Wednesday, July 9, 2014

LEO TUANGALIE BAADHI YA MISEMO NA METHALI TOKA TANZANIA

1. Mtoto wa kwale hapotezi njia yake (Kibena)
2.  Mtoto wa nyoka hukua na sumu yake (Kisambaa)
3. Mtoza ushuru sokoni huvumilia (Kichaga)
4. Mtu hodari husifiwa na watu (Kizigua na kinguu)
5. Mtu si sikio (Kiiraqw)
6. Muwa mmoja haujazi mtungi (Kipare)
7. mvua ya vuli imeanza (Kinyakyusa)
8. Mwanamke ni kambalemamba huamshwa na mkuki  (Kikerewe)
9. Ukiona mishale nyanyo ziko nyuma (Kimasai)
10. Kucheka hakuna majira, chenya majira ni kilimo (Kiha)
11. Tumbo la nguruwe halipasuliwi mbele ya watoto (Kisukuma)
12. Wazee walimtoa nyoka katika pua ya mwene (Kifipa)
KAMA NAWE UNA CHA NYONGEA KARIBU SANA SI MNAJUA  TUPO PAMOJA.....JUMATANO NJEMA SANA KWA WOTE..PANAPO MAJALIWA .  KAPULYA

4 comments:

  1. Utamaduni wetu umejaa misemo yenye busara na hekima nyingi. Tuutunze :)

    ReplyDelete
  2. Eeehh kaka Bwaya kumbe upo ni furaha ilioje kujua hili. Ni kweli ulichosema na tusisahau kuwasimulia kizazi kijacho

    ReplyDelete
  3. Hii ya mwanamke kuamshwa na mikuki si atakufanya bure? Huu si ukatili jamani? Kama wawama wataamshwa na mikuki mijibaba sitaamshwa kwa mibomu?

    ReplyDelete
  4. So sad hii mithali haitendewi kazi na inabaki kufundishwa tu darasani na kukaririshwa bila uelewa wowote. Leo watu washasahau hizi mithali na hata kama ni kukumbuka ni zile fupi fupi tu za sharti uiname au asiyesikia la mkuu. Labda kila mtu angezijua zote kwa uelewa mzuri zingesaidia hata maovu kutotendeka au hata kupungua kama zinavyo shamiri sasa hivi.

    ReplyDelete