Nimechoka kila siku, kila wakati kusikia viongozi wa Afrika wanaongoza nchi lakini hakuna kinachoendelea. Ninachotaka kusema ni kwamba ningependa kwenda au kutembelea katika miji wanayotoka na kuona maendeleo ya vijiji vyao. Kwani kwa mimi naona kama wao wanaongoza nchi lakini hakuna maendeleo Je? sio jukumu lao kuongoza nchi ile ambayo wanaongoza ili iendelee? Kwa mfano sasa Zimbabwe, bado sijaelewa kwa nini miaka yote hii Rais Mugabe amekuwa rais. Badala ya nchi kuendele imekuwa kinyume imerudi nyuma. Kwani kama nakumbuka vizuri Zimbabwe ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kwa maendeleo lakini sasa imekuaje?. Na sasa Rais Mugabe kwa kusema kweli inabidi awaachie vijana nao watawale nchi kwani yeye ametawala na inatosha kwani hakuna maendeleo. Kwani ni mzee kutosha miaka 84 sio mchezo waachie vijana labda tutaona maendeleo. Si jambo la aibu kuacha kuongoza nchi, ndiyo rais Mugabe anaipenda nchi yake lakini kuongoza nchi miaka 28 na kinachoendendelea hakionekani hakuna sababu ya kuongoza nchi, awaachie wengine (vijana wenye mawazo tofauti na hamu ya kuongoza nchi)
Na; Yasinta Ngonyani
TUNAHITAJI KUANZA UPYA WAAFRIKA
ReplyDeleteHapana nadhani sababu kubwa ya mzee Mugabe kugombea tena ni kuwaonyesha akina Bush na Blair kwamba siyo matakwa yao ndiyo yanayowafanya wananchi kuwaacha viongozi fulani,hata hivyo nina mashaka katika nafsi ya Morgan kama kweli ni mtu anayewafaa wazimbabwe kutokana na mambo yanavyokwenda kati yake na kina Gordon Brown.Kuporomoka kwa kiwango cha maisha ya wazimbabwe ni propaganda za kina Bush na wenzake kwani mara nyingi wamekuwa wakipanga namna ya kutawala wanavyotaka wao na iwapo wakipingwa basi hutumia mbinu zao za utajiri kuwaangamiza kwa kuwamkomoa wale wanao wapinga.
Mfano katika suala hili liliobatizwa ugaidi wakati mwingine tunaona wazi kwamba wale wasiokuwa upande wa marekani basi huitwa mhimili wa uovu au maneno makali kama wahalifu na magaidi n.k lakini ukitazama maisha ya watu wazimbabwe sasa zote hizo ni njma zilizopangiliwa toka tu Mugabe aamue kutekeleza makaubaliano yale ya mwaka 1980 kuhusu ardhi kwani makubaliano yale na La Smith ilikuwa lazima raia hao wa uingereza waondoke katika ardhi ile na kuwaachia wazimbabwe lakini mwaka 1999 Mugabe alipokumbusha hili akapuuzwa na kutukanwa sana na kina Margret Thatcher akiwa waziri mkuu.Sasa mara baada ya kuona kwamba mzee huyu sasa kaamua kufanya kweli kwa kuwapinga basi wanaanza kutengeneza njama za kuporomosha thamani ya hela ya nchi na kufanya hujuma za kiuchumi kupitia mashirika yao kama IMF na WB.kwa kuyatazama mashirika hayo tu unaweza kujua kwamba siyo mashirika ya kidunia bali ya Marekani na washirika wa ulaya.Mfano kwanini Chavez rais wa Venezuela anaonekana mbaya kwao?ukitazama utaona huyu analilia haki iliyoporwa kwani hawa jamaa wanafanya mambo wanayoyataka wao.vivyo hivyo Chavez alilipa madeni yote ya IMF na WB mpaka kufikia mwaka 2001 hivyo wakaamua kufunga ofisi za mashirika hayo na kuanza hujuma ambazo Chavez kafanikiwa kuzimudu lakini kwa mugabe imekuwa taabu.Hujuma hizi zinafanywa kwa kuutangazia ulimwengu mugabe aonekane mbaya na sisi waafrika tunakulaina na hili kwa kusikiliza hadaa na ghiliba za wachambuzi wanaoonekana katika CNN,BBC,SKY NEWS,FOX NEWS CBS,ABC,APF,REUTERS n.k Lakini kwa vyovyote kina Bush wanalazimisha mengi yafanye kama wanavyotaka wao lakini ukifanya kinyume au kupingana nao basi njama zinakujongea.Mimi sitaki kuona hawa jamaa wanamtimua madarakani mugabe bali wananchi kama kweli wanaona hawamhitaji basi wamtoe kwa kura hilo linawezekana iwapo tu watatumia kura zao kwa umakini kama inavyoendelea sasa.Na hilo siyo pekee tazama huko DRC-ZAIRE kuna jenerali Nkunda anaitwa ameasi,lakini ni kweli ameasi.Ukichunguza hadi sasa unaona mikono ya marekani na wenzake wafaransa wanasaka madini pale,wanamsaidia kwa hali na mali ili kupata wanachokitaka halafu wanatudanganya wanamsaidia ndugu Joseph Kabila,huu ni uhuni kabisa.Kinachofanyika zimbabwe ni hujuma zile tunazoziita kwamba unajifanya mjanja siyo?tutakuonyesha.hayo ndiyo wanayomwoshesha sasa na kuharibu maisha ya raia na kupandikiza chuki dhidi ya mugabe.sasa tatizo linakuwa kwamba wachambuzi wengi wa vyombo vya habari vya magharibi wanashindwa kubaini tofauti ya 'kutaka' na 'kupenda',siyo wote wanachama wa ZANU-PF wanamtaka mugabe au siyo wote wanaoshabikia chama hicho wanamhitaji mzee huyo bali wengine huamua kumsapoti tokana na kubaini yale yanayofanywa na kina Bush na wenzake.Leo mgogoro ya Darfur tunadanganywa kwamba sisi waafrika tunapenda vita lakini ukitafiti unakuta China ndiyo inayouza silaha ili kuendeleza mapambano pale na akina George Bush wanajifanya kutatua kumbe vita yao ni dhidi ya China hivyo wanapenda mtu anayetawala Khartoum akubaliane nao ili waendeleze vita.
Watu kama hawamtaki mugabe wamwache wampigie kura Morgan au Makoni lakini siyo kina Bush ndiyo waamue..hilo hapana.tazama kule Comoro wafaransa wanamsaidia dikteta Bacar,wakati sisi waafrika tukihangaika kuweka mambo sawa wao wanamlea wamatunza kama yai.
siyo siri tunahitaji kuanza upya
kama nilivyoandika awali hapo,kwani nimetumia anonymous baada ya kunisumbua namna ya kuingia katika maoni.hawa kina Bush wanatuharibu kwa mengi sana hivyo suala la mugabe nalo waliliandaa kuonekana kifujofujo tu hata uchanguzi wenyewe watasema ni fujo siyo wa haki iwapo mugabe atashinda.Iran wabunge wengi wa chama cha kina Ahamednejad kiliposhinda tukasikia kwamba waangalizi toka umoja wa ulaya wakisema siyo uchaguzi huru na wa haki.Wakati kipindi cha mjadala kikiendelea katika Tv ya SKY NEWS walishupalia hili jambo nikatuma maoni kwa barua pepe hivi nyinyi wa ulaya uchaguzi huru na wa haki ni mpaka pale wanaposhinda wagombea mnaowataka? dakika chache nikarudi katika chuma Tv nikaona mjadala ukiendelea huku wakijadili maoni hayo lakini hakuna aliyetoa jawabu sahihi hivyo nikauliza siku nyingine je wanaifahamu misingi ya uchaguzi huru na wa haki au wanazungumza tu bila kuelewa? na safari hii nikajitambulisha nilipo,wakaanza kujadili matatizo ya afrika,nikauliza kwanini mnakwepa hoja? hivi wakati wa Primitive accumulation of capital hapakuwa na matatizo kama haya ya afrika?wakanyamaza tena na kujadili namna nchi zinavyo haribu demokrasia,hapa ndipo nikaona wanakoroga nikauliza Chavez hastahili demokrasia? au demokrasia wanayo akina Bush kuua watoto wa pale Fallujah Irak?,nikauliza nini maana ya demokrasia?mantiki yake ni ipi?ndipo nikaona kipindi kikiendelea mwishowe nikaona hawa katika vyombo vya habari kama hivyo ni vya uwongo na porojo siyo siri dada ilinichosha nikaona hawajui mambo yenyewe wanazungumza bila kuyapitia katika maisha halisi.nikaachana nao.CNN ndiyo usiseme afadhali ya mzee Lary King anazungumza vitu vinavyoeleweka hafichi lakini hawa wanasababisha matatizo kwetu tukiwauliza wanajifanya kutubwagia mizigo wenyewe sawa,ipo siku labda tutaelewa vyema kwani wanadhani hatuelewi.
ReplyDeletemarkus/karibu nyasa
Nimerudi baada ya kusumbuka kidogo namana ya kuingi katika maoni yangu ya kila siku ndiyo maana nimetumia anaonymous,usijali.Suala hili limenikuna sana mstari kwa mstari kwani naamini kuna tatizo katika tawala zetu na hawa jamaa zetu wa ughaibuni.kuna uharamia mwingi wanaufanya kwa kisingizio waafrika tunapenda ugomvi au vita aua tuna njaa na utapimlo kila mahali lakini hawajiulizi kwani tupo hivi.Lakini nakuliana nawe kwamba mugabe anatakiwa kuondoka.Pia nikukumbusha Paul Biya wa Kameruni naye kaongeza miaka ya utawala lakini kweli hawa wa ughaibuni wanataka kutusaidia basi wasitoe condition kama wanavyofanya katika mashiri yao,ndiyo maana mimi siamani kama hayo ni mashirika ya dunia bali ni m,binu za unyonyaji n.k
ReplyDeletengoja nkomee hapa usije ukadhini Nihyomiti lepi dada imenivutia sana