Sunday, April 13, 2008

aprili,13,2008 maisha ni nini?

Kwa akili yangu bado sijaelewa maisha ni nini? au niseme maisha ni kitendawili, ni safari ndefu na fumbo. Hakuna ajuaye kwa nini amezaliwa. Mhh nina maana watu kwanza tunazaliwa tunaishi na mwisho tunakufa. Hii bado sijaelewa kwa nini na inaleta maana gani. Na pia kingine kwa nini wengine wanaishi mwaka mmoja na wengine thelathini na kidogo na hapohapo wengine wanaishi miaka hata miamoja na kidogo. Ni juzi tu nilialikwa kwenye sherehe mzee mmoja ametimiza miaka tisini. Binafsi nisingependa kuishi miaka tisini. Je kuna mmoja anaweza kuniambia maisha ni nini

No comments:

Post a Comment