MCHUNGAJI; "Unakunywa bia!?
MLEVI; "Ndio.
MCHUNGAJI; "Kwa siku
unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; "Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; "Bia moja bei
gani!?
MLEVU; "2500/
MCHUNGAJI; "Ulianza lini
kunywa bia!?
MLEVI; "Miaka 18
iliyopita!
MCHUNGAJI; "Kwa hiyo kwa
siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; "Ndio!
MCHUNGAJI; "Kama u gekuwa
unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range
Rover!?
MLEVI; "Samahani, naweza
kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; "Uliza!
MLEVI; "Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; "Hapana!
MLEVI; "Nionyeshe Range
Rover yako!
MCHUNGAJI; "Akakimbia..... |
Wednesday, March 25, 2015
UTANI KIDOGO- MLEVI NA MCHUNGAJI WAMEKUTANA!!
Ungana nami na utani huu nimeona si vizuri kupata elimu hii peke yangu ...nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio. KARIBU.....
Safi sana! Hapa ujumbe ni usihukumu kabla ya kujihukumu. By Salumu.
ReplyDeleteKUNA HII HAPA YA MWALIMU WA KISWAHILI NA MWANAFUNZI
ReplyDeleteMWALIMU: Sadiki tunda sentensi yenye neno SUKARI
MWANAFUNZI: Chai yaleo nitamu sana
MWALIMU: Sadiki sasa likowapi neno SUKARI?
MWANAFUNZI: SUKARI ipo ndani ya chai
by mikidizo
Kaka Salumu hakika umenena na hili huwa linatokea kila siku ya Leo. ...tunakuwa haraka sana kuhukumu wengine.
ReplyDeleteMikidizo! Kwanza kaeibu sana Maisha na Mafanikio. Ahsante kwa hii ama kweli nimecheka mno.
Hahaha!
ReplyDeleteSi umeona eeehh kaka Ray!
ReplyDeleteWatoto wawili watundu.
ReplyDeleteMtoto Mtundu wa Kwanza: Unajua chini ni wapi?
Mtoto mtundu wa pili: Wewe unajua juu ni wapi?
Mtundu wa kwanza:Juu si juu tu.
Wa pili: Chini si chini tu.
Mtundu wa kwanza: Ukiwa juu unaona chini.
Wa pili: Ukiwa chini unaona juu.
Mtundu wa kwanza :Kumbe juu na chini ni sawa?
Wa pili: Kwani mimi nawe ni sawa?
hakika hakuna siku nimecheka kama leo kaka Mhango umenichekesha mno ,,,,
ReplyDeleteDa Yasinta kicheko dawa. Cheka tu cheka sana tu. Nami nacheka na wakati mwingine naandima mambo ambayo hunichekesha.
ReplyDeleteKaka Mhango naendelea kucheka nawe cheka sana sana:-)
ReplyDelete