Nimekaa na kufikiria fadhila zako wewe. Nasema mama,Ukizingatia na wema wako kwa kunizaa na kunilea mimi mwanao. Wewe mama yangu cha kukulipa sina. Mama nakuombea tu mola akulaze pema, mola ndiye muweza. Nakupenda mama yangu. Zile siku za utotoni nazikumbuka mama, mapenzi yako ya moyoni uliyonipa mama hata sijui nikupe nini kwani umeshaondoka ewe mama. Naukuombea mola akulaze pema. Nakupenda mama yangu wewe ewe mama nakupenda mama yangu. Kifo chako kwangu moyoni chaniumiza najua ni kazi ya mungu.Hata sijui nifanye nini, mimi nakuwaza wewe nami bado nipo safarini najiliwaza wewe nakuombe dua. Ewe mama mola akulaze pema, ewe mama yangu. Mama yangu wewe, nakupenda mama yangu, nakupenda mama yangu. WOTE AMBAO HAWAJAWAAMBIA WAZAZI WAO USO KWA USO KUWA WANAWAPENDA. nAWAOMBENI CHUKUKUENI NAFASI SASA NA KUSEMA HILI NENO NAKUPENDA MAMA AU BABA. Binafsi nimechelewa kumwambia mama yangu.
Na: Yasinta Ngonyani
haya tutafanya hivyo maana naona unatusuta akina markus mmh.tutawaeleza hayo bila kukosa
ReplyDelete