Ijumaa ya leo itakuwa kuku ambayo ni:- kuku mzima, viazi, karoti, kitunguu, kitunguu saumu, tangawizi, nyanya kopo, binzari, mafuta, chumvi na maji..... Picha zaidi zinakuja baada ya muda tu....Kwa hiyo mnakaribishwa kujumuika nasi.
Na hapo ndivyo ilivyoonekana sahani yangu...wali, kuku, kiazi, karoti na mboga majani /figili ambayo imeliwa na mikono yangu mwenyewe......Karibuni chakula kipo kingiiiii kweli. Jioni njema sana na panapo majaliwa tutaonana tena kesho.
Mmmhhhh..Tamu saana,Asante.
ReplyDeleteKachiki, kipo bado kingi tu karibu, karibu, karibu sana
ReplyDeleteMwanamke mapishi babuee!! Mungu aubariki mkono wako dada Mkuu!
ReplyDeleteJamani jamani mie hicho chakula cha leo kinaonekana ni kitamu sana sana! Hongera kwa mapishi safi na yenye ladha. Siku ipo ntafika hapo kwako kuonja mapishi yako. Na hiyo kuku na figili jamani vilivyo vitamu.
ReplyDeleteduh... huo msosi unaonekana ni mtamu kweli... mi niko njiani hivyo tena..
ReplyDeleteUMENITAMANISHA!
ReplyDeleteDada Mkuu msaidizi! Unena..Ahsante.
ReplyDeleteUsiye na jina....Nakusubiri kwa hamu kweli kweli..Ahsante sana.
Kaka wa mimi Mrope! Msosi ulikuwa mtamu mno ila nasikitika sikuwa na ugali:-( Twakusubiri karibu kaka.
Dada P! Karibu sana chakula kipo kingiiii.