Saturday, April 27, 2013

JUMAMOSI YA LEO TUANGALIE VITENDAWILI VYETU...KITENDAWILI.....

Kwanza nina swali moja hivi kwa nini tunasema KITENDAWILI....na wengine wanajibu...TEGA..???? HAYA KITENDWILI...
1. Huyu mwanamume, huyu mwanamke, hwakutani...
2, Mtoto wangu ninapomtuma mmoja, wanarudi wengi.
3. unga wa kuanika usiku, mchana hakuna.
4. Shamba langu kubwa, ulezi nivunao kiganja kimoja
5. mtu mwenyewe mdogo, watoto wengi.

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NASUBIRI MAJIBU:-)

12 comments:

  1. Yaani kaka Said ni kweli...je umejua kitendawili kimoja?

    ReplyDelete
  2. Hapo najaribu dada Yasinta, jibu la swali NO.2 ni "KARANGA" au "MHINDI" nikiwa na maana karanga na mahindi huoteshwa kama mbegu na hapo baadae zao lake huvunwa likiwa na punje nyingi. Jibu la swali NO.4 ni "NYWELE ZA KICHWANI" nikiwa na maana zina wingi mkubwa lakini zitakaponyolewa ni fungu dogo na jibu la swali NO.5 ni "KIBIRITI" nikiwa na maana kibiriti ni boksi dogo ambamo ndani yake kuna njiti nyingi. Ahsante kwa maswali yako na naomba nisahihishwe nilipokosea.

    ReplyDelete
  3. Kaka Said ngoja kidogo kana kuna nwingine anaweza kutoa majibu tofauti nawe. ..hakika nimefurahi kusoma maoni yako:-D

    ReplyDelete
  4. Hii nayo kali.... nimeishia kucheka tu

    ReplyDelete
  5. Mie niliambua moja la nywele wakati nakaribia kupata majibu yote si nikaona hayo majibu hayo hapo juu. Hata hivyo inaburudisha na kufikirisha.

    ReplyDelete
  6. HAYA WAPENDWA NAONA NIWAPE MAJIBU....
    1. Vilima viwili
    2. Mtama
    3. Umande
    4. Nywele
    5. Funza

    kaka Said na mwl. Mhango mepatia ..namba nne Nyweli makofi waaaaaa wwaaa waaaa..ahsanteni..inabidi tuwe na somo hili kila wik ili tusisahau..

    ReplyDelete
  7. kitendawili... ni cheupe kama barafu na ni cheusi kama giza kuliwa ni haramu na kunywa na halali kina herufi tano kinaanza na M kinatumiwa na wanaume mara tatu kwa sikun awanawake mara moja katika umri wao je ni kitu gani hicho?

    ReplyDelete