Sunday, January 12, 2014

JUMAPILI YA LEO HALI YA HEWA ILIKUWA HIVI, KWANGU MIMI NAWEZA NIKASEMA HALI YA HEWA IMECHAFUKA.....BARIDI -10C...HAPA BAADHI YA PICHA NILINASA LEO

 Kuanzia jana asubuhi mpaka leo bado theluji inaanguka tu ebu angalia hapa ukiangalia kwa makini sana kushoto kwako ni lile enoa ambalo tumezoea kuiona bustani ya Kapulya lakini sasa mmmhhh! haiwezekani kabisa ....hata hivyo ni lazima kutoka nje ingawa ni -10C huko nje....angalia hapa ....

 ...hapa tupo nje ni siku ya wazazi na watoto wao kuwa nje kwa vile ni siku maalumu kwa darasa la binti yetu. Ni kwamba wamepata na wageni kutoka Colombia kutokana na darasa lake kusoma lugha ya spanish wao walikuwa kule Colombia mwaka jana na sasa waColombia wamefika hapa  juzi. Kwa hiyo wazazi na watoto ni jambo la muhimu kuwapokea wageni na kuwaonyesha nini kufanya...ila duh! wameshangaa kwani ni baradi mno ...hata hivyo wanafurahia hali hii.
Mama maisha na Mafanikio alivovalia tayari kwa kupambana na baridi ya leo lakini, wee bwana haikuwa joto vidole vilikufa ganzi kabisa  hata kama ningeenda kwa daktari na kuchomwa sindano nisingesikia maumivu...Si ajabu kuonekana kama tembo maana mtu unajitahidi  kuvaa nguo nzito ila kuepukana na baridi.....Hiii ndio JUMAPILI YANGU YA LEO..PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE.


10 comments:

  1. Pole da Yasinta na baridi ya huko! Lakini si wana gongo yao inayoitwa vodka, ukinywa kidogo itakusaidia. By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Hahaaaa kaka Salumu!...hiyo vodka mbona ntakauka...nakunywa CHAI . Ahsante kwa pole...maana miguu yangu bado imeganda mpaka sasa...

    ReplyDelete
  3. Pole sana shemejiiiiii.... Tuliopo Dar tunakomaa na joto la 37c

    ReplyDelete
  4. Shem Kajuna ! Kheri na joto waweza kupunzika kivulini pia kwensa baharini na kytoa jasho...

    ReplyDelete
  5. Huku nilipo joto kama hilo ni la kufanya mazoezi. Kwani tunakwenda hadi -40C ukiongoza na windchill wakati mwingine tunajikuta kwenye -70C

    ReplyDelete
  6. Mwal. Mhango, umenichekesha..labda niharibu kesho kukimbia. Ila duh -40C ni baridi kali hadi pua inaungua..na hiyo -70C mnatoka nje kweli?

    ReplyDelete
  7. Hiyo -70 C ni kujumlisha na windchill lakini bado tunatoka. Unachumpa toka kwenye nyumba na kuingia kwenye gari vinginevyo huwezi kuhimili zaidi ya dakika kumi kabla hujaganda. Pia miili yetu inaanza kuzoea kutokana na mavazi na vyakula tunavyokula. Huwezi kuamini kifaru changu kinatumia mara mbili ya mafuta zaidi ya kawaida yake kutokana na ku-iddle na kutumia mkaa wa mchina kwa sana. Wajua kifaru chenyewe nipendacho kutumia ni Toyota Yaris?

    ReplyDelete
  8. Duh! Ama kweli maisha haya kaaazi kwelikweli..yaani napata picha ya hiyo -40C maana hapa kusini ni hali hiyo...na mwaka mmoja ilikuwa hapa nilipo eehh bwana weeeh pua iliganda na mikono ndo kabisa na nikahisi sina vidole vyote vya miguuni na mikononi...kwa hiyo kwa mtindo huo vyakula inabidi viwe vya mafuta mafuta zaidi au?

    ReplyDelete
  9. Yes inabidi ule mafuta ila uwe makini ni aina gani na kiasi gani vinginevyo utanenepa na kuanzisha balaa jingine. Tunajitahidi kunywa vitu vya moto na kukaa ndani ili kuepuka kubukanya. Huku watu kufa kutokana baridi ni jambo la kawaida hasa kwa wale wanaojikuta kwenye mazingira kama vile ajali ambapo msaada unachelewa au kutofika kabisa.

    ReplyDelete
  10. Najua Mwal. Kula mafuta ovyo na hasa aina isiyotakiwa unaweza kuvimba kama tembo na kujitafutuia mengine. Hivi niwapi Upo?..Huko naona nikija nitakauka kabisa..Ila kwa vile napenda chai sana ningestahimili...Alo poleni sana!!

    ReplyDelete