Monday, November 18, 2013

HABARI NJEMA:- NI KWAMBA LEO NIMEPATA UNGA WA MAHINDI:- LEO MLO UGALI NA MBOGAMBOGA:-)!!!

Habari za wikiendi ndugu zanguni...kama mnakumbuka vizuri niliwaambia kuwa niliishiwa unga wa ugali. Sasa katika kutafuta tafuta nimepata kama muonavyo katika picha. Unga ni mweupe kama wa mahindi ya nyumbani. Huu unatoka Venusuela...Haya sasa karibuni kula ugali:-) NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMATATU!!!

5 comments:

  1. Da Yasinta. Huo unga mfuko una kilo ngapi? Na unanunua bei gani? Maana kama Venezuela wanaweza kuuza Sweden, vipi TZ ishindwe! By Salumu.

    ReplyDelete
  2. usitukaribishe nguna, tukaribishe ugali

    ReplyDelete
  3. Asante sana Yasinta kwa kujali made in Tanzania.Changamoto hapa ni jinsi ya kutangaza bidhaa za Tanzania huko ughaibuni.Unga wa nafaka mbalimbali unapatikana na jukumu watanzania kuwashawishi wafanyabishara wa huko ughaibuni jinsi wanavyoweza kunufaika na bidhaa kutoka Tanzaia.Unaposema unaipenda Tanzania lakini huchangii uchumi wake katika kupromoti mazao yake ughaibuni unamaanisha nini????

    ReplyDelete
  4. Kaka salumu huo ni mfuko wa kilo moja kwa mahesabu ya haraka haraka inaweza kuwa kama elfu saba vile.....Kaka Mkuu Mwaipopo duh! karibu sana sana yaani nilikumiss kweli wala usiwe na wasiwasi utapata UGALI KAKANGU:-)

    Tanexa karibu sana katika kibaraza hiki...Na ahsante kwa mawazo mazuri.

    ReplyDelete