HAPA NIPO NJOMBE
Mmmmhh! Miaka NANE leo imefika kama mchezo!!!!
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka Nane (8) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!.......... HAYA JUMANNE IWE NJEMA SANA KWA MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE
Nakupa pongezi la dhati kabisa da yasinta na inshallah itatimiza mara 10 zaidi ya hiyo. By Salumu.
ReplyDeleteKaka Salumu AHSANTE SANA kwa kuwa nami katika siku hii...KUFIKA MIKA KUMI TUMWOMBE MUNGU KAMA ULIVYOSEMA.
ReplyDeleteJitihada zako kama mtu binafsi zinastahili pongezi za hadharani bila kificho.HONGERA SANA MAU!!
ReplyDelete