Thursday, August 21, 2014

KISWAHILI:- METHALI ZETU!!

1. Usimwamshe aliyelala, utalala wewe.
2. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
3. Usitukane mkunga na uzazi bado.
4. Uso mzuri hauhitaji urembo.
5. Vikombe vikaka pamoja havina budi kugombana.
6. Waraka ni nusu ya kuonana.
7. Wagombanao ndio wapatanao.
8. Usiache mbachao kwa msala upitao.
9. Mchumia juani, hula kivulini.
10. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
Ni hizi tu kwa leo ila nawe kama una mojo, mbili tatu usisite kuweka hapa eilimu ni kugawana. Haya siku na kazi njema . Wenu Kapulya:-)

10 comments:

  1. Kuna Muhindi aliambia akamilishe methali:

    Alijibu hivi:

    1. Usipoziba ufaa.....miji tachungulia dani!
    2. Simba mwenda kimya.....iko gonjwa, kama siyo gonjwa kanisi!
    3. Mtaka cha uvunguni.....sogeza tanda!
    By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Kaka Salumu wewe yaaani nimecheka mpaka hoi hapa..Duh!! kaaaaazi kwelikweli...Ahsante sana kupita hapa na kuacha hili

    ReplyDelete
  3. Da Yacinta acha nikupe moja hapa. Simbuliko halisimbuliki ila kwa mikukuliko.

    ReplyDelete
  4. Kaka Mhango...nimeikubalu hii...ahsante sana!!

    ReplyDelete
  5. Da Yacinta ngoja nikupige nyingine. Atangazaye mirimo si mwana wa ruwari. Nadhani na hii utaipokea na kuikubali au vipi?

    ReplyDelete
  6. Nimeikubali na kuipokea kakangu...ahsante sana !!

    ReplyDelete
  7. Kiswahili lugha ya ajabu. Nimesoma nikajiuliza ameikubali au kumpiga nini hapo juu bila kuelewa kitu.

    ReplyDelete
  8. na hii jee
    Pema usijapo pema ukipema si pema tena.
    Sijui nimeipatia.
    Mama Wane.

    ReplyDelete
  9. Mmmhh.... hii kwangu ni mpya..ahsante nitaituza!!! Ni mchabgu nzuri

    ReplyDelete
  10. vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg

    ReplyDelete