Friday, December 12, 2014

KUADIMIKA KWA MUDA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO/KAPULYA!!!


HAPA MIAKA MINNE ILIYOPITA.
KWA HIYO NA SASA TUTAWAHI KULIMA NA KUPANDA PIA KUTIA MBOLEA

Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwataarifu wasomaji wake kwamba haitakuwa hewani kwa muda.
Sababu kubwa ya kutokuwa hewani,  kuwa KAPULYA atakuwa SAFARINI ....Sio safari nyingine bali ya NYUMBANI-TANZANIA.
Nitajitahidi kuwataafu mawili matatu. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE PAMOJA DAIMA. NAWATAKIENI WOTE CHRISTMAS JEMA NA MWAKA MPYA 2015. TUTAONANA.
SI VIBAYA KAMA TUKIMALIZIA NA KIPANDE HIKI CHA MZIKI....

KILA LA KHERI

12 comments:

  1. Safari njema .mungu akufikisheni na awarudishe salama Inshaallah.

    ReplyDelete
  2. Inshaallsh mama Wane...ahsante kwa sala...

    ReplyDelete
  3. Safari njema Dada yangu,Mwenyenzi Mungu awatangulie katika safari yenu.Nawatakieni wote sikukuu njema.

    ReplyDelete
  4. Safari Njema Da'. Majaliwa tutaonana utakaporudi.

    ReplyDelete
  5. Naomba sana Dada upitie kutusalimia Mafinga.....maana ndo barabara moja.

    namba yangu ni; 0767-191275.
    Nitafurahi sana kukuona.

    ReplyDelete
  6. Da Yasinta
    Nenda na rudi salama.
    Noeli njema na heri ya mwaka mpya.Bila kusahau kukupa wosia. Nenda nyumbani ule kila kitu ila usile vingi kama hiyo nguna hapo chini. Utaongeza uzito na kujikuta ukihangaika kuupunguza usiweze hasa ikizingatiwa kuwa maisha yetu pande hii yanategemea sana mashine tofauti na nyumbani ambapo mwili ni mashine bora ya usafiri. Ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  7. Nyumbani ni nyumbani japo..............................

    ReplyDelete
  8. Manka! Tulisafiri salama na tumerudi salama Ahsante kwa sala.

    Serina:- Tack nu är vi hemma i Sverige.

    Kaka Baraka...Ujumbe nimeupata ila nilishindwa kupita hapo Mafinga utanisamehe.

    Mwl. Mhango..Nimeenda na nimerudi salama..Na nimekusoma na ujumbe nimeupokea na wala usihofu uzito umepungua:-)
    Kaka Ray! ni kweli nyumbani ni nyumbani hata kama ni porini:-)

    ReplyDelete
  9. Nakutakia heri wakati wa likizo,
    Hilo shamba nimelipenda , limenikumbusha mbaliiiii sana

    ReplyDelete
  10. Dada P! Likizo ilikuwa njema kabisa....mtoto wa mkulima ni mkulima pia si unajua...

    ReplyDelete