Tuesday, August 19, 2014

BUSTANI YETU INAVYOENDELEA SIJALIMA MBOGA MBOGA TU NIMALIMA NA.......

 Mahindi na sasa yamechanua ila nina wasiwasi kama nitakula maana bado hayajabeba :-)
 Kule kwetu Litumbandyosi tunalima sana Karanga kwa hiyo nikaona niendeleze kilimo..
 Na kulima mboga bila kiungo/pilipili si safi sana na hapa nilijaribu na matokeo yake ni kama muonavyo.
..na bila kusahau nyanya  nazo sasa ndo zinaanza kuiva na tumeshaanza kula...kazi ya mikono yangu/yetu mwenyewe/wenyewe.

10 comments:

  1. Hongera saaana dada yangu. Yaani juhudi ukiwa nazo na matunda yanaonekana

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Dada Yasinta,na mimi mwaka nilifuata nyayo zako nimelima mchicha,sukumawiki,kunde,nyanya,hoho na zimestawi sana.

    ReplyDelete
  3. Manka nafurahi kusikia haya yote HONGERA SANA...NATAMANI KUINA BUSTANI YAKO...NA HIZO KUNDE NI KUNDE ZA AINA GANI? MAANA KUNA KUNSW ZA AINA NYINGI

    ReplyDelete
  4. Huu ndiyo wakati wa kumtembelea dada wa mimi...KADALA...Niwekee na mimi...

    ReplyDelete
  5. Mama Alvin ahsante....ni kweli matunda twayaona.....karibu..

    KACHIKI...YAANI USIHOFU YAANI HATA KESHO NJOO...

    ReplyDelete
  6. Hungera sana dada. Ubarikiwe! By Salumu.

    ReplyDelete
  7. Asante Dada Yangu,sikujua kama kuna kunde tofauti tofauti,mbegu zake ni ndogo kama za choroko ila zina rangi kama brown hivi.Nitakutumia picha uone

    ReplyDelete
  8. Kaka Salumu ...ahsante sana na karibu kuja kuvuna.
    Manka ndugu yangu nitafurahi kuona hiyo picha ya kunde.

    ReplyDelete
  9. Namie mwakani Inshaallah nitapanda.yaani umenifanya nitamani na kujutia muda wangu sama yote hii hata mchicha?Ubarikiwe sana dada yangu.Nafarijika sana kuingia humu.inanipunguzia home sick.
    Mama Wane.

    ReplyDelete
  10. Mama Wane ...nami unanipa moyo zaidi..nakutakia kila la kheri ndugu yangu!!!

    ReplyDelete