Kila kabila lina mila na desturi zake kuhusu vyakula. Kuna vyakula akina mama na watoto hawatakiwi kula kutokana na mila hizo. kwetu Ruhuwiko,Litumbandyosi, Kingoli ukila MANGATUNGU(aina ya upupu)au ukila ugali wa BUNDURA(mihogo ya kuvundika) ukila ....unaonekana wewe ni maskini sana. Pia nimeishi kule Ubenani na wao walikuwa wanakula sana MAKANDE(ng´nde)na kuna makabila waliona kuwa wao ni maskini sana. Katika utafiti nimegundua/nimekikuta kitu kama hicho Usukumani, kwa wasukuma wa sehemu za Maswa mpaka Mwagala njia ya kulelekea Meatu ambapo mtu akionekana anakula ugali wa MTAMA anaonekana amechacha ile mbaya!
Je? hali ikoje kwa makabila yenu? Je? wasukuma (najua wamegawanyika; wa Bariadi, Malya, kahama, mwanza, tabora nk) wote wana mila hizi?
Yasinta, katika kujibu swali lako, natapenda kuongelea kuhusu kabila ninalolifahamu vizuri, yaani kabila langu langu, kwa jina la WAIRAQW, maarufu piakama WAMBULU. Kwa ujumla wairaqw ni wakulima na wafugaji. Vyakula vya hadhi kubwa ni Ugali wa mahindi,makande, maboga, maharage, maziwa,nyama,asali samli, mnafu, mchicha pori, matunda pori nk. Vyakula vyote hivyo nilivyovitaja huandaliwa kwa namna nyingi tofauti. Mfano Maboga hupikwa namna nne tofauti, makande nayo hivyo hivyo.
ReplyDeleteTukirudi kwa upande wa suali lako, chakula ambacho kinaonekana ni cha hali ya chini ni ugali wa MTAMA.
Sie ni watu wa shoka. Kazi zetu ni za kutumia nguvu na akili.
ReplyDeleteHatubagui chakula, ila huwa hatupendi wali na ndizi maana ni kama appetizer to kabla ya main dish.
Tunahusudu sana ugali wa aina yoyote kwa samaki.
Hatuna chakula cha maskini kwetu.
Ingia hapo Ukara utapata habari yooooote
Kaka Chib nimecheka mno niliposoma maoni yako.
ReplyDeleteSisi Wabena kande siyo chakula cha kimasikini.
Kuna mboga fulani inateleza mno, huitwa 'delega' huota mara nyingi kwenye mabafu yalojengwa kwa manyasi. Hutambaa. Pia mboga iitwayo 'nyapula' majani ya maharage huchemshwa na kukaushwa ile yasukume miezi ya kiangazi. Pia ugali wa mtama.
Nielewavyo mimi ndivyo. Pengine leo ntajifunza zaidi.
Chib hivi kweli unajua kula samaki kama wanavyo kula wakara?, nijuavyo mimi wakara wakila samaki miiba inachambuliwa mdomoni, na wengine wakila samaki huoni mwiba hata mmoja uliotemwa ha ha ha!!!!
ReplyDeleteSie kwetu Pilau ndio chakula cha kimasikini sana.....LOL
ReplyDeleteKaka Chib LOL......
Sie kwetu kwa upande wa mama yangu yaani upareni kuna mboga inaitwa MSELE, ngoja nimuulize mama inavyopikwa then nitarudi kuwaeleza.....lakini inafana namlenda sema yenyewe inakuwa inatwangwa na kuwa kama unga halafu.....sijui ngoja niulize
ReplyDeleteHii Topic nimeipenda sana mimi kwetu ni Iringa,yaani mimi ni Mnyarukoro Original sijaishi sana huko lakini nafikiri ukila ugali wa dona na mrenda watakuona umeishiwa.Ila ukila kanyama ka mbwa utaonekana matawi ya juuuu....Hhaaa natania jamani wahehe hatuli nyama siku hizi.
ReplyDeleteMiye mwenzenu naona aibuu :-(
ReplyDeletetundizi fulani hivi huitwa GURUTU..aah ukionekana unafakamia hizo basi unaonekana dhofuli hali. namaanisha kule ufukweni mwa ziwa nyasa kunakolimwa mchele namba moja duniani- kyela.
ReplyDeleteYasinta kwa topic jamani. Hii nimeipenda sana halafu inaonyesha umekaa usukumani pia. Kusema ukweli sikujua kama ugali wa mtama ni chakula cha hali ya chini usukumani, ila ninachojua kwa Tanzania nzima ukionekana kila siku dagaa na mchicha unawekwa katika kundi la kuchacha.
ReplyDeleteebitoooke!@ kwetu ukila chakula tofauti na ndizi wewe ni masikini na rofa a kutupwa potelea mbali na umasikini wako
ReplyDeletesiku moja nilenda kijijini bila taarifa usiku kama saa mbili walipakua ugali! sikula na ilibidi wakatafute ndizi gizani na kupika fasta!
Nilisahau kule kwetu Litumbandyosi wanapenda sana kula ugali ulezi na chimbondi. Chimbundi ni karanga zilizokaangwa na kutwanga na chumvi. Je? huu ni umaskini pia?
ReplyDeleteNimerudi tena kusoma maoni, mataya na mbavu zinaniuma kwa kicheko. Nimejifunza kweli kweli.
ReplyDelete@ Mumyhery, kusema ukweli sikuwa najua kama samaki wana miiba, nimezoea kumtumbukiza wote mdomoni na kutema tuvitu tugumu tugumu ambatwo hatutafuniki. Hapo nimepata somo la miiba :-)
Chib:-) umeniacha hoj yaani mbavu zote zinauma inabidi niache kucheka lakini siwezi ningependa kuwaona hao samaki wasio na miiba ama kweli sio wewe tu umejifunza mengi hata mie nimejifunza mengiiiiiiiii. Duh Kublog raha kweli.
ReplyDelete@Yasinta: Blogging is my great companion :-)
ReplyDeleteunajua naweza kukaa kwenye internet 6 hours sana sana kwa ajili ya kublogu na kupekua blogu zoote nizijuazo na nisizozijua. yaani kublogu ni u-krezi
ReplyDeleteYasinta hii Topic ya leo imenichangamsha,unajua wewe mjanja sana umewatega watu wajiseme walikotoka, nimesoma comment zote nimegundua humu ndani kumbe nina ndugu zangu wengi na watani wengi,kila mtu kajitaja yeye katoka wapi,kumbe EDNA nae nimtani wangu hahahahaa! leo nimekupata mbona umesahau kale ka mboga kanakoitwa mkunungu? au kwakuwa wewe hujakulia huko?kwetu tunaita nswalu,hii nikama anayosema Koero ni mlenda uliosagwa kama hina au unga,ikipikwa ni lazima ichanganywe na karanga zilizosagwa!mmmh! mate yamenijaa mdomoni,bibi yangu alikuwa anajua kuipika hiyo utakula ugali hata kama ulikuwa huna njaa.
ReplyDeleteYasinta umenifanya nimkumbuke bibi Mbipa leo R.I.P bibi.
Chib huyo samaki labda awe furu, nembe au gogogo akiwa sato au sangara sijui inakuwaje?
ReplyDeleteEdina leo umenikumbusha rafiki yangu wa ki vietnam, sasa hivi yuko kwao, unajua sisi huku lunch time kila mtu huwa anakuja na chakula chake, kabla ya kula kila mtu anatest chakula cha mwenzie lakini kabla ya kutest anaelezea chakula chake kimepikwa na nini, basi yeye utamsikia Maria leo nina au au ua yaani siku hiyo ujue ni mbwa na akisema Maria leo miyao miyao siku hiyo ujue ni paka, basi hakuna kilicho niacha hoi kama siku ya birthday yake, wakati wa champagne nikaona analetwa nyoka mzima ilipo funguliwa champagne na nyoka akachinjwa sasa basi kila anae miminiwa champagne anamiminiwa na damu ya nyoka kwenye champagne yake nikaona wanakuja na kwangu wanitilie damu ya nyoka, nikawaambia nyie msinitanie walinicheka sana na kuniona mshamba sana, yaani ukienda kwenye super maket yao kila kitu kipo yaani chura, nyoka panya wote wapo kwenye freezer
ReplyDeleteHahaaaa Mumyhery usinichekeshe usikute walisha kulisha kanyoka we hujui Tu...PASSION4FASION.TZ nafurahi kwa kuwa list ya watani zangu inazidi kuongezeka...akiwemo dada Yasinta wa kuleeee!! bombi mbili kwa Mfaranyati....
ReplyDeletehaha hahahahaha!! ni kweli kabisa hapa tumepata kuwajua baadhi ya watani weyu. Dada Mariamu hiyo kali ya kuwekewa damu ya nyoka kwenye kinywaji DUH!! Edna unogage be we mlongo! Nimependa msemo huu nanukuu "akiwemo dada Yasinta wa kuleeee!! bombi mbili kwa Mfaranyati...."mwisho wa kunukuu. mpaka mbavu sina maana nimekumbuka wale ndugu zangu wandendeule wasemapo nishikie gari nipande nyengooooooo:-)
ReplyDeleteWahaya je?
ReplyDelete