoja nyingine, kwanza hakupinga hoja iliyotolewa na Koero na Bwaya pamoja na wadau wengine, bali yeye alikwenda mbali zaidi akitaka mjadala huu ujadiliwe kwa mapana. Chacha Wambura anadai kuwa kuna wakati wafadhili wanatoa $ 5,000 kwa ajili ya mradi halafu wanatumia $15,000 kwa ajili ya kufanya Monitoring na evaluation.
Chacha hakuishia hapo akazidi kubainisha kuwa unaweza kusikia zimetolewa bilioni kadhaa za dola kama msaada katika mradi fulani lakini asilimia 85 ya msaada huo ni technical support ambapo wanaotoa hiyo technical support ni wao hao hao yaani wafadhili, kwa hiyo utaona kuwa kuna mlolongo wa unafiki kutoka kwa hao wafadhili mpaka wanaotumia yaani wenye hizo NGOs.
Kitu kingione kilichojitokeza ni wamiliki wa hizo NGOs, ambapo inasemekana wengi wao ni wastaafu, waliotoka serikalini au world bank, ambao wanajua namna ya kuandaa makabrasha na kupata hizo fedha za wafadhili.
Wengine wanaotajwa ni vijana walioshindwa kujiajiri kulingana na taaluma zao, na kutokana na kuonekana kuwa NGOs ni njia ya mkato katika kujitengenezea fedha za chap chap kutoka kwa wafadhili, vijana wengi wamekimbilia huko na ndio sababu ya kukuta kuna utitiri wa hizo NGOs lakini tija hazionekani
Jamani mimi ni muongoza mjadala tu hapa na nilichoandika ni mnyumbulisho wa kile kilichozungumzwa na wachangiaji kwenye mada kuu. Je wadau mnasemaje juu ya hizi hoja zilizojitokeza?
Nawasilisha
NA NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA TATU YA MWAKA 2010 IWE NJEMA KWA WOTE!!!
Duh!
ReplyDelete@ yasinta: Ile NGO yako ya RNWCCE a.k.a Ruhuwiko NGO for Woman and Children Crying Everyday imenifurahisha sana. Nadhani wa kusaidiwa ni pamoja na mimi au vipi? Au kwa kuwa ni mwanaume na silii kila siku? :-(
ReplyDeleteTurejee kwenye mada: kama ilivo kwenye siasa kuna NGO genuine na feki. kuna zile zijulikanazo ka briefcase NGOs na sasa kuna terminology mpya kuwa kuna flush-disk NGOs. Sababu hasa ni kuwa unakuta wana plans safi sana, lakini hawana address. Kama kuna mfadhili wanaweza kumuomba Koero nyumba yake ikawa ofisi kwa masaa kadhaa ili huyo mfadhili aione 'ofisi' na akishatoa fweza ndo imetoka.
Tukija kwenye ishu uloieleza jinsi ulivoziona NGOs huko Ruhuwiko, hali ni hiyo hiyo kote Tanzania. Mfumuko wa NGOs ulianza mwaka 1992 mara baada ya mkutano wa Rio De Jeneiro ambapo baada ya mkutano huo fweza nyingi zilielekezwa kwenye maswala ya mazingira na kupelekea baadhi ya wajanja wakiwemo vingozi wa serikali kuanzisha NGOs ili fweza hizo zielekezwe huko na kuwaweka ndugu zao kuwa 'wasimamizi'!
Mlolongo wa matukio yenye pesa umefuata kama vile Ukimwi, mazingira, wanawake na watoto na sasa kivumacho ni climate change. Kwa hiyo NGOs nyingi za wajanja zinaanzishwa kufuata upepo wa pesa zilipo. Ni chache ambazo kama zinafanya mazingira hazibadilishi mwelekeo kwa kuwa zina mpango mkakati. Nakumbuka kuna NGO moja huku kanda ya ziwa iliwahi kumkatalia balozi mmoja wa nchi za scandnavia huko kwa akina Yasinta ambaye baada ya kuwatembelea akasema 'naona mnafanya kazi nzuri na nadhani mnahitaji kusaidiwa na nikirudi Dar ntaidhinisha kiasi cha $40,000 mzifanyie kazi'. Lakini bosi wa NGO hiyo akamwambia 'mkubwa, hatuzihitaji hizo pesa zako kwa kuwa bajeti yetu ya miaka 5 inazo pesa za kutosha hatuhitaji zingine, labda usubiri baada ya miaka 5'
Je kuna ngapi kama hizo?
LABDA WADAU WATUAMBIE: NGO NZURI NI ZIPI? AMA WAWEZA KUKUTA NGO NZURI AMBAYO INATEKELEZA MALENGO YAKE KAMA HIYO YA YASINTA? :-( NA TUFANYE NINI TUWE NA NGO BORA?
NAACHA :-(
Kaka Chacha hapo umenena kitu, na inaonekana wewe ni mzoefu wa mambo hayo.
ReplyDeleteNimekuwa mfuatiliaji wa mada za dada Yasinta mara kwa mara,na nimekuwa nikishuhudia wachangaiaji wengi kupta kiasi, nashangazwa na ukimya wa wadau katika hili, au ndio dada Yasinta kagusa pale penyewe, nadhani labda kawagusa walengwa na ndio maana sioni wadau wakichangia mada hii.
Nawatakia uchangiaji mwema..lOL
Ahsante wote mliotoa maoni na wale waliosoma tu na kupita.
ReplyDeleteMCHARUKOOOOOOOOOOOOOOOOOOO....... wajameni nani kawadanganya NGONO oooooh sijui NGOZI..... NGO zinamaanisha kweli wanachomaanisha? si mnajua utitiri wa NGO sasa naona mnaumiza vichwaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeleteYasinta ebu neda kalime mahindi huko wala tusidanganyane hapaaaaaaaaaaaa.
NIMEKUSHTUKIA CHACHA ni mmoja wa wamiliki wa NGO, unauhakika? kwaheriiii
@Mpangala: nadhani hujajadili mada.
ReplyDeleteMimi kwa taaluma nimesomea civil/highway engineering hapa njini na Ni kweli kwamba mara baada ya masomo hayo nilijiunga na major seminary kwa masomo ya (falsafa na theolojia) ili niwe PADRE lakini uliponishinda nilirejea kijijini nikutane na LAANA ya Bwana kwa kumkimbia :-(
Ni wakati natumikia Laana ya BWANA nilipoajiriwa na NGO moja na kufanya nayo kazi kwa miaka 10!
Hivyo biashara ya huko kwenye sekta hiyo naielewa vema na siyo lazima niwe mmiliki.
Turejee kwenye Hoja ya msingi kama nilivouliza hapo juuu...!