1. Usijilaumu kwa lolote lililokutokea
2. Usihofu kuhusu hali uliyo nayo sasa.
3. Usijilinganishe na mtu yeyote duniani.
4.
6. Usiwaze sana kuhusu kesho waza kuhusu leo.
7. Kukikosa ulichokikusudia yote ni mipango ya Mungu.
MUWE NA SIKU/JUMAMOSI NJEMA
KABISA DADA YASINTA, UMENENA.....UJUMBE WAKO NI MZURI NIMEUPENDA!
ReplyDeleteNi kweli Yasinta. Mungu atusaidie mana kwa akili za kibinadamu ni ngumu sana kuepukana na hayo, ila kwa uwezo wa Mungu tunaweza na kushinda. Ubarikiwe sana na ujumbe huu mzuri sana na wa kutia moyo.
ReplyDeletemaneno mazuri sana mimi peke yangu hapa sijiamini sijui ni kwa nini sijui ni malezi au nini najiona niko down saa zote sijui kwa nini
ReplyDeleteAsante sana KADALA kwa ujumbe mzuri....J'Mosi iwe njema kwako na familia pia.
ReplyDeleteDa Yacinta mimi sikubaliani kabisa nawe. Kwanini kumsingizia Mungu hata kwenye upuuzi? Hivi wabakaji, mafisadi, wauaji, wababaishaji na watenda maovu wote ni mpango wa Mungu? Ingekuwa hivyo basi asingetoa amri kumi. Kwa ufupi ni kwamba alipopewa akili tofauti na wanyama, mwanadamu alianza kuwajibika kwa matendo yake. Nitatoa mfano toka nyumbani. Hivi kweli umaskini wa watanzania ni mpango wa Mungu au wa kutengenezwa na binadamu waroho na wenye roho mbaya wasioona mbali? Hamuwezi kupewa raslimali zote hizo na Mungu halafu akajipinga. Tafakarini upya jamani.
ReplyDeleteYasinta siku hizi huchangii comments, ukishaandika hiyo mada ndio basi. Upo lakini?
ReplyDeleteNdugu zangu ahsanteni kqs mchango wenu...tupo pamoja...
ReplyDeleteUsiye na jina wa 2:05 pm sio hivyo michakato ni mingi tu ila nipo