Ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'
1. Chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati.
2. Chunguza kwa mwenzio juu ya tabia kama:- nidhamu, adabu, hasira, ulevi na uzinzi.
3. Mpeane muda wa kutosha kufahamiana.
4. Mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, mgahawani na sehemu mbalimbali ili muone kila mmoja anapenda nini.
5. Muwe wa imani moja, ila kama mmeendana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa.
6. Wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzi wako yukoje.
7. Pimeni afya zenu bila aibu, kuna maradhi mengi kama vile HIV/AIDS na mengine.
8. Kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.
9.Kwa Wakristo ndoa haina talaka, huu ni mpango wa Mungu. Kuachana na kuoa mwingine ni dhambi.
N.B: kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukitegemea atabadilika/abadilike wakati mkiwa wachumba na siyo kwenye ndoa, labda kama umeshamkubali kama alivyo.
NAWATAKIENI WOTE JUMATATU HII YA MWISHOYA MWEZI HUU WA TANO IWE NJEMA SANA. TUPO PAMOJA DAIMA!
ReplyDeleteVIJANA HUULIZA
Je, Niko Tayari Kufunga Ndoa?
Ili uweze kujibu swali hilo, unahitaji kujielewa vizuri. Kwa mfano, fikiria mambo yafuatayo:
Mahusiano
Wewe huwatendeaje wazazi wako na ndugu na dada zako? Je, mara nyingi wewe hushindwa kujizuia unapokuwa nao, labda hata kuzungumza kwa ukali au kwa kejeli? Wao wangejibuje ikiwa wangeulizwa swali hilo kukuhusu? Jinsi unavyoshughulika na watu wa familia yako huonyesha jinsi utakavyomtendea mwenzi wako.—Waefeso 4:31.
Mtazamo
Je, wewe huwa na mtazamo mzuri au mbaya kuelekea mambo? Je, wewe hukubali maoni ya wengine, au nyakati zote wewe husisitiza mambo yafanywe kwa njia fulani—njia ile wewe unataka? Je, unaweza kuendelea kuwa mtulivu unapokabili hali ngumu? Je, wewe ni mwenye subira? Kusitawisha sifa za tunda la roho ya Mungu sasa kutakusaidia kujitayarisha kwa ajili ya kuwa mume au mke wakati ujao.—Wagalatia 5:22, 23.
Gharama
Wewe hushughulikia pesa kwa njia gani? Je, mara nyingi wewe hujikuta ukiwa na madeni? Je, unaweza kudumisha kazi? Ikiwa huwezi, sababu ni nini? Je, tatizo ni kazi yenyewe? Je, tatizo ni mwajiri? Au je, ni kwa sababu ya zoea au tabia fulani unayohitaji kufanyia kazi? Ikiwa ni vigumu kwako kushughulikia gharama zako mwenyewe, utashughulikiaje za familia yako?—1 Timotheo 5:8.
-----------------------------
Chanzo:www.jw.org/sw-maktaba
Kaka Ray! Ubarikiwe sana kwa kutochoka kupita hapa na kuacha yaliyo ndani ya moyo wako
ReplyDeleteAsante kwa wema wa moyo wako,maisha na mafanikio ndiyo kibarani kwetu.
ReplyDeleteBaraka kwako na familia pia.
Asante kwa wema wa moyo wako,maisha na mafanikio ndiyo kibarazani kwetu.
ReplyDeleteBaraka kwako na familia pia.
Kaka Ray! Hakika umenena Maisha na Mafanikio bila ninyi isingekuwa ilipo. Ahsante sana...
ReplyDelete