Mwaka 1998 tarehe 21/2 alizaliwa binti huyu. Ni siku ambayo familia hii haitaweza kusahau. Twamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote. Na twazidi kumwomba amwongoze binti yetu Camilla katika kila akifanyacho ili kiwe vema. Pia twamshukuru Mungu kwa kutuongoza sisi wazazi/walezi katika malezi ya binti Camilla. TWAKUTAKIA SIKU YAKO IWE NJEMA SANA. HONGERA Binti, dada, rafiki, mjukuu nk.
Nyumbani Ruhuwiko 2015...naenda kwa babu kuomba mboga (mandondo) maharage si mnaona eti nimechukua na bakuli yangu kabisa/Poti:-)
Keki nayo haikukosa katika kumbukumbu hii ya leo ya miaka 18....Duh mama sasa najiona ule uzee/utu uzima unazidi kupiga hodi. Haya karibuni tujumuike kumpongeza binti Camilla!!
Hongera sana sanaaaaa Mdogo wangu kwa kutimiza miaka 18, nakutakia maisha mema sana na yenye upendo mwingi daimaaaa!!!!
ReplyDelete- Mama hongera sana kwa kukuza.
Niandika kwa niaba kama nilivyotumwa...Kaka Baraka AHSANTE sanaaaa kwa kunitakia yote mema pia kwa upendo wako. Nami mimi mama Camilla nasema Ahsante sana.
ReplyDeleteKwa niaba ya wajomba wote, kuanzia wa-Nyasa, wa-Ngoni, wa-Matengo, na kadhalika, nampa hongera binti Camilla, na hongera kwenu wazazi.
ReplyDeleteHongera sana binti Camila. Kuanzia sasa uachane na mambo ya kitoto. By Salumu.
ReplyDeleteHongera sana kwa kukuza, mungu azidi kumuweka binti yetu Amin. Grattis Camilla.
ReplyDeleteHappy birthday Camilla
ReplyDeleteKwa niaba ya mtimiza miaka maana kaande shule:-
ReplyDeletemjomba Mbele Ahsante sana. Nasi wazazi twasema AHSANTE
Mjomba Salumu Ahsante Nitazingatia ushauri wako.
Usiye na jina wa 9:48AM Ahsante ndugu yangu. Naye Camilla nasema TACK SÅ MYCKET!
Mjomba Ntyangiri! AHSANTE.
Hongera sana tena mno.Ninakutakia maisha mema yenye baraka na upendo daima dawamu.
ReplyDeleteUsiyejulikana wa saa 9:28AM ahsante sana baraka zako. Nawe Uwe salama.
ReplyDeleteHappy Birthday Camilla,
ReplyDeleteushauri kwa wazazi mle likolo kwa wingi mtoto asiwapite urefu
hongera kwa kukuza
nilikupoteza zaidi ya mwaka nimekupata furaha ilioje
Usiye na jina wa 6:36PM! Kwa niaba ya Camilla nasema Ahsante...Umenichekesha mno eti tule likolo kwa wingi ili tusipitwe urefu na wanetu:-) Nasi wazazi twasema Ahsante kwa pongezi!....KARIBU TENA NA TENA SANA
ReplyDeleteHongera , Umekuza mdogo wangu
ReplyDeleteDada P.....Ahsante kwa kweli namshukuru Mungu.
ReplyDeleteHongera ya kuzaliwa tototoooooooo cammila.
ReplyDeleteUsiye na jina wa 9:15 PM! Kwa niaba ya dada Camilla Nasema ahasante sana.
ReplyDeleteHuyu bi mkubwa nilimtakia heri ya kuzaliwa lakini sioni ujumbe wangu au nilisahau kubonyeza kitufe cha publish your comment. Woooi basi mpe hongera zangu hata kama zimechelewa.
ReplyDeleteBi mkubwa kanituma kwa niaba nikushukuru mjomba Wake na kasema wala hujachelewa kabisaaa. Ahsante njomba:-)
ReplyDelete