Friday, January 22, 2010

MZIKI NI MOJA YA MAISHA YETU LEO NGOJA TUMSIKILIZE DADA HUYO SOPHIA GEORGE!!



Mwaka ulikuwa 1992 kulikuwa na sherehe, katika ukumbi wa sherehe Wilima sec.school. EEhhh!! bwana we wacha watu wajimwage kwa mziki wa dada huyu. Kwa hiyo leo nimekumbumbuka sana Wilima-Matetereka na hasa siku ile. Ebu sikilizeni nawatakieni usikilizaji mwema na pia ikibidi uchezaji mwema. Muwe na wakati mzuri wa mwisho wa juma hili. Nataka kusema tuanza mwisho wa juma na muziki. TUTAONANA WAKATI MWINGINE!!!

7 comments:

  1. Ilikuwa ni Graduation au? Umenikumbusha Nganza wakati wa disko tulivyokuwa tukilisakata na wana Nsumba au Bwiru boys.

    ReplyDelete
  2. hii nzuri hii dada subi upo tumepotezana online!

    ReplyDelete
  3. Je nitachezaje wakati HAITI watu wanakufa?Je nitasikilizaje muziki wakati watu wanakufa?

    Je ni haki watoto wanalia huku sisi twasikiliza muziki na kucheza?

    Binadamu?

    ReplyDelete
  4. Muziki Kibonge sana Huu na si siri unanikumbusha mbali.

    @Nyabingi Worror: Kila siku ya Mungu kuna watu wanakufa. Na kama kuna Mungu na kaamua watu tufe kwa hiyo kufa pamoja na masikitiko yote tutakayo kuwa nayo bado ni kitu ambacho lazima kitokee. Let the living live because waishio nyimbo ni nyimbo na hata Msibani , Matatizoni, mpaka shereheni wataimba na kucheza. Kumbuka mila zinatofautiana na watu ni tofauti ndio maana utasikia kuna disco msibani kwa wajaluo au kuna watani tu ndani ya kabila jingine ambao kwenye huzuni kazi yao ni kuja Kucheka.

    Wote tuna matatizo kwahiyo usione watu wanacheka na kuimba ukadhani wanadharau wenye huzuni na kulia.


    Ni hilo tu.

    ReplyDelete
  5. Ya kale ni dhahabu, ukiwemo wimbo huu

    ReplyDelete
  6. nyabhingi shangilia! watu wakifa haimaanishi tuwe na huzuni muda wote let us help them while celebrating!. Nyabhingi shangilia!

    ReplyDelete
  7. D Mija! ni kweli ilikuwa Graduation nashukuru kama nimekukumbusha ya kale.

    Tandasi! ni kweli Da Subi sijui yu wapi?

    Nyahbing! kuna miziki mingine ni ya huzuni basi watu wanaweza kusikiliza wakiwa na huzuni. Pia naona MT. Simn katoa maelezo hapo chini Shukrani.

    Mt. Simon nashukuru kama unaona ni mziki kibonge na umekukumbusha mbali.Ndio ilikuwa nia kukumbuka ya kale.

    Kaka Bennet ni kweli ya kale ni dhahabu. Ahsante kwa kuipenda wimbo huu.

    Kaka Tandasi! Hapo umesema nilikuwa natafuta maneno hayo ahasante sana.

    ReplyDelete