Tuesday, July 21, 2015

MAWAZO MAKUBWA YA KUFIKIRISHA .....

Mvulana mmoja maskini alikuwa akiangalia gari la bwana mmoja ambaye alikuwa tajiri, tajiri alimchukua yule mvulani na kumwendesha katika lile gari. Mvulani  akasema una gari nzuri sana. Je? hili gari si ghali sana? Tajiri akamjibu, ndiyo ni ghali sana ila mimi nilipewa na kaka yangu kama zawadi.
Mvulana akawa anafikiri. Tajiri akamuuliza unawaza nini? Ebu ngoja, nawe unataka kuwa na gari kama hili eehh? Mvulana akamjibu HAPANA....NATAKA KUWA KAMA KAKAYAKO!!!

2 comments:

  1. Habari!
    Kweli hili ni wazo kubwa maana katika hali ya kawaida mwenye gari alitarajia kupatiwa jibu la kuwa anataka gari.
    Kwa kusema anataka kuwa kama kaka wa aliye na gari maana yake anataka kupata jinsi huyo kaka yake alivyoweza kuwa tajiri!




    ReplyDelete