Monday, November 12, 2012

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI ...JUA...!!!

Sikumbuki ni lini nimeona jua likichomoza kama hili hapa. Au sijui linazama hapa? kama ule wimbo wa mchaka mchaka.....Jua lile litelemke mama ...litelemke mama litelemke....mmmhhh ila hapa naona linachomoza angalia tu mionzi yake,,,au Wenzangu mnasemaje?...Haya JUMATATU NJEMA...!!!

3 comments:

  1. Nguvu za Kuumba—“Aliyezifanya Mbingu na Nchi”
    ==============================
    Huenda unajua kwamba jua letu ni nyota. Jua huonekana kubwa kuliko nyota tunazoona usiku kwa sababu liko karibu sana kuliko nyota hizo. Lina nguvu nyingi kadiri gani? Kipimo cha joto kwenye kiini cha jua ni nyuzi Selsiasi 15,000,000 hivi. Kama ungeweza kuchukua kipande cha kiini cha jua kinachotoshana na kichwa cha pini ndogo na kukiweka duniani, ungeteketea hata ukiwa umbali wa kilometa 140 kutoka kwenye chanzo hicho kidogo sana cha joto! Kila sekunde, jua hutoa nishati inayolingana na mlipuko wa mamia ya mamilioni ya mabomu ya nyuklia.
    Jua ni kubwa sana hivi kwamba zaidi ya dunia 1,300,000 zinaweza kutoshea ndani yake. Je, jua ni nyota kubwa kupindukia? La, wataalamu wa nyota husema kwamba jua ni nyota ndogo sana yenye mwangaza hafifu. Mtume Paulo aliandika kwamba “nyota hutofautiana na nyota kwa utukufu.” (1 Wakorintho 15:41) Paulo hakuweza kuelewa kabisa maneno hayo ya Mungu. Kuna nyota moja kubwa hivi kwamba ikiwa ingewekwa mahali lilipo jua, basi ingefika ilipo dunia yetu. Endapo nyota nyingine ambayo ni kubwa sana ingewekwa lilipo jua, ingefikia sayari ya Zohali—japo sayari hiyo iko mbali sana na dunia hivi kwamba roketi ya angani ilisafiri kwa muda wa miaka minne ili kufika huko. Mwendo wake ulizidi mara 40 mwendo wa risasi inayofyatuliwa na bunduki yenye nguvu!
    Lakini idadi ya nyota inastaajabisha zaidi ya ukubwa wake. Kwa kweli, Biblia inasema kwamba nyota haziwezi kuhesabiwa, kama vile “mchanga wa bahari” usivyoweza kuhesabiwa. (Yeremia 33:22)Maneno hayo yanadokeza kwamba kuna nyota nyingi sana ambazo hatuwezi kuona pasipo vifaa maalumu. Endapo mwandikaji wa Biblia, kama Yeremia, angetazama angani wakati wa usiku na kujaribu kuhesabu nyota zionekanazo, angefaulu kuhesabu nyota zipatazo 3,000 hivi. Wanadamu huweza kuona idadi hiyo tu ya nyota katika anga jangavu la usiku bila kutumia vifaa maalumu. Idadi hiyo yaweza kulinganishwa na idadi ya chembe za mchanga zinazoweza kujaza kiganja kimoja tu cha mkono. Hata hivyo, idadi halisi ya nyota haijulikani, ni nyingi kama mchanga wa bahari. Ni nani awezaye kuhesabu idadi kubwa hivyo?
    Andiko la Isaya 40:26)linajibu hivi: “Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina.” Zaburi 147:4) yasema: “Huihesabu idadi ya nyota.” “Idadi ya nyota” ni ngapi? Hilo si swali rahisi. Wataalamu wa nyota wanakadiria kwamba kuna zaidi ya nyota bilioni 100 katika kundi letu la nyota la Kilimia peke yake. Lakini kuna makundi mengine mengi mbali na kundi letu, ambayo yana nyota nyingi zaidi. Kuna makundi mangapi? Baadhi ya wataalamu wa nyota wamekadiria kwamba kuna makundi bilioni 50. Wengine wamekadiria kwamba kuna makundi yapatayo bilioni 125. Kwa hiyo, mwanadamu hawezi hata kujua idadi ya makundi ya nyota, sembuse kujua idadi kamili ya mabilioni ya nyota zilizomo. Lakini, Yehova anajua idadi yake. Isitoshe, yeye huipa kila nyota jina lake!
    Tunakuwa na kicho zaidi kwa Mungu tunapotafakari juu ya ukubwa wa kundi moja la nyota. Kundi la Kilimia limekadiriwa kuwa na upana wa kipimo cha miaka 100,000 cha mwendo wa mwanga. Hebu wazia mwali wa mwanga unaosafiri kwa mwendo wa kasi sana wa kilometa 300,000 kwa sekunde. Ingechukua mwali huo miaka 100,000 kuvuka kundi letu la nyota! Na makundi fulani ni makubwa zaidi ya Kilimia. Biblia inasema kwamba Yehova ‘amezitandika mbingu’ hizi pana kana kwamba ni pazia tu. (Zaburi 104:2)Pia anapanga mizunguko ya sayari na nyota alizoumba. Kila kitu kinazunguka kupatana na sheria za asili ambazo Mungu ametunga na kutekeleza, kuanzia chembe ndogo sana ya vumbi lililo angani hadi kundi kubwa zaidi la nyota. (Ayubu 38:31-33)Ndiyo sababu, wanasayansi wamelinganisha mizunguko barabara ya sayari na nyota na miendo hususa ya wachezaji-dansi wenye utaratibu wa hali ya juu! Basi fikiria Muumba wa vitu hivyo vyote. Je, hustaajabishwi na Mungu huyo mwenye nguvu nyingi hivyo za kuumba?


    ReplyDelete
  2. juahilo literemke mama tanganyika ipate pandajuuuuuu......... upo hapo mdada umeamka salama huko?

    ReplyDelete
  3. Kaka Ray! Ahsante kwa neno.

    Usiye na jina! umenifanya nitabasamu kwa kutunga wimbo mzuri kuhusu Tanganyika..Mie nipo hapa na nimeamka salama ila sijaona jua...

    ReplyDelete