Nimeona tuumalize mwezi kwa picha hii ya nyumbu. Nawatakieni wote mwisho mwema wa mwizi na pia mwanzo mwema wa mwezi wa tatu/machi. wenu Kapulya!
Tuesday, February 28, 2017
Monday, February 27, 2017
MALEZI:- WAACHE WATOTO WAWE WATOTO
Katika jamii yetu wengi wanadharu sana micezo ya watoto. Wanaona ni kupoteza mida tu lakini tukumbuka kwamba michezo yote wafanyayo watoto inachangia sana ukomavu wa ubongo wao maana pale hawachezi tu wanajifunza kitu pia. Kwa mfano katika michezo mingi ya watoto kuna kuhesabu kwingi sana, hapa tayari anajifunza kitu...tuwape nafasi watoto kuwa watoto na pia kama wazazi tujaribu kuwa pamoja nao na kushiriki baadhi ya michezo.
CHUKUA DAKIKA TU ANGALIA HII VIDEO HAPA CHINI ......
UJUMBE:- WAZAZI/WALEZI WATOTO WETU WANATUHITAJI SANA TUTENGE MUDA KWA AJILI YAO. TUSIWASAHAU NI JUKUMU LETU.
CHUKUA DAKIKA TU ANGALIA HII VIDEO HAPA CHINI ......
UJUMBE:- WAZAZI/WALEZI WATOTO WETU WANATUHITAJI SANA TUTENGE MUDA KWA AJILI YAO. TUSIWASAHAU NI JUKUMU LETU.
Thursday, February 23, 2017
KUMBUKUMBU:- BLOGG YA MAISHA NA MAFANIKIO LEO YAFIKISHA MIAKA TISA (9) YA KUBLOGG...!!
Napenda kuwashukuruni wasomaji wangu wa blogg ya Maisha na Mafaniko kwa kuwa nami bega kwa bega kuendesha libeneka hili. Nina uhakika bila ninyi nisingekuwa hapa leo...pia napenda kuishukuru familia yangu, kwani kublogg yataka moyo. Basi tuunganee pamoja kwa siku hii ya leo kwa kuisherekea BLOGG YETU YA MAISHA NA MAFANIKIO KWA KUTIMIZA MIAKATISA (9) YA KUBLOGG.
Wednesday, February 22, 2017
MAISHA:- KUTOKANA NA TABIA ZAKO UKIWA NA SHIDA UNAWEZA UKAACHWA BILA KUSAIDIWA
Katika maisha unaweza kufikwa na MATATIZO na watu wakatamani kukusaidia lakini wakashindwa kutokana na TABIA zako..
UJUMBE:- CHUNGA SANA ALIYE KUUMBA ANA UWEZO WA KUKUUMBUA.
UJUMBE:- CHUNGA SANA ALIYE KUUMBA ANA UWEZO WA KUKUUMBUA.
Tuesday, February 21, 2017
UJUMBE KUTOKA KWANGU KUJA KWENU
Kabla hujadhani, jifunze ukweli kwanza.
Kabla hujahukumu , elewa kwanza ni kwanini.
Kabla hujamuumiza mtu, hisi kwanza. Na
Kabla hujazungumza/sema, fikiri kwanza
NAWATAKIENI WOTE SIKU NJEMA NA KILA MUFANYALO LIWE JEMA!
Friday, February 17, 2017
TUMALIZE WIKI HII KWA HII:- ENZI HIZOOO
AU TU TUMSIKILIZE NA PWANGUZI NA PWANGUZI
Nakumbuka hiki kipindi kilikuwa hakinipiti kabisa...Je? ww wenzangu unakumbuka? TUSISAHAU KUWASIMULIA VIZAZI VYETU AU TU KUSIKILIZA PAMOJA:-) IJUMAA NJEMA!
Thursday, February 16, 2017
Monday, February 13, 2017
JUMATATU HII IANZE HIVI:- JIKONI LEO UGALI
Ugali, mchanganyiko wa maharege na viazi pia matembele
...na hapa ni ugali na mboga iliyoungwa karanga...
Binafsi nachagua ule mlo wa kwanza maharage na matembele kwa vile SIPENDI KABISA MBOGA au CHAKULA CHOCHOTE KILICHOWEKWA KARANGA....Ndiyo maana nimeandaa aina mbili isije nikashinda njaa:-)
Sunday, February 12, 2017
UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI....JUMAPILI NJEMA!
Kweli hapa kuna haja ya kuwita baba maana hakuna jinsi. NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI YENYE AMANI NA FURAHA.
Saturday, February 11, 2017
SIKU MBAYA (Jifunze kupitia simulizi hii)
Nimeamka asubuhi hii na kukutana na simulizi hii katika barua pepe yangu. Baada ya kusoma nikaona ni simulinzi nzuri na ya kufundisha katika maisha ya kila mwanajamii. Kwa hiyo nikaona niiweke hapa kibarazani kwetu ili kwani elimu hawanyimani...karibuni
Kijana akiwa katika maombi
Ilikuwa ni saa moja na nusu saa za asubuhi ambapo kijana aitwae John alikuwa ndo anaamka.
Mara baada ya kuamka na kukamilisha ratiba yake ya asubuhi ikiwemo kuoga, kupiga mswaki na kupata kifungua kinywa kijana alienda alipopaki gari yake tayali kwaajili ya kuelekea ofisini. Ile anataka kuwasha gari yake ghafla engine ikagoma kuwaka. Akashuka kwenye gari yake na kuamua ketembea kwa miguu mpaka kituo cha mabasi. Hata hivyo baada ya kufika kituo cha mabasi hakufanikiwa kupanda basi kwa kuwa mabasi yote yalikuwa yamejaa.
Ili asichelewe kazini kijana akaamua kukodi tax. Akiwa ndani ya tax alipigiwa simu na mmoja kati ya washirika wake kibiashara lakini kabla hajapokea simu ikazimika na hata alipojaribu kuiwasha akagundua betri ilikuwa imekufa. Akiwa bado yupo ndani ya tax mwendo kidogo baadae tax nayo ikazimika ghafla na haikuweza kuendelea na safari. Akamlipa dereva tax pesa yake na kuamua kukodi tena pikipiki (bodaboda) ambayo ilimfikisha mpaka kazini kwake.
Kabla hajaingia ofisini kwake mtu mmoja akataka kumshika mkono na kumpongeza kwa promotion ambayo ilitakiwa kufanyika siku hiyo.
Lakn kabla hajafanya hivyo akaitwa na mtu kwa nyuma ambaye baadae akamwambia kwamba promotion ilikuwa imeahilishwa.
Jioni baada ya kufika nyumbani kijana akaanza kunung'unika huku akisema:
"mambo gani haya!!!"
"kwanini leo imekuwa SIKU MBAYA kwangu kiasi hiki!!"
"Ee Mngu nimekukosea nini mimi mpaka siku yangu iwe mbaya kiasi hiki!!"
Mara ghafla akasikia sauti ya Mumgu ikisema:
"Asubuhi ulipowasha gari yako ikagoma kuwaka mm nilihusika kwa sababu ungepata ajali mbaya sana kama ungetoka na gari yako leo"
Ulipotaka kupokea simu betri ikafa mm nilihusika kwa sababu aliyekupigia simu alitaka kukupatia taarifa za uongo ambazo zingepelekea kuharibu uhusiano kati yako na wafanyabiashara wengine.
Hatua chache baadae tax ilishindwa kuendelea na safari kwa sababu yule dereva tax ni agent wa kikundi cha wateka nyara hivyo kama mngeenda mbele zaid huko angebadili mwelekeo na kukupeleka chini ya jengo moja kubwa ambalo limekuwa likitumika kwa shughuli zao za uharifu na hatimae wangekuteka.
Ulipofika ofisini nilizuia mtu mmoja asikushike mkono kwa sababu nilikuwa nakuepusha na maambukizi ya ebora kwani yule mtu amesha ambukizwa vurusi vya ugonjwa huo
Baadae kidogo ile promotion ambayo ulitegemea ikuingizie pesa nyingi sana ukaambiwa imeahilishwa hapo napo mimi nilihusika kwa sababu kuna mtu hakufurahia ww kupata nafasi ile hivyo akaamua kupandikiza mapepo kwenye kiti ulichotakiwa kukalia ndani ya ukumbi ambapo mapepo hayo yangepelekea kifo chako.
Sasa hebu niambie
-Siku ya leo ilikuwa mbaya kwako
-Na je yote niliyokutendea yalikuwa mabaya?Kijana kusikia hivyo alilia sana,akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung'unikia Mungu. Akapiga magoti akatubu, hukuakimshukuru Mungu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ninachotaka hapa uelewe ni kwamba upo hai leo ni kwa sababu Mungu amependa uwe hai na ana makusudi na maisha yako.
Wakati mwingine kuna mambo mabaya huwa yanatokea katika maisha yetu yanayotufanya tuone kama Mungu ametusahau.
Tunamnung'unikia na kumlaumu Mungu bila kujua kuwa Mungu ana njia nyingi sana za kutuepusha na mabaya.
Wakat mwingine tunasahau kuwa mabaya tunayokutana nayo yanafanya kazi kwa Manufaa ya hatma zetu.
Unaweza fukuzwa kazi usijue kumbe ndio unaelekea katika kazi bora zaidi,
Unaweza kuachwa na mtu uliyempenda sana ukadhani ndiyo mwisho wa maisha kumbe Mungu amekuandalia mtu mwingine mwenye mapenzi ya dhati mtakayefikia malengo ya kujenga familia,
Unaweza kukataliwa na kutengwa na ndugu kumbe Mungu amekuandalia watu-baki watakaofanikisha ufikie malengo yako pasipo masimango ya ndugu,
Unaweza kuona marafiki wanakusariti kumbe Mungu anawaondoa makusudi ili kukuepusha na mabaya waliyoyapanga juu yako.
MWISHO naomba nikuhakikishie kwamba Mungu anayaona matatizo yako na kwa hakika hatoacha yakuangamize bali atakwenda kufanya njia ya kutokea ktk magumu yote unayopitia.
Kama unaamini kwanini usiseme AMEN.
Thursday, February 9, 2017
BLOGG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA HII PICHA KUWA PICHA YA WIKI....
Hakuna kupoteza muda hapa...nimeipenda hii safi sana UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU....AU MNABISHA?
Tuesday, February 7, 2017
Monday, February 6, 2017
LEO NIMEYAKUMBUKA MATUNDA HAYA ADIMU MATUNDA DAMU/TAMARILLO
Mti wa matunda damu/tamarillo ukichanua
Hapa tayari yameiva
Mavuno tayari.
Kama nilivyosema kwenye kichwa cha hapo juu haya matunda ni adimu na pia ukiyapata ni ghali sana..Inabidi nianze kulima .... JUMATATU/MWANZO MWEMA WA WIKI !!
Sunday, February 5, 2017
VAZI LA JUMAPILI YA LEO KITENGE CHENYE ASILI YA TANZANIA....JUMAPILI NJEMA
MDADA LEO KATOKA KITANZANIA HASWA...ANGALIA KITENGE
Kwa mbali anaonekana kuchoka choka lakini ...ni vazi la jumapili ya leo kitenge chenye maandishi ka nitokako TANZANIA.JUMAPILI NJEMA KWA WOTE WATAKAOPITA HAPA NA PIA JIONI/MCHANA NA USIKU MWEMA KWA WOTE.