Tuesday, August 12, 2014

BAADA YA KUWA LIKIZO .....BUSTANINI/ MBOGA YA MABOGA IMEFUNGA/STAWI MNO:-)

 Nikaona niichuma kama muunavyo hapa na kuifanyia kazi ...nikapata kiasi hiki. Basi nikaichambua .....
 ....nikaikatatakata  kama muonavyo katika picha , wakati huo nishaweka maji katika sufuria ...
 ...ipo ndani ya sufuria ili ishemshwe kwa muda wa dadika 2-5
 na hapa baada ya dakika 2-5 inaonekana hivi, baada ya hapa nasubiri ipoe na halafu
...naiweka katika mifuko kwa ajili ya akiba  na pia naandika tarehe na ni mboga aina gani, baada ya hapo ni kuweka kwenye friza(freeze) ...mjanja  eehhh:-)

13 comments:

  1. Yaani mjanja mnoooo...dah nimetamani dada uwiii....kwenye friji zitakaa kwa muda gani? hongera sana kwa kulima

    ReplyDelete
  2. Mama A! ahsante kupita hapa na kuacha yako ya moyoni...Kwenye deep frriza itakaa hata miaka ndugu yangu:-)

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Kadala..Mhhh nimeitamani sana....

    ReplyDelete
  4. oooh asante sana dada kwa maujuzi......

    ReplyDelete
  5. Dada yangu umenitamanisha na mboga ya maboga.Naomba kuuliza je naweza kuifadhi mboga ya mchicha kwa njia hii??Asante

    ReplyDelete
  6. Manka ndugu yangu haswaaa unaweza hata kusamvu pia tembile na kadhalika. Nilikumissije!!!

    ReplyDelete
  7. Yay..asante sana nitafanya hivyo.Nami nilikumisi Dada yangu

    ReplyDelete
  8. Habari yako Dada Yasinta.naomba kukuuliza kwani kuna mbegu za kuvuna majani ya maboga tuu bila kuota maboga.au ni yale yale ya maboga ndio mnavuna majani yake. msinicheke jamani nataka kujua na tena ni mgeni humu.
    Mama wane.

    ReplyDelete
  9. ndugu yangu mama wane...kuuliza si ujinga. Hizi mbegu nilipewa na mama yangu wa hiari Njombe ni mbegu nyeusi mara nyingi hustawi na kuvumilia hali ya hewa ya ubaridi kama ile ya Njombe, Iringa, Makambako na pia niliishi Madaba_Matetereka. Huwa hayawi mabogo ni mboga tu. Na zile mbegu zitoazo mabogo hapa hazistawi sana hii ndiyo sababu kubwa.

    ReplyDelete
  10. ahsante dada yasinta kwa kunijulisha.samahani nimechelewa kushukuru watoto walinipelekesha kidogo.Mimi nipo Canada ,naona hizo mbegu zitanifaa.nitaziagiza Dar kama zipo.
    Mama Wane.

    ReplyDelete
  11. Mama Wane....Unaweza kuniagiza nitakwenda nyumbani karibuni ukitaka.. ..si unajua maisha kusaidiana...

    ReplyDelete
  12. nimeitamanije na hasa inavyopikwa kiusafi

    ReplyDelete
  13. Kaka Mwangoka! Usitamani tu Karibu nimekuwekea!

    ReplyDelete