Saturday, November 10, 2012

JUMAMOSI YA LEO NAPENDA KUSEMA:- AHSANTE MAMA MUNGU AKUPE KHERI DAIMA!!!

 
AHSANTE MAMA MUNGU AKUPE KHERI DAIMA
 
Nimeyapenda maandishi haya kwenye kanga hii na hapa si kwa ajili ya mama yangu tu nawaombeni wote ambao mnaweza kuwashukuru akina mama basi chukueni nafasi hii na kuwashukuru kwani
HAKUNA KAMA MAMA. JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!! NIPO  NANYI!! 

 

6 comments:

  1. Ahsante kwa kutukumbuka, mungu akupe amani siku zote


    ReplyDelete
  2. Hakika mama ni dhahabu isiyoisha thamani!

    ReplyDelete
  3. Dada P.. Ahsante kwa kuungana nami na pia kwa baraka.

    Kaka Ray.. Nimependa msema huo ...na ni kweli mama ni mtu muhimu sana na hakuna kama mama.

    ReplyDelete
  4. Hiyo misemo ingekuwa inathaminiwa kwa vitendo kwenye jamii zetu, basi kusingekuwa na ukandamizwaji wa haki za akina mama au manyanyaso ya akina mama.

    Sijawahi kuona misemo ya kuwasifia akina baba, lakini ndio wenye final say kwenye jamii. Inasikitisha sana, nahisi akina baba huwa tunatumia ubabe kudai haki zetu hata pale ambapo hatuna haki.

    Mtu anapokuwa kwenye hatari, akipiga kelele utasikia, "Mama yangu weeee!" au "Mungu wangu!". Sijawahi kusikia mtu akisema "Baba yangu weee!"

    Mauaji ya Kimbari yalipotokea, akina Baba walitimka na kuacha wake zao na watoto wao. Akina Mama hawakukubali kuacha watoto, walikuwa tayari kufa pamoja na watoto wao, kuliko kuacha watoto peke yao. Kauli za "Mama yangu weee!" pindi tunapokuwa kwenye ajali/hatari, huwa ni reflection ya hayo hapo juu, ukimwita mama anaweza kuja kukuokoa au akawa tayari kufa na wewe, lakini ukimwita baba, inaweza kula kwako, maana by the time unamwita anaweza kuwa alishatoka unyoya na yuko mbali sana.

    Sijui ni connection ya kukaa matumboni mwa mama zetu kwa miezi 9 ndio huwa inasababisha haya? Pamoja na akina mama kutuzaa kwa uchungu?

    Mungu adumishe upendo wa akina mama kwa watoto wao, maana sote hapa duniani tulizaliwa na akina mama!

    ReplyDelete
  5. Mtani! Hakika umenena..naweza kukubali nawe au niseme naweza kujibu haya maswali yako ni kwamba upo sahihi kabisa kuwa ni sababu ya kulea mimba miezi 9 na pia tunapozaliwa mama huwa nasi kila wakati na pia hupata chakula toka kwake...Hakuna kama mama...

    ReplyDelete
  6. KWELI HAKUNA KAMA MAMA NIHIYO KUKAATUMBONI KWAO MAANA MAMA NI MAMAKWELI LAKINI BABA Mhhhhhhh......pengine kasingiziwa

    ReplyDelete