Nina rafiki mmoja anazungumzia kuhusu maisha ya ndoa ya Afrika na kila anapojaribu kuwaelezea watu kuwa. Sisi waafrika tunapokaribia umri wa kuoa kitu cha kwanza ni kutafuta mchumba na ukishampata zinaanza shughuli za kupanga mahali. Lakini wao wanashangaa sana hata hawaelewi kabisa kwa nini tunatoa MAHALI. Wao wanadai ya kwamba tunauza, kama kuku. Yaani mzazi wa msichana anamuuza binti yake. Wanasema kama tunatoa mahali kwa kuwashukuru wazazi wa upande wa kike je kwa nini na wazazi wa upande wa kiume wasipongezwe kwa kazi nzuri ya kumtunza kijana wao. hata kama ukiwaambia ni njia ya kuonysha respect pia. Ndugu wasomaji kusema kweli sisi wanadamu tunaishi katika mila na desturi tofauti kabisa. Kwani hapa wao hili jambo la ndoa halihusishwi kabisa kwa wazazi. Ni baina ya kijana na msichana. wanaelewana wao wawili tu kama kufunga ndoa au kuishi hivihivi. Sasa hapa bado sijaelewa sawasawa kama hii ni sababu ndoa zao hapa hazidumu muda mrefu. Haya wasomaji je kuna maelezo zaidi ya kuwaeleza watu hawa. MCHANGO basi.
Na; Yasinta Ngonyani
Sunday, April 20, 2008
Tuesday, April 15, 2008
Aprili,15,2008 ughaibuni baada ya miaka 14
Gendayi ulolayi=Tembea uone.
Kuna watu wa kila wa kila aina duniani hap. Walio na roho nzuri na walio na roho mbaya, wengine wana huruma na wengine wema. Kwa mara ya kwanza nilipofika hapa sikugundua, lakini sasa nimeishi hapa miaka kama kumi na nne kwa kweli afadhali ya kuwa mwafrika na kuishi afrika. Nikisema hivi nina maana huku watu wana ubinafsi sana kila mtu na mke na watoto/mtoto wake. Ukoo mwingine hawahesabiki, sio kama sisi waafrika tupo pamoja, ukoo mzima tunasaidiana na kushirikiana. kama umesoma (MAMA,BABA NA WATOTO UTANIELEWA.) Sisemi mila ipi ni nzuri au ipi mbaya. Ila tu kwa mimi ni ajabu sana kuona watu hawatembeleani yaani wanaukoo. Unajua kama unatoka kwenye familia kubwa ni vigumu kuona hata kama watu wapo watatu wanashindwa kutakiana hali. Pia kama nilivyoseam huku watoto wakisha kuwa watu wazima basi kila mtu ajijue mwenyewe. Sio kama sisi kusaidiana, kutunzana hiyo hapa hakuna. Bado sijaelewa kwa nini mungu alituumba tofauti. Je huu ni upendo? Nina maana kila nikiwaza na kufikiri sipati jibu, kwa nini inakuwa hivi. Bado sijagundua, hili jambo linanipa shida sana kuelewa pia linanipa uchungu sana kuona watu wanaweza kuwa na roho kama hii. Kwani kwa akili yangu nilidhani sisi wanadamu wote tulikuwa na roho moja.
Na: Yasinta Ngonyani

Sunday, April 13, 2008
aprili,13,2008 maisha ni nini?
Kwa akili yangu bado sijaelewa maisha ni nini? au niseme maisha ni kitendawili, ni safari ndefu na fumbo. Hakuna ajuaye kwa nini amezaliwa. Mhh nina maana watu kwanza tunazaliwa tunaishi na mwisho tunakufa. Hii bado sijaelewa kwa nini na inaleta maana gani. Na pia kingine kwa nini wengine wanaishi mwaka mmoja na wengine thelathini na kidogo na hapohapo wengine wanaishi miaka hata miamoja na kidogo. Ni juzi tu nilialikwa kwenye sherehe mzee mmoja ametimiza miaka tisini. Binafsi nisingependa kuishi miaka tisini. Je kuna mmoja anaweza kuniambia maisha ni nini
Monday, April 7, 2008
Aprili 7,2008 mama
Nimekaa na kufikiria fadhila zako wewe. Nasema mama,Ukizingatia na wema wako kwa kunizaa na kunilea mimi mwanao. Wewe mama yangu cha kukulipa sina. Mama nakuombea tu mola akulaze pema, mola ndiye muweza. Nakupenda mama yangu. Zile siku za utotoni nazikumbuka mama, mapenzi yako ya moyoni uliyonipa mama hata sijui nikupe nini kwani umeshaondoka ewe mama. Naukuombea mola akulaze pema. Nakupenda mama yangu wewe ewe mama nakupenda mama yangu. Kifo chako kwangu moyoni chaniumiza najua ni kazi ya mungu.Hata sijui nifanye nini, mimi nakuwaza wewe nami bado nipo safarini najiliwaza wewe nakuombe dua. Ewe mama mola akulaze pema, ewe mama yangu. Mama yangu wewe, nakupenda mama yangu, nakupenda mama yangu. WOTE AMBAO HAWAJAWAAMBIA WAZAZI WAO USO KWA USO KUWA WANAWAPENDA. nAWAOMBENI CHUKUKUENI NAFASI SASA NA KUSEMA HILI NENO NAKUPENDA MAMA AU BABA. Binafsi nimechelewa kumwambia mama yangu.
Na: Yasinta Ngonyani
Na: Yasinta Ngonyani
Saturday, April 5, 2008
rais/kura na uchaguzi Aprili 5,2008
Nimechoka kila siku, kila wakati kusikia viongozi wa Afrika wanaongoza nchi lakini hakuna kinachoendelea. Ninachotaka kusema ni kwamba ningependa kwenda au kutembelea katika miji wanayotoka na kuona maendeleo ya vijiji vyao. Kwani kwa mimi naona kama wao wanaongoza nchi lakini hakuna maendeleo Je? sio jukumu lao kuongoza nchi ile ambayo wanaongoza ili iendelee? Kwa mfano sasa Zimbabwe, bado sijaelewa kwa nini miaka yote hii Rais Mugabe amekuwa rais. Badala ya nchi kuendele imekuwa kinyume imerudi nyuma. Kwani kama nakumbuka vizuri Zimbabwe ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kwa maendeleo lakini sasa imekuaje?. Na sasa Rais Mugabe kwa kusema kweli inabidi awaachie vijana nao watawale nchi kwani yeye ametawala na inatosha kwani hakuna maendeleo. Kwani ni mzee kutosha miaka 84 sio mchezo waachie vijana labda tutaona maendeleo. Si jambo la aibu kuacha kuongoza nchi, ndiyo rais Mugabe anaipenda nchi yake lakini kuongoza nchi miaka 28 na kinachoendendelea hakionekani hakuna sababu ya kuongoza nchi, awaachie wengine (vijana wenye mawazo tofauti na hamu ya kuongoza nchi)
Na; Yasinta Ngonyani
Na; Yasinta Ngonyani