Ukiwa MTEMBEZI utafaidi mengi ..jana nilitembela hapa na nikakutana na wazo hili ambalo nimelipenda sana na nikaona kwa nini lisiwekwe hapa Maisha na Mafanikio ..Haya karibu!!
WAZO LA LEO: Maisha yana mitihani yake, ukiona kwako
ni kugumu, ujue kuwa kuna wenzako kwao ni kugumu mara mbili yako, ukipatwa na
mitihani ka hiyo...usikate tamaa, pambana, ukijua kuwa wewe sio wa kwanza kupata
mitihani kama hiyo, wapo waliopata mitihani hiyo na wakaishinda, kwanini wewe
usiweze...kumbuka baada ya dhiki, mara nyingi ni faraja.
BONGE LA WAZO ....JUMAMOSI NJEMA SANA
Da Yasinta, nimeukubali hilo wazo la mtihani. Hapa duniani tunaishi na mitihani mingi sana. Hekima, busara na uvumilivu ndio utakao kuvusha kwenye lindi la mitihani. By Salumu.
ReplyDeleteWazo zuri na limeenda shule,ni yangu matumaini umzima wa afya wewe pamoja na familia yako mtani wangu.
ReplyDeleteJumamosi njema kwako pia.
Kaka Salum! Ahsante kwa kukubali wazo hili.
ReplyDeleteEdna wa mimi karibu tena maana uliadimika :-) wala usihofu tupo salama na ninaamini huko pia ni salama.