Tuesday, January 19, 2010

PIACHA YA LEO:- NAKUMBUKA ZAMANI NILIPOKUWA MDOGO!!!

Leo nimekumbuka nilipokuwa mdogo kwenda mstuni kuokota kuni, na hapo ujue ukirudi inabidi uende mtoni/kisimani kuchota maji. Wakati huo huo maharage yapo jikoni inabidi uchochee na kisha inabidi kutwanga mihogo. Ama kweli tumetoka mbali!!! Haya ndio maisha tuliopitia wengi huwa najiuliza sijui ni muda gani nilisoma?....!!

10 comments:

  1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!January 19, 2010 at 9:35 AM

    Na kwa mtizamo wa ki-NGO hiyo ni child labour? Sawa?

    Ni kweli umepitia hivo...hebu tweleze ulikuwa unajisikiaje? na kwa kumuuliza mwanao sasa anajisikiaje?

    ni katika kujua hayo ndipo tutakapoelewa tofauti ya malezi yale ya wakati ule ambapo mtoto akikosea njiani huko atacharazwa mboko na jirani na akirejea akasema ni mboko kwnda mbele na haya ya sasa ambapo jirani akikucharazia mwanao hata kama alikuwa na makosa inakuwa vita :-(


    na kwa wenye hasira kama Mt. Simon na Yasinta wanaweza wasisalimiane mwaka mzima :-(

    sasa tuko katika maisha ya haki za mtoto na akina mama. Unadhani zinajenga ama zinabomoa tofauti na makuzi tulopata huko zamani?

    cheers!

    ReplyDelete
  2. Wengine hatujapitia huko ila ni interesting memories. Nilikuwa na rafiki yangu nadhani darasa la pili au tatu alikuwa anajua kusonga ugali...mie najua kusonga ugali sijui miaka mingapi...we all grow up differently

    ReplyDelete
  3. huwa nadhani tunakuwa na fikira potofu kudhani maisha haya ya kisasa ni bora zaidi ya haya ya vijijini. vijijini kuna uhalisia na ya kweli.

    Candy1 unajua kusonga ugali au kupika ugali?

    ReplyDelete
  4. haya ndio maisha wanayoishi vijana wetu wanaosoma shule za kata!

    ReplyDelete
  5. uharibifu wa mazingira au.....
    Tafuta na picha ya kijana anayechunga ng'ombe ili nasi tuvute hisia zetu za wakati huo

    ReplyDelete
  6. Kwani hata shule zenyewe za kusoma zipo Da Yasinta? Tunapoteza vipaji vingi sana kwa kutotilia mkazo suala la elimu vijijini.

    ReplyDelete
  7. CBE Dodoma, mtoto wa watu jua kali anaenda kuuza mzigo wa kuni sh. 100 au 200 Duh tutatoka kweli???

    ReplyDelete
  8. Ni kweli watoto, si vizuri kuwafanyisha kazi hasa kazi ngumu.
    Binafsi kwa kweli nilikuwa sipendi kabisa kazi kkama kulima, kutwanga nk. lakini ilibidi kwani nisingejitahidi nadhani sijui kama leo hii ningekuwa hivi nilivyo. Na sasa nimepata kitu cha kuwaeleza watoto wangu pia kuwafunza nawaza kusema NAJIVUNA sana. Na pia nimeshaona tofauti za watoto wa hapa na nyumbani TZ. "mtoto mleavyo ndivyo akuavyo"

    ReplyDelete
  9. umenikumbusha maisha ya kijijini kwetu

    ReplyDelete