Gendayi ulolayi=Tembea uone.
Kuna watu wa kila wa kila aina duniani hap. Walio na roho nzuri na walio na roho mbaya, wengine wana huruma na wengine wema. Kwa mara ya kwanza nilipofika hapa sikugundua, lakini sasa nimeishi hapa miaka kama kumi na nne kwa kweli afadhali ya kuwa mwafrika na kuishi afrika. Nikisema hivi nina maana huku watu wana ubinafsi sana kila mtu na mke na watoto/mtoto wake. Ukoo mwingine hawahesabiki, sio kama sisi waafrika tupo pamoja, ukoo mzima tunasaidiana na kushirikiana. kama umesoma (MAMA,BABA NA WATOTO UTANIELEWA.) Sisemi mila ipi ni nzuri au ipi mbaya. Ila tu kwa mimi ni ajabu sana kuona watu hawatembeleani yaani wanaukoo. Unajua kama unatoka kwenye familia kubwa ni vigumu kuona hata kama watu wapo watatu wanashindwa kutakiana hali. Pia kama nilivyoseam huku watoto wakisha kuwa watu wazima basi kila mtu ajijue mwenyewe. Sio kama sisi kusaidiana, kutunzana hiyo hapa hakuna. Bado sijaelewa kwa nini mungu alituumba tofauti. Je huu ni upendo? Nina maana kila nikiwaza na kufikiri sipati jibu, kwa nini inakuwa hivi. Bado sijagundua, hili jambo linanipa shida sana kuelewa pia linanipa uchungu sana kuona watu wanaweza kuwa na roho kama hii. Kwani kwa akili yangu nilidhani sisi wanadamu wote tulikuwa na roho moja.
Na: Yasinta Ngonyani
Hii habari umenikuna sana yaani nimejikuta natabasamu huku nikikumbuka wazungu wa aina mbalimbali hapa ulimwenguni.Yaani imechachcfya sana kwani ni hali ambayo kuna mama mmoja hivi ana uraia wa Ghana sasa yeye hataki kusikia kuhusu nchi yake ya kuzaliwa uingereza kwani anadai maisha wanayoishi wazungu wenzake siyo maisha sahihi hivyo yeye aanaona fahari kujiita mwafika.Hivi hii blogu yako Ndesanjo ameiona kweli.Huyu ni mwalimu wangu wa kublogu kwani naona kuna mambo muhimu lazima atakubaliana nami kwamba hii ni blogu ya kipekee yenye muunganiko wa ughaibuni na afrika yetu.
ReplyDeletemtembelee hapa
www.jikomboe.com